Tafuta

Kanisa Kuu la Mtakatifu Yosefu Jimbo la  Morondava, huko Madagascar. Kanisa Kuu la Mtakatifu Yosefu Jimbo la Morondava, huko Madagascar. 

Askofu Gustavo Bombín ni Askofu Mkuu wa Jimbo kuu la Toliara,Madagascar

Askofu Mkuu Espino alizaliwa tarehe 24 Septemba 1960 na kupewa daraja la Upadre katika shirika la Utakatu Mtakatifu sana mnamo tarehe 21 Machi 1987.

Vatican News

Jumamosi tarehe 22 Julai 2023, Baba Mtakatifu Francisko alipokea na kuridhia barua ya kuomba kung’atuka katika  shughuli za kichungaji la Jimbo Kuu Katoliki la Toliara (Madagascar) iliyowakilishwa na Askofu Mkuu Fulgence Rabeony, S.I. Kwa wakati huo huo Baba Mtakatifu Francisko akamteua kuwa Askofu Mkuu wa Jimbo hilo hilo, Askofu Gustavo Bombín Espino, O.SS.T., kwa kumhamisha kutoka Jimbo la Maintirano.

Askofu Mkuu Espino alizaliwa tarehe 24 Septemba 1960 na kupewa daraja la Upadre katika shirika la Utakatu Mtakatifu  mnamo tarehe 21 Machi 1987. Kunako tarehe 4 Oktoba 2003 akiwa na umri wa miaka 43 aliteuliwa kuwa Askofu wa Tsiroanomandidy, Madagascar na mnamo tarehe 8 Februari 2017 ateuliwa na Papa Francisko kuwa Askofu wa Maintirano. Mnamo tarehe 13 Novemba 2018 aliteuliwa kuwa Msimamizi wa kitume wa Jimbo pia la  Mahajanga hadi 12 Februari 2023.

 

22 July 2023, 14:17