Askofu Mkuu Gallagher yuko Mongolia kwa mahusiano ya nchi hizi!
Na Angella Rwezaula, - Vatican.
Mara baada ya Ofisi ya Habari ya Vatican kutangaza safari ya kitume itakayompeleka Baba Mtakatifu Francisko nchini Mongolia kati ya tarehe 31 Agosti na Septemba 4, 2023, ziara ya Askofu Mkuu Paul Richard Gallagher katika nchi ya Asia imeanza tarehe 4 Juni kwenye utume wake kwa ajili ya ajenda ya muda, ambayo ni sehemu ya mfumo wa mahusiano baina ya nchi hii na Vatican na ambayo itakamilika Jumanne tarehe 6 Junu 2023.
Misa na kukutana na wamisionari
Katika Tweet iliyozinduliwa Dominika tarehe 4 Juni 2023 na akaunti ya Terza Loggia ya Sekretarieti ya Vatican kwa utaratibu umeonesha mpango wa siku tatu wa utume wa Katibu wa Vatican wa Mahusiano na Mataifa na Mashirika ya Kimataifa, kuanza na pia maadhimisho ya Ekaristi takatifu ya tarehe 4 Juni 2023 katika Kanisa kuu la Watakatifu Petro na Paulo ambalo lipo huko Ulaanbaatar, ambao ni mji mkuu wa nchi, ikifuatiwa na mkutano na jumuiya ya wamisionari mahalia.
Mikutano na viongozi wa Mongolia
Tarehe 5 Juni kuna mfululizo wa mikutano na mamlaka ya Mongolia kuanzia na Waziri wa Mambo ya Nje, Bi Batmunkh Battsetseg, baadaye na Waziri Mkuu Luvsannamsrain Oyun-Erden. Siku ya Jumanne tarehe 6 Juni 2023 kabla ya kuondoka ni mazungumzo yaliyopangwa na ambayo oua yatapelekea mwakilishi wa Vatican kwenye mazungumzo na Rais wa Mongolia Ukhnaagiin Khürelsükh, pamoja na ratiba ya kusimama katika Makumbusho ya Kitaifa ya Chinggis Khan, muundo wa jengo la kisasa uliozinduliwa mnamo mwaka 2022 ambao unaonesha sanaa zaidi ya 12,000 za kihistoria zinazojikita katika muhtasari mpana wa ufalme wa Genghis Khan na warithi wake!