Papa awatembelea watoto na vijana wa kituo cha majira ya kiangazi mjini Vatican
Vatican News
Akizungumza na waandishi wa habari, Msemaji wa vyombo vya habari Vatican, Jumanne tarehe 18 Julai 2023, Dk. Matteo Bruni alisema kuwa “Leo asubuhi saa 3:00 kamili, Baba Mtakatifu Francisko alitembelea kituo cha majira ya joto cha watoto mjini Vatican (“Summer for children in Vatican”), akifuatana na Padre Franco Fontana, S.D.B., mwenye jukumu la kuandaa Juma za shughuli za kimwili, kielimu na kiroho katika kituo hicho.”
Dk. Bruni alingeza kusema kwamba “Baada ya salamu fupi kwa wahuishaji, ambao Papa alipendekeza kwao kuwa na hali ya kutotulia inayohamia kuwatumikia wengine, na kwa wafadhili, Papa alijikita katika mazungumzo na watoto na vijana wanaoshiriki katika kituo hicho cha majira ya joto”. Na “katika kujibu maswali yao, yanayohusiana na njia ya tafakari na shughuli wanazofuatilia katika siku hizi, Papa Francisko alisisitizia haja ya hisia kuwa na shukrani kwa wazazi wa wao binafsi hasa thamani ya babu na bibi kwa sababu ni mashujaa ambao waliunda familia na pia wao wanapaswa na hekima na hitaji la uhusiano mzuri na ulimwengu wa kidijitali.”