Papa kwa Mtakatifu Maria Mkuu kukabidhi ziara yake nchini Mongolia
Vatican News
Baba Mtakatifu Francisko, anakwenda nchini Mongolia katika ziara yake ya 43 ya kitume kuanzia tarehe 31 Agosti hadi tarehe 4 Septemba 2023. Kabla ya kuondoka kama kawaida yake, mchana alikwenda katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Maria Mkuu, mbele ya Picha ya Bikira Maria Salus Populi Romani,yaani Afya ya Waroma, ili kumkabidhi ziara yake hiyo.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka vyombo vya habari Vatican inabainisha kuwa: "Jumatano tarehe 30 Agosti, Papa Francisko amendoka kutoka nyumba ya Mtakatifu Marta na kufika Kanisa Kuu la Mtakatifu Maria Mkuu, mahali ambapo amekaa mbele ya Picha Bikira Salus Populi Romani kwa sala, akimkabidhi ziara yake ijayo ya kitume nchini Mongolia. Na hatimaye amerudi mjini Vatican."
Hii ni kwa mara ya 111 Papa Francisko kuingia katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Maria Mkuu. Katika Nchi ya Asia Baba Mtakatifu atakaa huko kwa siku nne kwa kuzingatia utofauti wa masaa 6 mbele kati ya Italia na Mongolia. Baba Mtakatifu anatarajia kurudi mjini Vatican mnanmo Jumatati tarehe 4 Septemba 2023.