‘Not Alone? Ni mkutano wa kimataifa utakaofanyika Juni 10 jijini Roma
Na Angella Rwezaula, - Vatican.
Kufanya neno udugu lisikike ulimwenguni kote kwenye vyombo vya habari vya Vatican, Televisheni ya Italia (Rai 1) na katika utiririshaji, kutoka Uwanja wa Mtakatifu Petro na kutoka viwanja vingine nane duniani huko Brazzaville, Bangui, Ethiopia, Buenos Aires, Nagasaki, Lima, Yerusalemu na kwa meli ya uokoaji. Bahari ya Jonio, huko Trapani ili udugu uweze kupenyeza tamaduni na kuleta kwa usikivu wa mioyo na watu kwamba watu wote ni ndugu, kwa sababu wanashirikishwa na ubinadamu mmoja. Kwa mujibu wa Kadinali Mauro Gambetti alielezea hayo tarehe 5 Juni 2023 wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika Ofisi ya Vyombo vya Habari Vatican kwamba lengo la ‘No alone’, yaani ‘Si peke yake’, ambao ni Mkutano wa kimataifa wa Udugu wa Kibinadamu utakaofanyika tarehe 10 Juni 2023 na ambao pia utahudhuriwa na Papa Francisko. Kwa msukumo wa waraka wa Fratelli tutti, mpango huu umeandaliwa na Mfuko wa Vatican wenye jina hilo hilo kwa ushirikiano na Kanisa kuu la Mtakatifu Petro, Baraza la Kipapa la Huduma ya maendeleo Fungamani ya Binadamu , ili kukuza utamaduni wa udugu, mazungumzo na amani na itawaleta pamoja watu mbalimbali na vijana kutoka duniani kote ikiwa ni pamoja na vijana wa Kiukreni na Kirussi ambao, mwisho wa siku, wakishikana mikono, watajiunga na kukumbatiana kwenye nguzo ya Mtakatifu Petro kama , ishara ya usanii wa kulikumbatia Kanisa zima.
“Not alone “Si peke yake” ni siku iliyotungwa kama mchakato na uzoefu wa kujenga udugu ambao utagawanywa katika nyakati mbili: kuanzia asubuhi vikundi 5 vya kazi vitakutana jijini Vatican, ambao ni washindi wa Tuzo ya Nobel, mazingira, shule, watu walio katika mazingira magumu, na vyama ambayo vitashughulikia mada ya udugu na vitashiriki njia za ushirika. Alasiri, kuanzia saa 10.00 hadi usiku, Mkutano utakaoongozwa na mtangazaji wa Italia Carlo Conti utaanza, wakati wa sherehe na umoja chini ya bendera ya kushiriki, sanaa na muziki, ambayo inalenga kuwa fursa ya kugundua tena hisia za udugu na urafiki wa kijamii. Pia kutakuwa na nafasi kwa wawakilishi wa sekta ya tatu, vyama vya kutetea haki za binadamu, wanamazingira na wajasiriamali ambao watazungumza kuhusu uchaguzi wao na dhamira yao ya kujenga utamaduni wa udugu. Uzoefu pia utasikika kutoka katika viwanja vingine duniani vitakavyounganishwa.
Katika Mkutano huo, Filippo Grandi, Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Wakimbizi, Jumuiya ya Mtakatifu Egidio, Kituo cha Astalli na Rondine Cittadella della Pace watazungumza kuhusu utume wao. “Tuna furaha kujiunga na ombi la Papa la udugu wa binadamu na amani, alisisitiza Bwana Grandi akizungumza kwa mbali katika mkutano wa waandishi wa habari. Katika ulimwengu unaoteswa sana na migogoro, ujumbe huu lazima ukaribishwe kwa manufaa ya wanadamu wote. Bwana Grandi aliongeza kuwa leo hii kuna jumuiya nyingi ambazo zinawakaribisha wakimbizi kama kaka na dada na kwa pamoja zimejitolea kufanya jamii zetu kukua na anatumai kwamba Si peke yake bali hiyo inawakilisha mwanzo wa mshikamano ulioimarishwa kwa zaidi ya watu milioni 103 waliohamishwa na wakimbizi bado wanatafuta ulinzi”.
Davi Yambio, msemaji wa mtandao wa Wakimbizi nchini Libya, ambaye alitoroka kutoka kambi za mateso huko Tripoli na sasa ni mkimbizi wa kisiasa nchini Italia, pia atashiriki katika mkutano huo; Sandra Sarti rais wa Mfuko wa Kipapa wa Kanisa Hitaji Italia; kiongozi wa haki za watoto Kinsu Kumar; Heidi Kuhn mwanzilishi wa Root of peace, yaani Mizizi ya mani ambalo ni shirika linalojitolea kusafisha mashamba ya migodi ya kuzuia wafanyakazi ili kuyafanya kuwa ardhi yenye rutuba ya kilimo; Catia Bastioli mwanzilishi wa Novamont; Ermete Realacci, muundaji wa Mfuko wa Symbola. Meli ya uokoaji ya Bahari ya Jonio, ambayo katika hafla hiyo itabadilishwa katika uwanja kukaribisha, wanawake na wanaume 50 kutoka katika uzoefu mbalimbali wa mshikamano, ukarimu na kushirikiana, walei na watawa, wanaofanya kazi huko Sicilia.
