WYD,Lisbon:Tamasha la I la Uinjilishaji Kidijitali na Wamisionari
Na Angella Rwezaula, - Vatican.
Katika maadhimisho ya Siku ya 37 ya Vijana Duniani huko Lisbon kuanzia tarehe 1 hadi 6 Agosti, yanaongozwa na kauli mbiu isemayo "Maria akaamka na akwenda kwa haraka” (Lk 1:39). Mama wa Bwana Yesu, Maria anaoneshwa na Baba Mtakatifu kama mfano bora kwa vijana wanaotembea, kwa haraka lakini katika kutoa huduma , kuwa na ukaribu kama Mama Maria alivyokimbia upesi kumsaidia binadamu yake mjamzito na mzee mara baada ya kupata Tangazo kutoka kwa Malaika kuwa atakuwa Mama wa Mungu. Kwa hiyo Mama Maria ni kioo cha vijana hawa. Uinjilishaji katika karne hii umepata sifa kuu na mabadiliko hadi kufikia mitandao ya kijamii na sasa uwepo wa wamisionari wa unjilishaji wakiwa na wafuasi wao kupitia mitandao. Ni kwa njia hiyo kama mipango iliyomo ndani ya maadhimisho ya Siku ya vijana, kulikuwa na tukio la kimataifa la kutaka kushukuru “kazi kubwa” ambayo watu wenye ushawishi wa kidijitali na wamisionari kutoka mabara matano hufanya kila siku, wakisambaza Injili kupitia mitandao yao ya kijamii.
Uteuzi huu ulikuwa ni siku ya Ijumaa tarehe 4 Agosti, 2023 kuanzia saa 3.00 hadi 4.30, usiku huko jijini Lisbon, katika Eneo la Cristonautas, kwenye kiwanja cha Martim Moniz, ambapo mkutano wa kwanza wa ulimwengu wa wainjilishaji wa kidijitali na wamisionari ulifanyika wenye kauli mbiu: “Tamasha la washawishi wa Kikatoliki.” Mpango ulioanzishwa na wamisionari wa kidijitali ili kuitikia wito wa Papa Francisko kwa Kanisa zima kwa ajili ya Sinodi la Kisinodi, kwa nia ya kulifikisha katika mazingira ya kidijitali pia. Kutokana na hilo, Padre Bernardo Suate, wa Radio Vatican kati ya wanaotuwakilisha katika Siku ya Vijana duniani huko Lisbon 2023, aifanya mahojiano na Dk. Paolo Ruffini, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano na katibu wake Monsinyo Adrean Luiz kuhusiana na tukio la wainjilishaji kwa njia ya mitandao na ambao bado wanaendelea kufuatilia moja kwa moja kwa njia ya mitandao tukio hili la Siku ya vijana duniani huko Lisbon lililoanza tarehe Mosi hadi 6 Agosti 2023.
Kwa upande wake Dk. Ruffini alisema: “Ninaamini kuwa, zaidi ya tukio la Kanisa, hili ni tukio la watu wa Mungu, vijana, wadogo, wanaoishi katika mitandao ya kijamii na ambao kwa namna fulani wanaliomba Kanisa liwasindikize, wawe pamoja na kujenga mtandao wa pamoja tofauti, ulio wazi, wa ushirika, na si wa mgawanyiko. Kwa njia hiyo Baraza la Kipapa la Mawasiliano lisingeweza kushindwa kuwepo, kwa maana hiyo si kitu chetu, ni kitu cha kila kitu ambacho hakuna mtu wa katikati isipokuwa Yesu na hakuna anayetengwa kwa sababu ni mtandao wenye mawazo ya wazi, wa Kanisa lililo wazi, ambalo daima linajifunza jinsi ya kuzungumza katika wakati anaoishi.
Akiendelea kuelezea kadhalika Dk. Ruffini alieleza kuwa anaamini “vijana wakubwa na wadogo, ikiwa watakuza fikra wazi ambayo ndiyo njia pekee ya kuweza kubadili ukweli, ni lazima kila mara wawaombe vijana waandamane nao ili kuelewa jinsi ya kuzungumza lugha ya siku za usoni na wakati huo huo lazima wawape vijana mizizi ya mawazo na kumbukumbu ambayo bila hiyo tungeishia kung'olewa.” “Ni kwa pamoja tu, kama Papa Francisko anavyotuambia kila mara, ndivyo vizazi mbalimbali vinaweza kupata njia ya umoja ulio mkubwa zaidi kwa maisha bora ya baadaye. Ni kuwatakia matashi mema ya heri ulimwengu wote na kwa Wakatoliki ambao wanajua jinsi ya kulima kwa uzuri, na kupanda vizuri.
Na kwa upande wa Katibu Mkuu wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano Monsinyo Adrean Ruiz alisema huo ni utimilifu wa Baraza letu lakini ambalo linawajumuisha wengi kwa sababu ni kama kuchukua roho ya kimisionari ya huduma ya mawasiliano kwa moyo ili kufikia miisho ya dunia na ujumbe. Kwani kujiweke katika utamaduni wetu, kuufahamu na kusaidia, kusindikiza wote, vijana hao ambao, kwa ujasiri na ubunifu, wanataka kuwa Kanisa linalotoka nje na kufikia pembezoni. Akijibu ni wakina nao ambao wanaoshawishi, Monsinyo Ruiz alijibu kwa ni “Wale walio na Yesu mioyoni mwao na hisia zao, kama mitume wanavyosema, hatuwezi kukaa kimya juu ya kile tulichoona na kusikia. Na kwa hiyo mwenye ushawishi ni mtu yeyote aliye na Yesu moyoni mwake na anataka kumshirikisha na wengine”. Kwa njia hiyo; “Ni sherehe ya vijana, ni sherehe ya wale wote ambao, wakiona mateso, wanataka kuleta huruma na huruma ya Yesu hadi miisho ya dunia! Lazima tuwe na ujasiri wa kwenda, tusiogope! Kuna mambo mengi ambayo hayafanyiki vizuri, lakini kuna upendo mwingi na imani kubwa ya kumleta Yesu”.
