Tafuta

2023.09.28 Papa amepokea barua na hati kutoka kwa Bwana Hendy Anak Assan, Balozi wa Malaysia akiwakilisha nchi yake Vatican. 2023.09.28 Papa amepokea barua na hati kutoka kwa Bwana Hendy Anak Assan, Balozi wa Malaysia akiwakilisha nchi yake Vatican.  (Vatican Media)

Uwakilishi wa Barua na hati kutoka kwa Balozi wa Malaysia

Papa Francisko Barua na Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi wa Malaysia Bwana Hendy Anak Assan.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Alhamisi tarehe 28 Septemba 2023, Baba Mtakatifu amepokea Barua na hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi wa Malaysia Bwana Hendy Anak Assan, kuwakilisha nchi yake katika Mji wa Vatican. Bwana Hendy Anak Assan ameoa na ana watoto wawili.

Alizaliwa Kuching (Sarawak), mnamo tarehe 22 Mei 1970 na katika masomo yake alihitimu katika historia kutoka Chuo Kikuu cha Malaya (1994) na kupata Diploma ya Utawala wa Umma kutoka “Taasisi ya Taifa ya Utawala wa Umma” (INTAN) (1997).

Balozi wa Malaysia amewakilisha barua na hati za utambuzi mjini Vatican
Balozi wa Malaysia amewakilisha barua na hati za utambuzi mjini Vatican

Alishika nyadhifa zifuatazo: Mkurugenzi Msaidizi wa ASEAN, MAE (1995-1996); Katibu Msaidizi Kitengo cha Amerika, MAE (1997-1999); Katibu Msaidizi wa Ubalozi wao nchini Senegal (1999–2002); Mshauri, Ubalozi wao nchini Italia (2002–2006); Naibu Katibu wa  Ubalozi wa nchi yake huko Cambodia, Laos, Myanmar, Vietnam na Australia (CLMVO), MAE (2006–2010); Balozi huko Shanghai/Jamhuri ya Watu wa China (2010–2014); Naibu wa Balozi, nchini Japani(2014-2017); Katibu Msaidizi, wa Kitengo cha Ushirikiano wa Kimataifa na Maendeleo (ICADD), MAE (2017–2018; Katibu wa Kitengo cha Asia Mashariki, MAE (2018); Balozi wa Uzbekistan, Kyrgyzstan na Tajikistan (2018-2023).

28 September 2023, 12:08