Tafuta

Jengo la IOR mjini Vatican. Jengo la IOR mjini Vatican. 

Ripoti ya mwaka 2022 ya IOR:Faida ni Euro milioni 29.6

Imechapishwa Ripoti ya Taasisi ya Matendo ya Kazi za Dini ( IOR):imedumisha dhamira yake ya kufuata viwango vya juu zaidi vya kimataifa na vya maadili na udhibiti.Ukadiriaji wa Moneyval unaiweka kati ya taasisi zilizoorodheshwa bora zaidi ulimwenguni.Katika kipindi cha kutokuwa na uhakika sekta ya benki,OR imesimama kidete kwa nguvu yake ya mtaji na akiba imara.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Ripoti ya kila mwaka ya shughuli kuhusu Taasisi ya Matendo ya  Kazi za Dini ( IOR imechapishwa Jumanne tarehe 6 Juni 2023, ambayo, kwa utoaji wa kanuni za hivi karibuni  zilizotolewa na Papa Francisko, inawajibika kwa jukumu la meneja wa mali na amana wa mali zinazohamishika za Vatican  na Taasisi zinazohusishwa na Vatican. Taarifa kwa vyombo vya habari inaarifu kwamba faida halisi ni milioni 29.6 (ilikuwa milioni 18.1 mwaka uliopita), na kwamba kiwango cha riba kilikuwa +3.7%, kwamba kiasi cha kamisheni halisi kinafikia + 20.9% na kwamba ukadiriaji wa Moneyval unaweka Banki hiyo (IOR) kuwa   miongoni mwa taasisi zilizoorodheshwa na ubora zaidi duniani.

“Kwa mwaka wa kumi na moja mfululizo, Taasisi ya Matendo ya Kazi za kidini (IOR) kwa hiyo imechaposha Ripoti ya Mwaka iliyo na Taarifa za Fedha za 2022 zilizoundwa kwa mujibu wa viwango vya kimataifa vya uhasibu vya IAS-IFRS. Taarifa za Fedha zilipokea ripoti isiyo na sifa kutoka katika  kampuni ya ukaguzi ya Mazars Italia S.p.A. na, mnamo tarehe 25 Aprili 2023, iliidhinishwa kwa kauli moja na Baraza la Msimamizi wa IOR na, kulingana na Mkataba, kutumwa kwa Tume ya Makardinali kwa uchunguzi wake. Kwa kuzingatia uthabiti wa Bajeti ya 2022 na kwa kuzingatia mahitaji ya mtaji ya IOR, Tume ya Makardinali imeamua juu ya usambazaji wa faida.”

Ili kuhakikisha kuwa Taasisi inaweza kuendeleza malengo yake ya maendeleo kwa muda mrefu, Bodi ya Usimamizi imependekeza kwa Tume ya Makardinali kudumisha sera ya busara katika ugawaji wa gawio kama mwaka wa 2022. Kwa mjibu wa Ripiti inasomeka kuwa  mbinu ambayo imeimarishwa na migogoro ya hivi karibuni ya benki nchini Marekani na Ulaya na kwa haja ya kulinda Taasisi kwa muda mrefu, kutokana na mazingira ya pekee ambayo inafanya kazi. Kuhusiana na faida ya 2022, Bodi kwa hivyo imependekeza kwa Tume ya Makardinali usambazaji wa gawio la euro milioni 5.2.” Mapendekezo ya Bodi ni kugawa gawio kama ifuatavyo:- Euro milioni 3 kwa kazi za kidini za Papa Francisko; Euro milioni 2 kwa shughuli ya upendo wa Tume ya Makardinali;- Euro 200,000 kwa shughuli za usaidizi zinazoratibiwa na Mkuu wa Taasisi. Monsinyo Battista Ricca, amebainisha  kwamba kuna ufahamu kwamba Taasisi ni sehemu ya chombo kikubwa zaidi na muhimu zaidi na kwamba chombo hiki sio ulimwengu wa kifedha bali ni Vatican. Ufahamu wa hili umepunguza sana mawazo ya kujitegemea katika kutenda na karibu kuwa na uwezo wa kufanya kazi bila sheria yoyote. Zaidi ya hayo, hisia za maafa ya kweli yaliyofanyika siku za nyuma daima zipo ili kutufanya kuwa makini zaidi”.

