Tafuta

Siku ya kutafakari ndoto za watu wa Amazonia jijini Roma Siku ya kutafakari ndoto za watu wa Amazonia jijini Roma  (AFP or licensors)

Roma:Siku ya kujikita na Amazonia na ndoto za watu wake

Katika Jumba la Calisto,Roma walitoa onesho la filamu kuhusu upinzani na matumaini ya watu wa Amazoni na mazungumzo na makamu wa rais watatu wa Baraza la Kikanisa wa Amazonia,waliokutana na Papa mnamo Mosi Juni.Sista Smerilli:alisema Baraza la Kipapa la Huduma ya Maendeleo Fungamani ya Binadamu liko pamoja na wale wanaopata matatizo ya mazingira.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Mustakabali wa watu wa Amazonia kwa kuzingatia Sinodi na nafasi ya wanawake katika eneo kubwa la Amerika Kusini ndiyo kilikuwa kitovu cha Mkutano alasiri tarehe 6 Juni 2023  huko Roma, katika Jumbla la  Calisto, katika  mada ya mpango wa Walezi wa msitu, wa  mazungumzo na makamu wa rais watatu wa Baraza la  Kikanisa la Amazoni (Ceama), Patricia Gualinga, wa kiasilia  wa watu wa Sarayaku huko Mexico, Yesica Patiachi, Mperu wa kabila la Harakbut,na Sista Laura Vicuña, Mbrazili wa shirika la watawa makatekista wa Kifransiskani, mzaliwa wa Kiriri. Mkutano huo kwa kutanguliwa na onesho filamu yenye kichwa “Anamei”, ya  Alessandro Galassi, juu ya upinzani na matumaini ya watu wa Amazonia, pamoja na mambo mengine, Patiachi ndiye mhusika mkuu.  

Wakati wa kubadilishana zawadi na wawakilishi wa watu asiliano kutoka Amerika Kusini
Wakati wa kubadilishana zawadi na wawakilishi wa watu asiliano kutoka Amerika Kusini

Kwa njia hiyo tukio hili liliandaliwa na Tume ya Kipapa ya Amerika ya Kusini, kwa ushirikiano na Baraza la Kipapa la Huduma ya Maendeleo fungamani ya Binadamu. Kwa hafla hiyo, maonesho ya picha ya Amazzonia"pia yalianzishwa, yakisimamiwa na Cospe, shirika lisilo la kiserikali la ushirikiano wa kimataifa, na vijisehemu vya Giovanni Marrozzini na Giammarco Sicuro.

Wakati wa kuwasilisha hata filamu (ANAMEI) kuhusu watu wa Amazonia na utunzji wa msitu
Wakati wa kuwasilisha hata filamu (ANAMEI) kuhusu watu wa Amazonia na utunzji wa msitu

Makamu  rais wa watatu wa Ceama, ambao wamechagua kwa maisha yao kuwa walinzi wa Amazoni kwa ajili ya maisha ya watu wao na wanadamu wote, walipokelewa na Papa Francisko manamo  tarehe 1 Juni 2023. Kwa lengo la kutafuta “njia za ushirika na umoja ili kutafakari huduma mpya za wanawake katika Kanisa”, tarehe 4 Machi iliyopita, walikuwa wamemwandikia barua Baba Mtakatifu wakieleza nia ya kukutana naye na kuweza kufanya mazungumzo naye na jibu kutoka Vatican halikukawia. Kwa hiyo Viongozi hao watatu wa kiasilia waliviambia vyombo vya habari vya Vatican kwamba mkutano na Papa Francisko ulikuwa nimazungumzo ya kupendeza, matulivu na ya kuaminiana na kwamba walikuwa na usalama na uaminifu mkubwa kutoka kwa kwa Papa.

Papa alikutana na wawakilishi wa Baraza la Kikanisa la Amazonia
Papa alikutana na wawakilishi wa Baraza la Kikanisa la Amazonia

Katibu wa Baraza la Kipapa la Huduma ya maendeleo Fungamani ya Binadamu, alishiriki katika mkutano huo na kuelezea Vatican News, jinsi ilivyo muhimu kusikiliza shuhuda za wale wanaoteseka kwa ngozi zao wenyewe kutokana na matatizo yanayotokana na unyonyaji wa kupindukia ya asili, akiongeza kuwa kwa Amazoni na kwa maeneo yote yaliyo katika hatari lazima kuchukua hatua kwa kuzuia ili kuepuka uharibifu mkubwa kwa mazingira na hatari kwa maisha ya binadamu. “Ni vizuri kwamba dhamiri zetu zimetahadharishwa na sote tunafahamu kwamba kila mmoja wetu lazima afanye sehemu yake kwa mazingira. Katika mzungumzo yake kuhusu upinzani anaamini kwamba moja ya upinzani mkubwa ni kufikiri kwamba tatizo ni kubwa sana kwamba huwezi kufanya mengi. Na bado hii ndiyo hasa inazuia. Ikiwa tungeweza kufikiria, katika ishara zetu za kila siku, katika tabia zetu, katika matendo yetu, kwamba tunaweza kufanya mabadiliko madogo, ikiwa sote tungefanya mawazo haya, ulimwengu ungebadilika. Kwa hivyo, kwa maoni yangu, tunahitaji kufunua mifumo hii ambayo inatufanya tujihalalishe kwa kutofanya chochote. Ni lazima tuamini kwamba kila mmoja wetu anaweza kufanya jambo lolote.

Papa yuko mstari wa mbele kutetea wasu asilia. Tarehe 6 Juni alipokea wawakilishi wa watu asilia
Papa yuko mstari wa mbele kutetea wasu asilia. Tarehe 6 Juni alipokea wawakilishi wa watu asilia

Sr. Smerriri alifafanua kuwa Baraza la Kipapa la Maendeleo Fungamani ya Binadamu  inashughulikia maeneo mengi, lakini inajaribu kutekeleza kwa vitendo kile  ambacho Papa Francisko anaandika katika Laudato si', yaani kwamba kila kitu kimeunganishwa na kwamba mtu hawezi kufikiria masuala ya mazingira bila kufikiria uhamiaji, bila kufikiria afya. Kila kitu kimeunganishwa. Baraza hilo inachojaribu kufanya sasa ni kuanza kutoka kusikiliza, kutoka kusikiliza ukweli wa kile ambacho Maaskofu, watu wanaokuja kututembelea, wanawaletea kutoka katika maeneo yao, kujaribu kuelewa jinsi wanavyoweza kusaidia na jinsi gani wanaweza kuwasindikiza. Ni Matumaini yao  rahisi kuzungumzia matatizo ya kimataifa, lakini basi hatua zinahitajika kuchukuliwa katika maeneo tofauti. Kwa hiyo, huduma ya baraza hilo  labda kwa ukimya ni kuwa karibu na wale wanaosumbuliwa na hali fulani na kujaribu kuelewa jinsi tunaweza kusindikiza, jinsi gani wanaweza kuhamasisha  mafundisho ya Papa katika muktadha huo.

Wawakilishi wa Baraza la Kikanisa la Amazonia
08 June 2023, 17:11