PMS:kwa mara ya kwanza,shirika la matendo ya kimisionari linashiriki WYD na mtandaoni!
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Kwa mara ya kwanza Mashirika ya Kimisionari ya Kipapa (PMS) yatakuwepo katika Siku ya XXXVII ya Vijana Duniani ya kwenye Mji wa Furaha, ndani ya Maonesho ya Miito", mahali ambapo vijana watakutana na harakati, vyama mbalimbali, jumuiya, jumuiya za kitawa na mipango ya kikanisa. Uwepo wa PMS katika sehemu maalum iliyopambwa na uhuishaji umewekwa bango (V-528, ambapo itaanza kufanya kazi tangu Jumanne tarehe 1 Agosti hadi Ijumaa 4 Agosti 2023 kwa nyakati zilizoanzishwa na shirika) na kuna tume za matokeo ya harambee ya kurugenzi za kitaifa za Ulaya (pamoja na Ureno), kurugenzi ya Wapolandi , Waaustria, Wahispania na Waingereza) kwa kuungwa mkono na uongozi wa Marekani, unataka kuwa njia madhubuti ya kumulika mwelekeo wa kimisionari wa Kanisa la kiulimwengu."
Kwa mujibu wa maelezo ya Padre José António Mendes Rebelo, M.C.C.J, mkurugenzi wa PMS ya Ureno, ambaye aliratibu uwepo wa Siku ya Vijana Duniani WYD2023 kwenye tovuti alisema: “Tunataka kuwa ishara ya umoja wa Kanisa na Tutakuwepo kushuhudia utume wetu: kuwa ishara ya udugu na ushirika kati ya Makanisa yote mahalia ulimwenguni." Shirika habari za Kimisionari Fides, linaeleza kwamba, “Hii ni fursa muhimu sana ya kuwajulisha vijana historia, dhamira na mipango ya PMS inayofanya kazi kama mtandao mkuu duniani kote, ili kuwafanya wawasiliane na wale wanaofanya kazi katika nyanja ya kazi ya umisionari na kushughulikia kila mmoja wao binafsi, mwaliko wa kujisikia kuhusika katika mwelekeo huu wa umisionari ambao unatia changamoto kila mtu aliyebatizwa.”
Kwa maana hiyo, ukurasa wa Tovuti uliowekwa maalum kwa WYD2023 sasa uko mtandaoni kwenye tovuti ya PMS ambayo wavulana na wasichana wataweza kufikia kupitia QRCODE iliyowekwa kwenye safu ambayo itafanya kazi kama mandhari nyuma ya bango. Rozari za kimisionari pia zitatolewa katika kituo hicho, ambapo elfu tano kati yao wanaowasili kutoka Poland wanatoka kwenye Hija ya Kitaifa ya XI ya Jumuiya za Rozari kutoka nchini Poland kote, hadi mahali patakatifu Jasna Gora, ambapo idadi ya mfano ya rozari zilizokusudiwa kwa WYD zilibebwa kutoka madhabahuni katika maandamano ya zawadi.
Ukurasa wa Tovuti umegawanywa katika sehemu tatu: sehemu "PMS ulimwenguni" na ili kujua ni nchi gani ambazo PMS zipo; sehemu ya "Tubaki tunawasiliane", ina ukurasa wa kuanzisha uhusiano na PMS, na sehemu ya "Salini pamoja", ambapo inaeleza yaliyo muhimu kwa sala na hutolewa kama vile muhtasari wa kusali Rozari ya Wamisionari, maarifa juu ya Wenyeheri kama vile Paulina Jaricot (mwanzilishi wa Shirika la Kipapa la Uenezaji wa Imani, mwanamke wa imani na matendo, ambapo historia ya Mashirika ya Kimissionari ya Kipapa ilianzia) na pia toleo la podcast la Rozari Takatifu ya WYD2023 iliyoundwa na “Bofya ili Kusali” na hatimaye kuna jukwaa la Sala ya Papa kwa ajili ya Mtandao wa Kimataifa.”
“Rozari ni zawadi nzuri sana, hasa kwa sababu inatukumbusha kusali. Sala ni tendo la kwanza la utume kama vile Papa Francisko ametukumbusha mara kwa mara,” amesema hayo Padre Josè Rebelo. "Pili Rozari inatukumbusha Bikira Maria, ambaye hutembea na kusali pamoja nasi" aliongeza kusema mkurugenzi wa kitaifa wa PMS Ureno. Hatimaye, tarehe 3 Agosti saa 5:30 PMS itakuwa na nafasi maalum katika eneo la ushuhuda lililo ndani ya "Maonesho ya Miito" ambapo baadhi ya wavulana na wasichana kutoka maeneo mbalimbali ya kijiografia watashiriki uzoefu wao wa kimisionari.
Ukurasa wa Tovuti ya PMS ni: https://www.ppoomm.va/it/wyd2023.html
Unataka kufuatilia,pakua app ya WYD inapatikana kwa lugha tano:
"Lisboa 2023" ndiyo programu rasmi ya simu ya WYD Lisbon 2023 iliyotolewa na MEO, kama mshirika wa teknolojia na mwanzilishi wa WYD Lisbon 2023, na kutayarishwa na Bliss Applications. Inapatikana kwenye Android na IOS na inamulika yaliyomo katika lugha tano rasmi za WYD Lisbon 2023 (Kireno, Kiingereza, Kifaransa, Kihispania na Kiitaliano).