Katika ripoti ya usimamizi, Rais wa IOR,  Jean-Baptiste de Franssu aliandika kwamba 2022 imeshuhudia usimamizi wa Taasisi ukijikita katika maeneo mbalimbali: uboreshaji endelevu katika usimamizi wa uwekezaji, upanuzi wa sera za maadili, kuanzishwa kwa jukwaa jipya la IT, kuajiri wataalamu wa ziada na kuanzishwa kwa sera ya 'tathmini ya wafanyakazi na mfumo wa motisha' ambayo inaleta mfumo wa malipo ulio wazi na uliopangwa kulingana na matokeo yaliyopatikana”. Katika sehemu ya ripoti inayohusu taarifa ya hali ya uendeshaji, Mkurugenzi Mkuu wa IOR, Gian Franco Mammì, aliwasilisha kuwa kufikia tarehe 31 Desemba 2022 mali ya mizania ya IOR ilifikia euro bilioni 2.8”. Mammì alielezea kwa vyombo vya habari vya Vatcan kwamba katika kipindi hiki cha kutokuwa na uhakika katika sekta ya benki, IOR inasimama imara kwa uthabiti wake wa juu wa mtaji na fedha taslimu thabiti" na vigezo juu ya mahitaji ya udhibiti, ambayo yanaifanya kuwa moja ya imara zaidi katika eneo la benki ya kimataifa”.

Naye Meneja Mkuu alisisitiza kwamba “kwa ujumla, utoaji wa huduma za benki na uwekezaji umepanuliwa ili kukidhi mahitaji ya wateja wanaozidi kufahamu na kuhitaji. Hili liliwezekana pia kutokana na matumizi ya majukwaa na programu zinazozidi kuwa za kiubunifu na Taasisi, ambayo inaendelea kuwekeza katika uwekaji digitali". Mwisho, Mammì ali kumbuka kwamba IOR ndiyo taasisi pekee ya fedha katika huduma ya Kanisa ulimwenguni ambayo inaegemeza shughuli zake katika kanuni ya kuafikiana na maadili ya Kikatoliki na si kwa kanuni ya faida ya juu iwezekanavyo. hata kufuata viwango vya kimataifa vya benki na mbinu bora”.

Ikumbukwe  Benki Kuu ya Vatican, IOR, au Taasisi ya Matendo ya Kidini  ilianzishwa kunako mwaka 1942 na Papa Pio XII, ambayo kwa hakika inajihusisha na huduma kwa mashirika ya kitawa, kazi za kitume na shughuli za uinjilishaji unaofanywa na Kanisa la Kiulimwengu wote.  Kadili ya siku zilivyokwenda Papa Pio XII alifanya mabadiliko kwenye Katiba yake mwaka 1944 na  mnamo 1990, Mtakatifu Yohane Paulo II alirekebisha Katiba hiyo ambayo kwa miaka ya karibuni na Baba Mtakatifu Francisko, tarehe 10 Agosti 2019 amefanya marekebisho makubwa kuhusu IOR, yaani  Taasisi ya Matendo ya Kidini ili kuwekwa uwazi zaidi na kuendana na mfumo mzima wa kimataifa. Katika marekebisho ya Katiba hiyo, Baba Mtakatifu alifafanua kuhusu lengo la Benki Kuu ya Vatican, IOR; Mkaguzi wa nje; Muundo wa Benki chini ya Tume ya Makardinali; Baraza la Washauri, Askofu, Uongozi, sheria, kanuni na taratibu za kutunza taarifa za mikutano ya Benki Kuu ya Vatican. Hayo yote ni katika kuendelea na misingi ya   ukweli, uwazi, uadilifu na maadili katika matumizi ya fedha na mali ya Kanisa zisizo hamishika na zinazo hamishika.

Shughuli za Benk ya Vatican ( IOR)
08 June 2023, 17:02