'Not Alone' ni kukumbatia ulimwengu kwa amani na udugu
Na Angella Rwezaula, Vatican.
Udugu ni kukumbatiana. Kwa hiyo kwa vijana ambao, kila mmoja alivaa shati la bendera ya kila nchi yake ulimwenguni, kwa sauti ya "Sisi ni ulimwengu", walioungana katika uwanja wa Kanisa wa Mtakatifu Petro Vatican, ambao labda ndio ulikuwa wakati mzuri wa maana ya mkutano wa kwanza wa Kimataifa kuhusu Udugu wa binadamu, uliofanyika jioni ya Jumamosi tarehe 10 Jani 2023 katika Viwanja vya Mtakatifu Petro. Tukio lililoandaliwa na Mfuko wa wa Fratelli Tutti kwa ushirikiano na Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro, Baraza la Kipapa la Huduma ya maendeleo Fungamani ya Binadamu na Baraza la Kipapa la Mawasiliano na kuhamasishwa na waraka wa Papa Francisko wa mnamo 2020 (Fratelli tutti) na kujitolea kwake kwa amani kati ya watu wa dini zote na kwa sababu hakuna mtu aliye peke yake.
Kwa hiyo Kauli mbiu ya ‘Note alone’ yaani Si peke yake", ndiyo hakika iliongoza mkutano huo wa siku. Kwa hiyo katika mazungumzo na amani waliunganisha vijana wote ulimwenguni. Kulikuwa na vipindi viwili vya siku, asubuhi na mchana ambao asubuhi hiyo waliunganisha katika makundi matano ya kazi ya kukabiliana pamoja makundi ya: Washindi wa Tuzo la Nobel, mazingira, shule, mashirika dhaifu, na vyama ili kushughulikia mada ya udugu na walishiriki njia za ushirika. Alasiri, saa kumi jioni, ndipo ukaanza mkutano ukiongozwa na mtangazaji Carlo Conti, wakati wa afla hiyo ambayo iliwaona wasanii wa muziki na michezo wakiwemo hata kwaya ndogo ya watoto wa Antony.
Wito kutoka kwa Washindi wa Tuzo ya Nobel kwa ajili ya amani na haki
“Hakuna vita tena! Amani, haki na usawa ndio unaongoza hatima ya wanadamu wote. Hapana kuwa na hofu, unyanyasaji wa kijinsia na majumbani! Kumaliza migogoro ya silaha. Sema vya kutosha kwa silaha za nyuklia na mabomu ya ardhini. Hakuna tena uhamaji wa kulazimishwa, utakaso wa kikabila, udikteta, ufisadi na utumwa. Tuache matumizi mabaya ya teknolojia na akili bandia, tuweke maendeleo ya kiteknolojia mbele na kuyarutubisha na udugu". Hoja hizo zilipata mwangwi kwa ulimwengu na Nadia Murad, mwanaharakati wa haki za binadamu nchini Iraq na mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel 2018, na mwanauchumi wa Kibengali Muhammed Yunus, mkuzaji wa mikopo midogo midogo na Tuzo ya Amani ya Nobel mwaka wa 2006, kwa niaba ya washindi wengine zaidi ya thelathini jijini Roma katika tukio hilo kwenye taarifa iliyotolewa katika uwanja wa Mtakatifu Petro na na kutiwa saini na Kardinali Pietro Parolin Katibu wa Vatican.
Kila mwanaume ni kaka, kila mwanamke ni dada
Mwaliko ulioelekezwa kwa watu wote wenye mapenzi mema ni kutia saini wito huo ili kukumbatia ndoto hiyo na kuigeuza kuwa ya vitendo vya kila siku, ili ifikie akili na mioyo ya viongozi wote wa serikali na wale ambao, katika kila ngazi, wana jukumu kidogo kubwa la kiraia. Pamoja na Papa Francisko, ambaye mara kadhaa amepokea upendo na vifijo kwenye Uwanja wa Mtakatifu Petro na ambaye hotuba yake iliyopangwa kufanyika ilisomwa na Kardinali Mauro Gambetti, Mkuu wa Kanisa ka Kipapa katika mji wa Vatican, washindi wa Tuzo ya Nobel walikariri kwamba “kila mwanaume ni kaka yangu; kila mwanamke ni dada yangu, daima”.
Bustani ya Dunia ni udugu na hali ya maisha kwa wote
“Tunataka kuishi pamoja, kama kaka na dada katika Bustani ambayo ni Ardhi, kwa sababu Bustani ya udugu ni hali ya maisha kwa wote. Maelewano yaliyopotea, kiukweli, huchanua tena wakati utu unaheshimiwa, machozi yanakauka, kazi inalipwa kwa haki, elimu inahakikishwa, afya inatunzwa, utofauti huthaminiwa, asili hurejeshwa, haki inaheshimiwa na jamii inakumbatia upweke. na hofu”
Udugu huzaliwa na mtu na kufikia ulimwengu
Kwa maana hiyo, udugu ni juu ya yote binafsi. Ni ile ya moyo, inayorutubishwa na huruma, ushirikiano, utovu wa adabu, kiasi na uwajibikaji. Na kwa kupanda mbegu ndogo kwa siku katika mahusiano ya maisha ya kila siku ya mtu (nyumbani, shuleni, kazini, taasisi), udugu wa kiroho unakua, ambao lazima uelekeze kwenye udugu wa kijamii" ambao unatambua hadhi sawa kwa wote. Watuzwa Nobel wameandika kuwa "Pamoja, tunataka kujenga udugu wa mazingira, kufanya amani na asili kwa kutambua kwamba kila kitu kinahusiana: hatima ya ulimwengu, utunzaji wa uumbaji, maelewano ya asili na maisha endelevu. Lengo ni mpito ya haki ya kiikolojia, kilimo endelevu ambacho kinahakikisha upatikanaji wa chakula kwa wote, kukuza mahusiano yenye usawa, yenye msingi wa kuheshimiana na kujali ustawi kwa wote".
Kardinali Parolin: Kila mtu ahisi kuhusika na jukumu hilo
Naye Kardinali Pietro Parolin Katibu wa Vatican kuwa “Sote tunatumaini kuwa maneno haya yanayodai yatatafsiriwa katika mazoezi ya kila siku,”na jinsi ambavyo kila mtu lazima ajisikie kuhusika katika ahadi hii. Hatuwagawi wengine, na kila mmoja wetu lazima afanye sehemu yake", alisema. Kwa kuongezea: "Tuna matatizo mengi sana duniani, lakini pia tunalo jibu, njia kuu ambayo sote tunaweza kutembea ili kujaribu kutatua matatizo haya kwa nia njema na kujitolea na ni njia ya udugu ambayo Kanisa daima limeonesha kwa ulimwengu na ambayo Papa Francisko amechukua kwa njia sahihi na iliyodhamiriwa katika waraka wa Fratelli Tutti. Kila kitu kinachokwenda katika mwelekeo wa udugu wa kibinadamu kinaweza kweli kuwa njia ya kujenga ulimwengu mpya, tofauti wa amani na mshikamano na ishara hii tuliyofanya inakwenda kwa njia hii".