Kwa hiyo Nyimbo, ngoma, shuhuda vilisindikiza Tamasha la kwanza la washawishi wa kidijitali wa Kikatoliki kwenye jukwaa la Siku ya Vijana Ulimwenguni huko Lisbon ambalo lilikuwa onesho la talanta na Imani. Hisia bado ilikuwa kubwa baada ya mkutano katika Buastani kubwa ya Edoardo VII, ambapo mamia ya maelfu ya mahujaji walikuwa wametoka kusali Njia ya Msalaba na Papa Francisko. Kwa hiyo katika Bustani yenye mwingiliano ya Siku ya Vijana WYD , hawa vijana washawishi wa kidijitali wa Kikatoliki walikusanyika ili kujadili mustakabali wa mawasiliano ya Kikatoliki, wa hitaji la kuendana na nyakati na kutumia vyombo vya habari vya kidijitali katika kueneza furaha ya Injili. Pamoja nao kulikuwa na Kardinali Oscar Rodriguez Maradiaga, Askofu mkuu mstaafu wa Tegucigalpa.
Wimbo uliofungua mkutano huo uliibua furaha ambayo imekuwa ikijitokeza tangu kuanza kwa Siku ya Vijana Duniani 2023. Ni wimbo rasmi wa tamasha hilo, unaoitwa “Vamos por todo el Mundo”, ambao muziki wake na maandishi yake yalitungwa na watu mbalimbali, wasanii kutoka nchi mbalimbali: Aldana Canale (Argentina), Tomas Romero (Colombia), P. José Pablo (Chile), Pablo Martínez (Argentina) na Felipe Contreras (Marekani). Ufafanuzi wa lugha nyingi, kwa upande mwingine, haukuundwa tu na mmoja wa waandishi (Pablo Martínez kwa Kihispania) lakini pia na waimbaji wa Kikatoliki: Pitter Di Laura (Kireno), Gen Verde (Kiitaliano), Juan Delgado (Kiingereza) na DJ. Halver ( Kifaransa).
Monsinyo Lucio Adrian Ruiz, katibu wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano , aliwakaribisha wote waliohudhuria, akiwaalika kwenda mbele kwa ujasiri na ubunifu. “Muwe na umoja ninyi kwa ninyi, kama mitume waliokwenda wawili-wawili”, alihimiza, na baadaye akapendekeza kwa vijana kuwa karibu na maaskofu daima na kuwa na umoja, kwamba “kwa sababu tunaweza kuwa Kanisa moja, kwani Yesu ndivyo anataka” Kwa matumaini sawa, Papa alitoa zawadi kwa washawishi wa Kikatoliki: mti mdogo wa mzeituni aliobariki siku moja kabla.
Ushuhuda
Vijana watatu wenye ushawishi walishirikisha ushuhuda wao. Jonathan Romie, aliyeigiza Yesu katika filamu ya “The Chosen One,” alizungumza kuhusu imani yake na jinsi ilivyomsaidia kuigiza katika filamu hiyo. Pitter di Laura alieleza, hata hivyo, jinsi ya kuwa mvuto wa Mungu katika maisha, akiwakumbusha vijana kwamba mtu hapaswi kuwa hivyo kwa ajili yake mwenyewe tu, bali kwa kila mtu. Naye Padre Rob Galea alizungumzia kuhusu wito wa Uinjilishaji na mwitikio wake. Mwanamuziki, Padre pia aliwaburudisha vijana kwa wimbo wake mmoja, uliochochewa kwa uhuru na muziki wa “Amazing Grace”.
Baraka kwa vyombo vya habari vya kidijitali
Msemaji wa mwisho wa mkutano huo alikuwa ni Kadinali Oscar Rodriguez Maradiaga, ambaye aliongoza muda wa sala. “Ni furaha iliyoje hatimaye kuweza kuja pamoja katika vyombo vya habari vya kidijitali ili kudumu katika utume wetu," alisema. Hatimaye, Monsinyo Ruiz alimwomba Kadinali kubariki vyombo vya habari vya kidijitali na waeneza Injili wake, kisha akawataka waliokuwepo kuwasha taa za simu zao za mkononi ili kuwakilisha mwanga wa vyombo vya habari vya kidijitali. Kwa hivyo, wakiangaziwa na taa nyingi zilizomulikwa gizani, kwa ukimya, washawishi walipokea baraka. Hatimaye muziki, nyimbo na ngoma. Kwa hiyo Muziki wa Missionarios Shalom ulifunga tamasha hilo, na baada ya hapo vijana wa ushawishi waliondoka kwenye bustani, wakiimba na kucheza, kama walivyofanya kila jioni kwa siku hizi na kama watakavyoendelea kufanya hadi Jumamosi usiku wa mkesha wa Misa Takatifu ya Dominika tarehe 6 Agosti 2023.