Tafuta

Siku ya Vijana duniani itafanyika huko Lisbon Agosti 2023. Siku ya Vijana duniani itafanyika huko Lisbon Agosti 2023. 

Papa atakwenda Lisbon katika Siku ya vijana duniani Agosti 2-6

Msemaji wa vyombo vya habari Vatican kwa waandishi wa habari,amethibitisha juu ya ziara ya kitume ya Papa Francisko huko Lisbon katika Siku ya Vijana Duniani(WYD)itakayoanza tarehe 2-6 Agosti.Papa atatimiza hija yake katika Madhabahu ya Fatima Agosti,5.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Kwa mujibu wa Msemaji wa Vyombo vya habari Vatican Dk Matteo Bruni kwa waandhsi wa Habari kuhusu ziara ya kitume ya Papa Francisko huko Lisbon katika dursa ya Siky ya vijana Dunina kuanzia tarehe 2-6 Agosti 2023, amesema kuwa “ kwa kuchukua fursa ya  Siku ya Vijana duniani na kwa kukubali mwalkio wa Mamlaka ya raia na ya kikanisa huko Ureno, Baba Mtakatifu Francisko atakwenda huko Lisibon kuanzia tarehe 2 hadi 6 Mei  mwaka huu kutimiza hija yake katika Madhabahu ya Fatima tarehe 5 Agosti.

Siku ya Vijana duniani, ni ya Nne kwa   Papa Francisko

Kwa mara ya pili, Papa Francisko atatembelea madhabahu ya  Maria, marudio ya maelfu ya mahujaji kila mwaka. Papa alikuwa ameitembelea  madhabahu hiyo mnamo tarehe 12 na 13 Mei 2017, katika fursa ya  kuadhimisha miaka 100 tangu tokeo la Bikira Maria huko Cova ya  Iria. Kuhusu Siku ya Vijana WYD, ni siku ya nne ya Vijana Duniani inayoongozwa na Papa Francisko  baada ya zile za Brazil (2013), Krakow (2016) na Panama (2019). Tukio hilo linaloleta pamoja mamilioni ya vijana kutoka mabara yote mwaka huu, kama ilivyotajwa, linafanyika katika mji mkuu wa Ureno. Hapo awali ilipangwa kwa 2022, kama Papa Francisko alivyokuwa ametangaza mnamo tarehe 27 Januari 2019 huko Panama, (WYD) ya XXXVIII ambayo ilihamishwa hadi sasa kwa sababu ya dharura iliyosababishwa na UVIKO-19. Mada iliyochaguliwa ni: “Maria akaondoka akaenda kwa haraka” (Lk 1:39), ambacho ni kifungu kutoka katika Injili ya Luka inayozungumzia juu ya Bikira Maria kumtembelewa binamu yake Elizabeti.

Mwaliko wa Papa

Katika ujumbe wa hivi karibuni kwa njia ya video, ulioelekezwa kwa washiriki wote, Papa alisisitiza mwaliko wake wa kushuhudia tukio hilo kwamba “Kushiriki katika Siku ni jambo zuri.” Papa kwa hiyo aliongeza kusema "wekeni matumaini hapo, wekeni matumaini”  alirudia  " kwa sababu tunakua sana katika siku kama hii. Hatutambui lakini mambo yanabaki ndani, maadili tuliyoyapata yanabaki ndani, uhusiano ambao tumekuwa nao na vijana wengine kutoka nchi zingine, mikutano, kila kitu kinabaki ndani na, zaidi ya yote, kuona nguvu ya vijana, na watu. Kanisa lina nguvu za vijana. Kwa hivyo endelea.”

22 May 2023, 16:37