Papa akutana na Rais wa Ghana
Vatican News
Tarehe 22 Julai 2023, katika ofisi ndogo ya kwenye ukumbi wa Paulo VI, Baba Mtakatifu Francisko alikutana na Rais wa Jamhuri ya Nchi ya Ghana, Mheshimiwa Nana Addo Akufo-Addo, ambaye baadaye alikutana na Kardinali Pietro Parolin, Katibu wa Vaticvan akifuatana na Askofu Mkuu Paul Richard Gallagher, Katibu wa Mahusiano na Mataifa na Mashirika ya kimataifa.
Kwa mujibu wa Taarifa za vyombo vya Habari Vatican, inabainisha kuwa katika mazungumzo yao ya amani yaliyofanyika katika Sekretarieti ya Vatican, walionesha uhusiano mzuri kati ya Vatican na Ghan, na baadhi ya mambo ya hali ya kisiasa na kijamii na kiuchumi ya nchi yalijadiliwa, hasa kuhusu ushirikiano katika nyanja za elimu na afya. Vile vile kulikuwa na mabadilishano ya maoni juu ya mambo ya sasa ya kimataifa kwa kuzingatia masuala ya amani ya ulimwengu na usalama katika nchi za Afrika Magharibi.