Matashi mema kwa Papa kutoka kwa Kard.Parolin Katibu wa Vatican
Na Angella Rwezaula, - Vatican.
Kardinali Pietro Parolin, Katibu wa Vatican alielekeza matashi mema kwa waandishi wa habari kwa ajili ya Baba Mtakatifu Francisko ambaye alasiri alikuwa afanyiwe upasuaji tarehe 7 Juni 2023 katika hospitali ya Gemelli, Roma kwamba "Tunamfuatilia kwa upendo wetu kwa maombi yetu tukitumaini kuwa kila kitu kitatatuliwa haraka iwezekanavyo." Hata hivyo mapema asubuhi habari hiyo ilitolewa na Ofisi ya Vyombo vya Habari vya Vatican, ambayo ilieleza kuwa: “ni Laparotomy na upasuaji wa plastiki wa ukuta wa tumbo na bandia chini ya anesthesia ya jumla, iliyoratibiwa na timu ya matibabu, ambayo itahitaji kukaa hospitali kwa siku kadhaa.” Alisema hayo katika fursa ya afla ya Uzinduzi wa kituo cha maelezo ya Jubilei 2025.
Kardinali Parolin kwa njia hiyo majira ya saa 6 kamili hivi alizindua Kituo cha maelezo cha Jubilei 2025 mahali ambapo patakuwa ni sehemu ya maelezo na mapokezi kwa ajili ya mahujaji wote watakaoshiriki Jubilei inayofuata kwenye njia ya Conciliazione, mita chache kutoka katika Uwanja wa Mtakatifu Petro. Katika fursa hiyo kwa sala na usomaji wa Injili, Kardinali Parolin akiwa pamoja na Askofu Mkuu Rino Fisichella, wa Baraza la Kipapa la Uinjilishaji alibariki jengo hilo ambalo tayari limeanza kufanya kazi kwa muda.
Akiwa pembeni, ya afla hiyo alisimama kidogo na wahandishi wa habari waliokuwepo kujibu maswali kuhusu upasuaji wa Papa, wa baada ya ule wa 2021 kwenye utumbo mpana. Alipoulizwa kama alikuwa na wasiwasi, Kadinali huyo alisema: “ Nisingejua la kusema, kwa sababu sina vipengele vyovyote vile. Hakuna cha kuongeza kwenye taarifa za vyombo vya habari kutoka Ofisi ya Vyombo vya Habari ya Vatican ambayo, alisema, mambo kwa njia ya kiufundi sana akijaribu kutoa vipengele vinavyoruhusu tatizo la kupangwa vizuri. Akijibu swali jingine tena la mwandishi kuihusu shughuli: “ Hakuna uhamisho wa madaraka. Akiwa katika muda wa upasuaji huo, alieleza: “Nadhani itakuwa saa chache, muda muhimu wa upasuaji basi shughuli zitaanza tena, hata ikiwa ni kutoka kitanda cha hospitalini. Ikiwa kuna mambo ambayo yanahitaji kuamuliwa na ya haraka, yatapelekwa kwake huko Gemelli”.
Katika mazungumzo mafupi ya Kardinali Parolin na waandishi wa habari, hakukosekana kurejea suala la utume wa Kardinali Matteo Maria Zuppi, rais wa Baraza la Maaskofu Italia (CEI) na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Bologna italia, huko Kyiv, nchini Ukraine, hatua ya kwanza ya utume aliyokabidhiwa na Baba Mtakatifu "ili kupunguza mvutano wa kuteswa Ukraine. Kwa hiyo “Utume wa Kardinali Zuppi ulikusudiwa kama ushirikiano, mchango zaidi ambao Vatican inaweza pia kutoa kwa ajili ya amani”, Kardinali Parolin alisisitiza.
Akiendelea na ufafanuzi huo alisema "Ninaamini kuwa hakuna jipya lililofanyika ikilinganishwa na yale ambayo Rais Zelensky alimweleza Papa wakati wa mkutano wao mnamo tarehe 13, wakati kiongozi huyo wa Ukraine alipoomba msaada kutoka kwa Papa na Vatican ili kuwarudisha nyumbani watoto wa Ukraine walipelekwa nchini Urussi na Papa alipendekeza “Mfumo wetu wa Amani kama kanuni pekee ya ufanisi ya kufikia amani ya haki. Msimamo wa Ukraine siku zote ni sawa”, Kardinali Parolin alifafanua, “lakini ukweli wa kuzungumza na kusikia misimamo na mitazamo tofauti kidogo bila shaka unaweza kuwa wa manufaa na kupendelea amani. Na jinsi gani kutakuwa na maendeleo, Sijui, itabidi tuone”, alisisitiza Kardinali.
Safari inayowezekana kwenda Moscow
Katika safari inayowezekana ya Kardinali Zuppi kwenda Moscow, Katibu wa Vatican alisema kwamba: “tutajadili naye (Kadinali Zuppi, ni hatua gani zaidi za kuchukua”. “Kwa upande wa Papa wazo lilizaliwa kama utume wa kutekelezwa katika miji mikuu miwili, ambapo matarajio ya Moscow yanapaswa kubaki wazi, lakini kwa hakika tutaona”, alisema. Kwa sasa, mkutano kati ya Parolin na Zuppi umepangwa mara tu atakaporudi, basi bila shaka wataripoti kwa Papa.