Nembo ya Kardinali Protase Rugambwa:Enendeni Ulimwenguni kote!
Na Angella Rwezaula, - Vatican.
Sasa tunao makardinali wapya wa Kanisa ambao wamesimikwa na Baba Mtakatifu Francisko na kuongeza idadi nyingine ya Baraza la Makardinali. Ilikuwa ni tarehe 9 Julai 2023 ambapo Baba Mtakatifu Francisko aliwateua Makardinali wapya 21 wanaowakilisha makanisa mahalia ulimwenguni kote. Miongoni mwa makardinali hao watatu ni kutoka bara la Afrika ambao ni Askofu mkuu mwandamizi Protase Rugambwa wa Jimbo kuu la Tabora, Tanzania, Askofu mkuu Stephen Ameyu Martin MULLA, Jimbo kuu la Juba, Sudan ya Kusini pamoja na Askofu mkuu Stephen Brislin wa Jimbo kuu la Cape Town, Afrika Kusini.
Makardinali wapya wamesimikwa kwa hiyo rasmi katika mkutano wa kawaida wa Baraza la Makardinali ulioadhimishwa Jumamosi tarehe 30 Septemba 2023 mjini Vatican Katika Uwanja wa Mtakatifu Petro saa 4.00, majira ya Ulaya. Katika Muktadha wa Kardinali Rugambwa, "Euntes in mundum universum", yaani Enendeni Ulimwenguni kote" ambacho ni kifungu cha Injili ya Marko 16, 15 ndiyo kauli mbiu ya utume wake unaorejea maneno ya Yesu kabla ya kupaa Mbinguni alipowatuma mitume wake wahubiri Injili kwa mataifa yote. Utume huo bado unaendelea kupitia makuhani wake.
Parokia ya Kardinali Rugambwa Roma linaitwa Mtakatifu Maria wa Montesanto
Wakati wa kuvalishwa Kofia na Pete, makardinali wapya kama kila utamaduni wamepewa Maparokia mjini Roma, kwa njia hiyo, Kardinali Protase Rugambwa amepewa Kanisa la Mtakatifu Maria wa Montesanto, yaani Maria wa Mlima Mtakatifu ambalo ni kanisa lilikoko mjini Roma, katika eneo liitwalo Campo Marzio, (Piazza del Popolo) yaani katika 'Uwanja wa Watu' karibu na njia ya Babuino. Pia Kanisa hilo linajulikana kama Kanisa la Wasanii. Kadhalika ni linaitwa Kanisa pacha na la Mtakatifu Maria wa Miujiza, ingawa lina utofauti mkubwa hasa katika mpangilio wa Kisanaa. Sio rahisi kupotea unapofika katika eneo hilo, maana ni makanisa mawili yanayofanana mbele ya Uwanja Mkubwa huo wa WATU.
Katika maadhimisho ya kuundwa kwa Makardinali wapya, isipokuwa Padre Drin Mkapuchini, Mzee wa Miaka 96 wa Aargentina ambaye katika mahojianoa alisema afya yake haimruhusu, waliuodhuria ni makardinali, maaskofu, mapadre, watawa kike na kiume na waamini walei ambamo ni pamoja na wengine waliowakilisha Nchi zao kama vile: Bwana Félix Bolanos Garcia, Waziri kutoka Ofisi ya Rais nchini Hispania, na familia yake; Bwana Gérald Darmanin, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Ufaransa na familia; Bwana Matteo Piantedosi, Waziri wa Mambo ya Ndani nchini Italia na familia yake; Bi Grazyna Ignaczak-Bandych, Waziri wa Ofisi ya Rais nchini Poland na familia yake.
Wengine pia ni Bi Ana Caterina Mendes, Waziri wa Masuala ya Bunge nchini Ureno na familia yake; Bi Verónica Alcocer Garcia, Makamu Rais wa Jamhuri ya Colombia na mwenza; Bi Maria Fernanda Silva, Balozi wa Vaticananayeakilisha Nchi yake mjini Vatican na familia; Bwana Majid El Katarneh, Katibu Mkuu wa Waziri wa Mambo ya ndani nchini Jordan na familia , Dk. Mouin Elias Yousef Khouri, kutika Ofsi ya Rais kwa ajili ya Masuala ya Makanisa huko Palestina na familia; Dk. Benjamin Bol Mel Kuol, mwakilishi maalum wa Rais nchini Sudan Kusini na mwenzake, Ndugu Emmanuel Rousseau, Mkuu wa Shirika la Kijeshi la Malta; Kaburi Takatifu; Leonardo Visconti di Modrone, Mtawala Muuu wa Kaburi Takatifu la Yerusalemu. Na wengine ni Ndugu Alois Löser, Mkuu wa Jumuiya ya Kiekumeni ya Taize, Dk Patrick E. Kelly, Mkuu wa Shirika la kijeshi la Clumbus, mweshimiwa Lorenzo Fontana, Rais wa Bunge ya Jamhuri la Italia, Pia Profesa Romano Prodi; Balozi wa Tanzani, nafamilia yake na maafisa.