Kongamano la Ekaristi Takatifu huko Quito,Equador
Na Angella Rwezaula, - Vatican.
Kongamano 53° Kimataifa (IEC2024) litafanyika huko Quito, nchini Ecuador, kuanzia tarehe 8 -15 Septemba 2024, kwa kuhitimisha na maadhimisho makuu ya “statio orbis” ya tukio. Mada kuu inayoongoza Kongamano hilo ni , “Fraternidad para sanar el mundo”, yaani. “Udugu kwa ajili ya kuponesha ulimwengu ambayo inatokana na neno la Kiinjili kuwa “Ninyi nyote ni ndugu” (Mt 23,8). Ishara hiyo inakumbusha uzoefu wa sasa wa kisinodi wa Kanisa, ambalo linaalika kugeuka kuwa mahali pa udugu wa ujumuishi, na uwepo wa kushirikisha na ukarimu wa kina.
Wimbo rasimi na Nembo
Tarehe 10 mei 2023 iliyopita, katika Makao makuu ya Baraza la Maaskofu Katoliki nchini Equador waliwakilisha Nembo na Wimbo Rasimi wa Kongamano hili. Katika Nembo hiyo unaonekana Msalaba, Moyo, Ekaristi na mji Mkuu wa Nchi hiyo. Kwa habari zaidi zinazohusiana na tukio hilo zinaweza zinapatikana katika mtandao wa Kamati ya Maandalizi:(www.iec2024.ec) na Tume ya Kipapa kwa ajili ya Makongamano ya Ekaristi Kimataifa: (www.congressieucaristici.va).