Korea,sanamu iliyobarikiwa ya mfiadini Andrew Kim iko nje ya Kanisa Kuu
Vatican News.
Tarehe 16 Septemba 2023 mchana sanamu ya Mtakatifu Andrew Kim Taegon, Padre na Mfiadini wa kwanza wa Korea ambaye Kanisa linamkumbuka kila tarehe 16 Septemba iliwekwa kwenye ukuta nje ya Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro, baada ya kubarikiwa na Kardinali Mauro Gambetti, Mkuu wa Kanisa kuu la Mtakatifu Petro. Katika afla hiyo Ujumbe wa waamini zaidi ya 300 wa Kanisa la Korea walishiriki katika uzinduzi huo, wakiwemo maaskofu, mapadre, watawa kike na kiume na walei.
Asuhuhi hiyo Septemba 16 hata hivyo waliopokelewa na Baba Mtakatifu Papa Francisko asubuhi wakisindikizwa na Kadinali Lazzaro Heung-sik You, Askofu wa zamani wa Daejeon Korea ambaye sasa ni Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Wakleri.
Kwa njia hiyo kabla ya kuweka sanamu hiyo sehemu iliyoadaliwa, Kardinali Lazzaro aliadhimisha Misa takatifu kwa lugha ya Kikorea katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican. Wazo hilo lilihamasishwa na Baraza la Maaskofu la Korea katika hitimisho la sherehe za kumbukumbu ya miaka 200 ya kuzaliwa kwa Mtakafitu mfiadini Andrea Kim. Kazi ya sanaa, yenye urefu wa karibu mita 4 na iliundwa katika marumaru ya Carrara na mchongaji wa sanamu wa Kikorea Han Jin-Sub, ambaye alifanya kazi pamoja na msanii wa Kiitaliano Nicolas Stagetti huko Pietrasanta, Versilia.