Na tena kutakuwa na nafasi kwa mapadre, watawa wa kike na kiume na walei waliojitolea kujenga utamaduni wa mshikamano na urafiki wa kijamii duniani, huku kutoka Buenos Aires, miongoni mwa wengine, Sergio Sánchez katika katuni za kushiriki uzoefu wao, kutoka Lima Sr.María Helida, mpishi na mwanachama wa jumuiya ya kidini ya Hijas de María, na Maricela Macavilca, mfugaji wa Huarochirí. Kwa kuongezea, Padre Matthieu atakuwepo kutoka Bangui (Afrika ya Kati), na Patriaki wa Kilatini wa Jerusalem Askofu Mkuu Pierbattista Pizzaballa atazungumza kutoka Yerusalemu. Baba Mtakatifu Francisko atafikia Uwanja wa Mtakatifu Petro saa kumi na mbili jioni, atasalimia waliopo na viwanja vitakavyounganishwa ulimwenguni kote na kusikiliza kile kilichojitokeza katika vikundi vya kazi itakayokuwa imefanyika asubuhi. Wakiwakilisha washindi wa Tuzo ya Nobel, Muhammad Yunus na Nadia Murad - ambao walitunukiwa tuzo ya amani mwaka wa 2006 na 2018, watawasilisha hati kuhusu udugu kwa Papa na kwa pamoja watazindua mkusanyiko wa sahihi bilioni moja kwa ajili ya udugu duniani kote. Itakuwa mwanzo wa mchakato, huo alisema Kardinali Gambetti. Kwa kuongezea alisema “Ama sisi ni ndugu, tunatambuana kama ndugu, au tunakuwa maadui. Kila mtu lazima achague upande gani anataka kuwa.”
Wale wote watakaotia saini tamko hilo katika mchakato huo ambao utatokea baada ya tarehe 10 Juni watakuwa sehemu ya ulimwengu unaotaka kujenga udugu. Papa Francisko pia ataoneshwa kazi juu ya udugu na video iliyotengenezwa kwa wale walio dhaifu zaidi na wale wanaoishi kando ya jamii. "”isi sote ni wa hadhi sawa lakini sisi ni tofauti”alisisitiza Kardinali Gambeti kutoka kwa kila mtazamo: wa kiaanthropolojia, kiutamaduni, kijamii, kikabila na kidini. Lakini hii ni uzuri mkuu na pia zawadi kubwa na uwezo, kwa sababu karibu na tofauti hizi, kwa kuusoma katika mwanga wa udugu, ushirika, jumuiya inaweza kujengwa. Vijana wa kike na kiume kutoka mabara matano watamfikia Papa, wakifuatana na Kwaya ndogo ya Coro Antoniano, ili kuunda mzunguko wa kukumbatia kama ishara, ambayo itahusisha mzunguko nzima ya Bernini. Tukio la Not Alone litaoneshwa mbashara na Televisheni ya Italia Rai1 kuanzia saa 11 Jioni masaa ya Ulaya hadi 12.45, lakini hafla hiyo itaendelea hadi usiku na kuanza saa 2.45 hadi 22, katika Uwanja wa Mtakatifu Pietro kutakuwa na sarakasi na wasanii wa mitaani ambao watatumbuiza kati ya watu. Mwisho wa siku, kila mshiriki atapokea bonge la udongo-hai kama zawadi na mbegu za kupanda na kuota, kama ishara ya kujitolea kulinda udugu.
Tarehe 5 Juni Kadinali Zuppi ameanza utume huko Kyiv kuendeleza maono haya, ambayo ni, kwamba inawezekana kutambuana kama ndugu na kwamba wanatambuana kama zawadi na wanaweza kuishi pamoja kwa amani, alisema Kardinali Gambetti huku akisisitiza kwamba madhumuni ya siku ya tarehe 10 Juni 2023 itakuwa ni kuzindua upya neno la udugu na kutoa sauti kwa kile ambacho Papa Francisko aliandika katika waraka wa Fratelli tutti ili kutoa umakini wa upeo wa kukutana na kuelewa upya ulimwengu, utandawazi, na haraka inayopendelea ukuaji awali ya yote maelewano kati ya watu, katika nyanja ya uchumi, haki, siasa, kazi na mazingira”. Kwa njia hiyo alihitimisha kwa kusema wanataka kweli kuwa hapo ndugu.