Askofu Jean Claude Randrianarisoa wa Jimbo Katoliki la Miarinari Ang'atuka Madarakani
Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.
Baba Mtakatifu Francisko ameiridhia ombi lililowasilishwa kwake na Askofu Jean Claude Randrianarisoa wa Jimbo Katoliki, Miarinarivo, Madagascar la kutaka kung’atuka kutoka madarakani. Itakumbukwa kwamba, Askofu Mstaafu Jean Claude Randrianarisoa wa Jimbo Katoliki, Miarinarivo, Madagascar alizaliwa tarehe 4 Desemba 1961 huko Nandihizana Carion, nchini Madagascar. Baada ya malezi na majiundo yake ya Kikasisi tarehe 21 Septemba 1991 akapewa daraja Takatifu ya Upadre kwa ajili ya Jimbo kuu la Antananarivo lililoko nchini Madagascar.
Tarehe 15 Februari 2007, Baba Mtakatifu Benedikto wa kumi na sita akamteuwa kuwa Askofu wa Jimbo Katoliki la Miarinarivo, nchini Madagascar. Kumbe, kama Padre amelitumikia Kanisa kwa muda wa miaka 31.72 na kama Askofu akiwa na dhamana ya kufundisha, kuongoza na kuwatakatifuza wa Mungu kwa muda wa miaka 16.6.