Sinodi na mawasiliano:Siku ya mafunzo katika Chuo Kikuu LUMSA
Vatican News.
Zimesalia takribani siku chache kabisa kabla ya kikao cha kwanza cha Mkutano Mkuu wa XVI wa Kawaida wa Sinodi ya Maaskofu, “Kwa ajili ya Kanisa la Sinodi: Ushirika, Ushiriki na Utume”, kitakachofanyika kuanzia tarehe 4 hadi 29 Oktoba 2023, wakati huo huo kikao cha mwisho kitafanyika mwezi Oktoba 2024. Ili kuwezesha vyombo vya habari vilivyoitwa kuripoti tukio hilo, Chama cha Greenaccord, kwa kushirikiana na Sekretarieti Kuu ya Sinodi ya Maaskofu na Baraza la Kipapa la Mawasiliano walikusudia kuandaa siku ya mafunzo kwa waandishi wa habari yenye kichwa: “Sinodi inahoji mawasiliano. Mawasiliano yanahoji Sinodi.”
Hafla hiyo, iliyogawanywa katika vikao viwili, kuanzia saa 3.30 asubuhi hadi 12.00 jioni katika Ukumbi wa Jubilei wa Chuo Kikuu cha LUMSA, Roma tarehe 19 Septemba 2023. “Sinodi inaashiria mtindo maalum unaostahili maisha na utume wa Kanisa, kama watu wa Mungu wanaotembea pamoja kutangaza Injili”, alifafanua hayo Alfonso Cauteruccio, rais wa Chama Kisicho cha Kiserikali cha Greenaccord. Kwa hiyo, alisema kuwa si swali rahisi la ndani la kuwa na usimamizi au seti ya mikutano ya maaskofu na makusanyiko, lakini badala yake ni namna maalum ya kuishi Kanisa wakati inatenda.
Vikao viwili
Paulo VI alianzisha Sinodi ya Maaskofu mnamo mwaka 1965. Akirudia kile alichokidumisha, Papa Francisko alisema kwamba “Sinodi hiyo ina jukumu la mashauriano, kutoa taarifa na mapendekezo kwa Papa wa Roma kuhusu masuala mbalimbali ya kikanisa, chini ya uongozi wa Roho Mtakatifu.” Na hiyo kiukweli kama malengo, awamu mbalimbali, mbinu, hitimisho, ambayo Papa Francisko pengine atafupisha katika Waraka wa Kitume, ni mada ambazo lazima ziwasilishwe kwa watu wa Mungu kwa njia bora zaidi amesema Cauteruccio. Lakini, kwa kuwa ni somo lililobobea sana, ili lisibaki kuwa haki ya wataalamu tu, ni lazima litafsiriwe kwa maneno ya uandishi wa habari.
“Hii ndiyo sababu ya siku yetu ya mafunzo, ambayo yaligawanywa katika sehemu mbili: kikao cha asubuhi kilijikita na mbinu, na kipindi cha alasiri kilijitolea kabisa katika nyanja za mawasiliano na msaada ambao Baraza la Vatican itatoa kabla, wakati na baada ya tukio kwa waandishi wa habari wanaopenda. Kazi ilifungwa kwa kikao kuhusu masuala ya Ikolojia, kwa kuzingatia kwa ujumla sifa ambazo matukio ya kikanisa yanapaswa kuwa nayo ili kusindikiza na maagizo ya Laudato si', na kuchunguza mpango wa kufanya Sinodi kuwa na matokeo sifuri kwa kulipa fidia ya hewa chafuzi ( CO2) inayozalishwa.
Wazungumzaji
Wangumzaji walikuwa ni Kardinali Mario Grech, Katibu Mkuu wa Sinodi; Padre Giacomo Costa na Riccardo Battocchio, Makatibu Maalum wa Sinodi 2023/2024; Padre Dario Vitali wa Chuo Kikuu cha Kipapa cha Gregoriana; Monsinyo Hyacinthe Destivelle, afisa wa Baraza la Kipapa la Kuhamasisha Umoja wa Wakristo; Sr Nadia Coppa, rais wa zamani wa UISG; Sr Nathalie Becquart, katibu msadizi wa Sinodi; Padre Luis Marín de San Martín, katibu mmsaidizi wa Sinodi; Kardinali Francesco Coccopalmerio, rais mstaafu wa Baraza la Kipapa la Maandiko ya Kutunga Sheria; Romilda Ferrauto, mshauri mkuu wa Idara ya Mawasiliano; Matteo Bruni, mkurugenzi wa Ofisi ya Vyombo vya Habari vya Vatican; Andrea Monda, mkurugenzi wa Gazeti la Osservatore Romano; Padre Walter Insero wa Chuo Kikuu cha Kipapa cha Gregoriana; Padre Lucio Adrian Ruiz, katibu wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano; Walter Ganapini, mratibu wa Kamati ya Kisayansi ya mradi wa uendelevu wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro; Simona Roveda na Simone Molteni, Mkurugenzi wa Mawasiliano na Mkurugenzi wa Sayansi wa LifeGate. Wasimamizi wa Tukio hilo walikuwa ni Paolo Ruffini, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano; Silvia Guidi, mwandishi wa habari kutoka Osservatore Romano; Vincenzo Corrado, mkurugenzi wa Ofisi ya Kitaifa ya Mawasiliano ya Jamii ya CEI; Christiana Ruggeri, mwandishi wa habari wa TG2.