2023.08.15  Kardinali Pietro Parolin akiwa nchini Sudan Kusini alikutana na Rais wa Nchi hiyo. 2023.08.15 Kardinali Pietro Parolin akiwa nchini Sudan Kusini alikutana na Rais wa Nchi hiyo. 

Ziara ya Kardinali Parolin inaendelea Sudan Kusini katika ishara ya amani!

Jumanne Agosti 15 Agosti,Kardinali Parolin,Katibu wa Vatican ameondoka asubuhi kuelekea jimbo la Malakal,mahali ambapo aliadhimisha misa Takatifu na kutembelea wakimbizi.Ni kambi iliyokua kwa miaka 10 ambayo hadi sasa ni watu 37,000.Alipowasili Agosti 14,alikutana na Viongozi wakuu wa Sudan Kusini.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Kardinali Piero Parolin, Katibu wa Vatican akiwa katika ziara yake ya kichungaji nchini Sudan Kusini kwa mara ya pili kuanzia Jumatatu tarehe 14-17 Agosti 2023 kama mwendelezo wa ziara ya hivi karibuni ya Baba Mtakatifu Francisko nchini humo, mara baada ya kufika alikutana na viongozi wa Sudan Kusini akiwemo Rais Salva Kiir na Naibu wake na kushiriki katika upandaji wa baadhi ya miti kama ishara ya amani.

Mkutano wa Kardinali Parolin na wakuu wa Serikali ya Sudan Kusini
Mkutano wa Kardinali Parolin na wakuu wa Serikali ya Sudan Kusini

Kwa mujibu wa ratiba ya ziara hiyo, Jumanne tarehe 15 Agosti 2023, Kardinali Parolin amesafiri kwenda huko Malakal ambapo aliadhimisha Ibada ya Misa Takatifu katika Kanisa Kuu la Malakal na wakati huo huo Malakal ikiwa ni mwenyeji wa kambi kubwa ya watu waliokimbia makazi yao  na ambao wako chini ya ulinzi wa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini (UNMISS). Eneo hilo lilianzishwa takriban muongo mmoja uliopita ili kuwahifadhi hadi wakimbizi wa ndani 12,000, lakini hadi  sasa ina wakazi  wapata 37,000. Kwa njia hiyo mgogoro wa wakimbizi wa Sudan Kusini bado ni mkubwa zaidi barani Afrika, na ambapo watu milioni 2.3 wanaishi kama wakimbizi katika nchi jirani na wengine milioni 2.2 wakiwa wakimbizi wa ndani. Nchi hiyo inaendelea kuteseka na urithi wa vita vya wenyewe kwa wenyewe, migogoro ya kikabila inayoendelea na hivi karibuni zaidi, athari mbaya zailizo sababishwa na mabadiliko ya tabianchi na kuacha mamilioni ya wakihitaji msaada kuwa kubwa sana

Kardinali Parolin yuko Sudan Kusini
Kardinali Parolin yuko Sudan Kusini

Kardinali Parolin , Katibu wa Vatican, Jumatatu tarehe 14 Agosti 2023 alipofika alipokelewa uwanja wa Ndege na viongozi kadhaa wa Kanisa, watawa, waamini na  viongozi wa kiraia; alikutana na Rais Salva Kiir Mayardit, wa Jamhuri ya Sudan Kusini na makamu wake Rieck Machar na viongozi wengine na pia na Askofu Mkuu Stephen Ameyu.

Upandaji wa miti kama ishara ya amani na mshikamano
Upandaji wa miti kama ishara ya amani na mshikamano

Vile vile akiwa huko, aliungana na Vijana wa Kiekumeni na watoto wa Sudan Kusini katika kupanda miti kama ishara ya amani. “Kushuhudia kujitolea kwao bila kuyumba yumba kwa amani na jitihada zao zisizochoka za kuiendeleza kulitia moyo. Tukio hilo lilikuwa ni ufuatiliaji wa Hija ya Amani ya Kiekumene, na kuona kila mtu akikusanyika kwa ajili ya jambo moja kulitia moyo. Miti waliyopanda itasimama kama ishara yenye nguvu ya matumaini na umoja kwa vizazi vijavyo”, kwa mujibu wa taarifa kutoka eno la tukio lilitoangazwa kwenye ukurasa Facebook wa Baraza la Makanisa Sudan Kusini.

"Kushinda ‘pigo la kisasi’ kwa imani, tumaini na upendo",  ndiyo maneno ambayo Kardinali  Parolin aliendelea kuomboleza wakati wa mahubiri yake katika Kanisa kuu kuhusiana na vita vingi vinavyowakumba watu katika sehemu mbalimbali za dunia, ikiwa ni pamoja na vita vya wenyewe kwa wenyewe vya Sudan Kusini. Aliwakumbuka kwa hiyo watu wengi ambao wamekimbia makazi yao kwa sababu ya migogoro, huku  akibainisha pigo kubwa la kulipiza kisasi ambalo alisema linaharibu jamii zao. Hata hivyo, aliongeza Kardinali Parolin, katika mahubiri yake kuwa tendo la Kupalizwa kwa Mama Maria kinawakumbusha Wakristo  wote kwamba uovu hauna neno la mwisho kamwe na kwamba nguvu za wale wanaofedhehesha wengine ni za muda mfupi tu, kwa kuwa kiburi, silaha, na pesa zao hazitawaokoa”

Kardinali Parolin akishiriki upandaki wa baadhi ya miti kama ishara ya amani
Kardinali Parolin akishiriki upandaki wa baadhi ya miti kama ishara ya amani

Kardinali Parolin katika mahubiri aliwahimiza watu wa Sudan Kusini kumtegemea Kristo na mama yake kukumbuka kwamba tumaini kwa Mungu halikatishi tamaa, hasa Wakristo wanapochanganya tumaini letu na imani na matendo madhubuti ya huduma ya unyenyekevu kwa niaba ya amani. “Imani, upendo, unyenyekevu/ hasa udogo,” alisema Kardinali, Parolin  “ndiyo njia ya Injili, njia ambayo Maria aliipitia na iliyompeleka hadi mahali penye ung’avu, kama Malkia, upande wa kuume wa Mwanawe Yes una  kuwa ishara ya faraja na matumaini kwa ulimwengu wote.”

Kardinali Parolin huko Sudan Kusini
15 August 2023, 10:59