Nitakutunza ni kitabu cha maneno Papa kuhusu kujitolea
Vatican News
Kitabu kilichochapishwa na Nyumba ya Vatican LEV na Solferino kinaitwa ‘Nitakutunza. Wito kwa manufaa ya wote’, ambapo kitakuwa katika maduka ya vitabu kuanzia tarehe 19 Septemba 2023. Ni aina ya ‘Katekesi’ kama alivyoeleza mtunzi Riccardo Bonacina. Kwa hakika, kinakusanya matamshi yote ya Papa Francisko katika miaka hii kumi ya Upapa wake juu ya mada kuu ya kuwakaribisha wahitaji. Ni mada ya sasa sana, ambayo kama inavyoonesha katika kichwa kidogo kinakumbusha mzizi wa chimbuko la ujenzi wa wema kwa wote, unaoakisi mtazamo wa kiinjili wa kila mwamini.
Nadharia yake ni kwamba Papa ambaye alitoka Argentina kwa wakati fulani alithibitisha kuwa amejua uzuri wa watu wa kujitolea sana nchini Italia na kwa hiyo mtunzi wa kitabu Bonacina anabainisha kuwa hilo ni chaguo la bure kwa wengine ambalo lina sifa ya utamaduni wa nchi ya Italia na ambayo inajidhihirisha hasa katika hali za dharura. “Kiukweli tumeiona katika janga la Uviko na vile vile katika matukio mengine kwa mfano ya hivi karibuni ya mafuriko ya Emilia Romagna hadi tetemeko la ardhi huko Morocco na kwingineko.”
Bila chaguo hili la bure, manufaa ya wote yatasambaratika, amesisitiza mtunzi wa kitabu Bonacina, huku akifafanua jinsi ambavyo kama kitabu kinavyozungumzia juu ya hotuba za Papa wakati wa Katekesi zake, kwa mikutano, vyama, mashirika, Barua za kitume hata mikutano mingine ya umma.