SPE:‘Fanya kazi nasi’,ukurasa wa kuomba nafasi ya kazi mjini Vatican
VATICAN NEWS
"Fanya kazi nasi" ni jina linalosema yote. Iwapo mpaka sasa walei walioajiriwa katika ngazi mbalimbali za Vatican walichaguliwa kwa misingi ya CV zilizotumwa na zilizopo, kuanzia sasa itawezekana kuomba moja kwa moja nafasi ambayo imekuwa au inayokaribia kuwa wazi. Huo ndiyo msingi mkuu wa tovuti mpya ya Sekretarieti ya Uchumi,SPE (del nuovo sito web della Segreteria per l’Economia),inayoongozwa na Mwenyekiti Maximino Caballero Ledo, ambayo iko mtandaoni tangu tarehe 24 Oktoba 2023 inaanza kufanya kazi katika mtandao. Maximino Ledo ameeleza kuwa: “Mada msingi katika mageuzi ya uchumi yanatazama watu ambao kama inavyotokea daima ni moja ya mageuzi magumu sana ya kufanya, hata kwa sababu ili kuongeza mageuzi na kutimiza utume wa Vatican kuna haja ya watu wenye uwezo wa kutosha, motisha na, juu ya yote, kwa maana ya maadili
Je ni jinsi gani ya kufanya kazi katika Kiti kitakatifu, Ni nafasi zipi zilizopo? Katika swali hili Luis Herrera, Mkurugenzi wa Rasilimali Watu, mjini Vatican amethibitisha, “kwamba sasa itawezekana kujibu kwa umma, shukrani ya uwepo wa sehemu ya mtandao “fanya kazi na sisi” inayojikita na suala hilo. Maelezo yote yanayohusiana na nafasi zilizo wazi yatatangazwa hapo na sifa za mwombaji. Yeyote atakayekuwa anapenda ataweza kuwakilisha ombi lake kupitia mtandaoni.” Kwa namna hiyo, SPE itakuwa na uwezekano wa kufikia wote, hasa kwa namna ya watu wanaotaka na ambao wanaweza kujua ni nafasi zipi zilizopo. Kwa hivyo, uteuzi wa wafanyakazi wanaovutiwa na jukumu hilo maalum utapendelewa.
Kwa kuendelea Herrare amesema: “Inatokea mara nyingi kwamba kwa upande wa mabaraza ya kipapa na majengo yake, wanafika wakuomba watu kwa namna maalum, kwa mfano wa lugha au ufundi ambao kirahisi huwezi kupata. Shukrani kwa mtandao mpya utasaidia mawasiliano, kati ya maombi na nafasi.” Kwa hiyo itakuwa daima na uwezekanao wa kutuma kupitia mtandaoni (CV,) wasifu bila kuunganisha kwa eneo maalum, huku wakingojea nafasi inayofaa ipatikane. Fanya kazi nasi” ni kitengo kinachokita na watu walei wanaopenda ambao wanaweza kuajiriwa Vatican na wanaelekeza waombaji wa nje ya Vatican. Lakini Sekretarieti ya Uchumi Vatican iko inafanya kazi ili kweza kujikita na ndani na hivyo ikiwa inatokea nafasi wazi, taarifa itatolewa hata kwa njia ya Mtandao wa Wafanyakazi, kwa kuhakikisha kuwa hata watu ambao walikuwa tayari ni sehemu ya kiungo cha Vatican bado wangetaka nafasi hiyo.
Mtandao mpya wa Sekretarieti ya Uchumi mjini Vatican, SPE zaidi pamoja na taarifa juu ya kazi na michakato ya kufanya maamuzi ya idara za kipapa, pia inatoa kwa njia ya uwazi sheria zinazodhibiti, udhibiti na usimamizi katika masuala ya kiuchumi na kifedha; na zile za udhibiti na usimamizi katika masuala ya utawala. Kwa mfano, Ofisi ya Kudhibiti wa Ununuzi ambayo inatafsiri na kutumia “Kanuni za uwazi, udhibiti na ushindani katika taratibu za kutoa kandarasi za umma za Kiti kitakatifu na Mji wa Vatican,” iliyopitishwa mnamo Mei 2020. Kwa maelezo zaidi unaweza kubonyeza kkatika Tovuti mpya wa SPE: https://www.spe.va