Kardinali Parolin katika kongamano kuhusu sura ya Kardinali Silvestrini aliyekuwa mwanadiplomasia wa Vatican nchini Italia. Kardinali Parolin katika kongamano kuhusu sura ya Kardinali Silvestrini aliyekuwa mwanadiplomasia wa Vatican nchini Italia.  (ANSA)

Katibu wa Vatican:Kardinali Silvestrini,sanaa ya diplomasia kwa umoja

Katibu wa Vatican alizungumza tarehe 27 Oktoba 2023 katika kongamano lililowekwa kwa ajili ya Kardinali Silvetrini baada ya miaka 100 baada ya kuzaliwa kwake, liyoandaliwa huko Campidoglio Jijini Roma:Alitafsiri diplomasia kama chombo cha kuchanganya matarajio ya roho na yale ya ukweli wa maisha ya watu

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

“Kadinali Silvestrini alikuwa mbunifu wa roho ya Helsinki na mchango uliotolewa naye na Vatican” ambaye aliona katika Mkutano wa Usalama na Ushirikiano barani Ulaya (Csce), uliomalizika  mnamo mwaka wa 1975 katika mji mkuu wa Finland, “hatua yenye uwezo ya kuziba mpasuko uliogawanya Ulaya mbili, lakini pia kwa msingi wa 'mizizi ya kawaida ya Kikristo', ya kufikia mkutano na umoja wa kweli wa bara hilo.” Hiyo ndiyo picha halisi ya Achille Silvestrini, aliyekuwa  Kadinali kutoka mazaliwa Mkowa wa Emilia Romagna ambaye aliyefariki mnamo mwaka 2019, kama ilivyooneshwa na Kardinali Pietro Parolin, Katibu wa Vaticani, wakati wa hafla  iliyokuwa na mada: “"Kadinali Achille Silvestrini, mtu wa mazungumzo,” iliyofanyika tarehe 27 Oktoba 2023 , katika kumbukumbu ya miaka mia moja ya  kuzaliwa kwake, iliyofanyika Ukumbi wa Campidoglio Roma.

Jukumu lake muhimu katika Kanisa na kwa Kanisa

Mbele ya Rais wa Jamhuri ya Italia Bwana Sergio Mattarella, katika hafla iliyohamaishwa  na Villa Nazareth  ya chuo kikuu cha sifa kwa wanafunzi wenye mahitaji ambayo Silvestrini alikuwa rais wake, Kardinali Parolin alikumbuka kwamba "Don Achille", aliyekuwa  mshiriki wa muda mrefu, kama katibu wa Baraza la Masuala ya Umma ya  Kanisa (tangu 1979 hadi 1988), wa  Katibu wa Vatican  Agostino Casaroli, alikuwa pamoja naye mhusika mkuu wa Ostpolitik ya Vatican na kwa hivyo katika mazungumzo na nchi za Ulaya ya Mashariki wakati huo katika Umoja wa Kisovieti au katika bonde lake la ushawishi. Kwa sababu hiyo Kardinali aliyezaliwa mnamo tarehe 25 Oktoba 1923 huko Brisighella, katika jimbo la Ravenna, Italia  alijua kujikita katika “jukumu muhimu katika Kanisa na kwa Kanisa, pamoja na mapapa saba, akipitia nyakati zenye maana hasa kwa maisha ya kikanisa na kwa misimu ya historia.”

Kard Silvestirni alifasiri diplomasia kama chombo cha ukweli wa wanadamu

Akirejea wasifu wake, Kadinali  Parolin alifafanua kuwa  Silvestrini  alikuwa mhusika mkuu madhubuti na anayeheshimika ambaye, kupitia juhudi zake, alifasiri diplomasia kama chombo cha kuchanganya matarajio ya nafsi na yale ya ukweli wa wanadamu.” Leo, kwa Kardinali Parolin, baada ya miaka 48, alisema “tunaweza kusema kwamba, “ikionekana katika mtazamo mahususi wa Ostpolitik, mchango wa Silvestrini ni wa kutopendezwa lakini ni wa kina; amefungwa kwa uthabiti na hiyo ni kwa ajili ya utu, haki zake na uhuru wake, ikitunuku kila kipengele chenye uwezo wa kujenga umoja kamili kati ya raia na muumini.” Kwa hiyo ‘Don Achille’ kama walivyozoea kumwita hakika alikuwa “mwanadiplomasia muhimu ambaye katika kumbukumbu za historia ya kikanisa anabaki kuwa mtumishi wa kweli wa Mrithi wa Petro na kikanisa kilichohuishwa na imani ya kweli na maisha ya ndani ya kina. Hivi ndivyo tunavyopenda kumkumbuka miaka 100 baada ya kuzaliwa kwake.”

Mwanadiplomasia katika huduma ya Mapapa wanne

Katibu wa Vatican  alikumbuka kwamba Silvestrini, ambaye aliweka uzoefu wake wa kidiplomasia usiopingika katika huduma ya Papa wanne, Pio XII, Mtakatifu Yohane XXIII na zaidi ya yote Mtakatifu Paulo VI na Mtakatifu Yohane Paulo II, alichukua jukumu muhimu katika mazungumzo ya Mkutano wa Usalama na ushirikiano barani Ulaya ambao ulihitimishwa kwa kutiwa saini Makubaliano ya Helsinki mwaka 1975, ambayo yalijumuisha, pamoja na mambo mengine, kutambuliwa kwa uhuru wa kidini kama haki ya msingi ya binadamu. Zaidi ya hayo, dhamira ya kidiplomasia ya Kardinali Silvestrini pia ilikuwa na ushawishi mkubwa katika marekebisho ya Mkataba kati ya Italia na Vatican mnamo  mwaka 1984.

Kard Parolin kuhusu Kardinali Accille Silvestrini
28 October 2023, 16:19