Ask.Mkuu Nappa anasema kuwa karama,uinjilishaji na sinodi ni msingi wa PMS
Na Angella Rwezaula, - Vatican.
Karama, uinjilishaji na sinodi hayo ndiyo maneno matatu ambayo Askofu mkuu Emilio Nappa, Katibu Msaidizi wa Baraza la Kipapa la Uinjilishaji na Rais wa Mashirika ya Kimissionari ya Kipapa (PMS), muhimu yanayoelezea vyema mchakato wa safari ya Mkutano Mkuu wa Mashirika ya Kipapa ya Kimisionari PMS tarehe 31 Mei 2023 ambao umeanza rasmi tangu tarehe 30 Mei hadi tarehe 6 Juni ambao unajishughulisha na shughuli za kawaida za kila mwaka. Kwa hiyo katika ufunguzi wa mkutano huo , Askofu Mkuu Nappa aliwashukuru wakurugenzi wa kitaifa zaidi ya 100 waliohudhuria, akihutubia kwa namna ya kipekee wakurugenzi walioteuliwa hivi karibuni na kuwashukuru kwa dhati Makatibu Wakuu wanne kwa msaada wao wa hali ya juu katika kazi zao za kila siku na hasa kwa tukio hilo muhimu.
Ushiriki wa Kazi ya Papa kwa ulimwngu wote
Kila mtu anashiriki katika kazi ya Baba Mtakatifu ya ulimwenguni pote ya kutoa uinjilishaji katika Makanisa yote na hasa kwa wale wanaohitaji ushuhuda na usaidizi zaidi, alisisitiza Rais ambaye alikumbuka utayari wake wa kusikiliza na kukaribisha mawazo . Hapo Roma, alisema hawafanyi lolote zaidi ya kuratibu na kufasiri utambulisho wao wa pamoja wa kuwa vyombo vya kukuza wajibu wa kimisionari wa kila mtu aliyebatizwa na kusaidia Makanisa mapya kama Papa mwenyewe Francisko alivyo sema katika Katiba ya Kitume ya hivi karibuni ya Praedicate Evangelium. Mchakato wa safari ya wake wa PMS ambayo ina sifa bainifu za karama iliyopokelewa kama zawadi kutoka kwa Mungu kupitia waanzilishi, muhimu hasa kwa kuzingatia marekebisho ya Sheria za PP.OO.MM ambayo itatekelezwa kwa misingi ya Katiba Praedicate Evangelium; Uinjilishaji unaoelezea utambulisho wa Kanisa, kama Papa alivyothibitisha tena katika Ujumbe wake kwa Siku ya Kimisoonari Duniani kwa mwaka 2022 na sinodi.
Kuendeza imani na kuhuisha msimu mpya wa utendaji wa kimisionari
Kwa kuzingatia hati za Majisterio ya hivi karibuni, alibainisha jinsi ambavyo anaona wazi ahadi tatu walizopewa alisisitiza Rais huko , akizingatia kipengele cha uinjilishaji cha mchakato wa safari ya PMS . Kwanza, kusaidia Makanisa maalum kuunda imani iliyokomaa na ya kimisionari ya watu wapya na waliokwishabatizwa, na pili, kusaidia Makanisa mahalia kwa ruzuku mbalimbali, hasa kwa ajili ya kueneza imani, na hatimaye; ili kuchochea na kuhuisha msimu mpya wa utendaji wa kimisionari wa jumuiya za Kikristo (akinukuu usemi wa Papa Francisko katika Ujumbe wa Siku ya Utume Duniani 2022), na hii pia katika maeneo ya mapokeo ya Kikristo ya kale, kwa upeo wa juu uwezo wa mtandao wa duniani uliopo wa kurugenzi za PMS za kitaifa na za majimbo.
Umuihimu wa kufanya kazi kama timu
Katika kuhimiza kila mtu kuwa na mtindo wa maisha ya umisionari wa Kikristo unaochochea kazi ya kawaida, Rais pia alikumbuka umuhimu wa kufanya kazi kama kucheza kama timu ili kuepuka kishawishi hatari ya kucheza peke yako. Pia alitoa baadhi ya mawazo madhubuti kwa Wakurugenzi kwa siku za mbeleni katika kushuhudia katika maeneo ya utume ambayo yanaunda jumuiya na shauku ya uongofu; kujifunza njia bora za kutoa ruzuku ambazo hutoa faida kubwa zaidi; kazi juu ya uwasilishaji wa miradi na ripoti za matokeo; kujaribu kuunda mtandao unaowezesha kushirikishana kwa uwazi na kutarajia mafunzo mazito yanayosaidia maeneo mbalimbali kuwa na watendaji wa Utume. Kwa hivyo basi tunajaribu kujiingiza kikamilifu katika njia kuelekea ushirikiano wa kimisionari wa karibu zaidi wa washiriki wake wote katika kila ngazi katika Kanisa, kama Papa Francisko alivyosisitiza katika Ujumbe wake wa hivi karibuni kwa Siku ya Kimisionari Duniani kwa mwaka 2023, alihitimisha, Askofu Mkuu Nappa.