Dk.Ruffini:Filamu ni kurejesha uwezo wetu wa kuelewa&kuchukua hatua
Na Angella Rwezaula, - Vatican.
Kama ilivyokuwa imetaarifa hivi karibuni kwamba Filamu yenye kichwa In-Visibles’ itaweza kuonekana kwa mara ya kwanza mnamo Jumamosi tarehe 13 Mei 2023 asubuhi, wakati wa Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mashirika ya Wanawake Wakatoliki Duniani (UMOFC, WUWCO) ambao unaendelea Roma na Asisisi, kwa mujibu wa Bi Maria Lia Zervino, rais wa UMOFC, hatimaye Wanawake hao wameweza kuiona. Hata hivyo kabla ya kuweka filamu hiyo ya dakika 30 tu, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano, Dk. Paolo Ruffini alikuwa na yake ya kuelezea kuhusiana na filamu hiyo. Kwanza kabisa aliwasalimia na kuwaomba apate fursa ya dakika chache kuzungumza akiwa anawasindikiza katika mkutano wao. Pia alieleza furaha yake ya kuwa nao siku hiyo. Alifikiria kuwa Baraza la Kipapa la Mawasiliano na mawasiliano mema kwa ujumla, “yanawahitaji wao wote, yaani wanawake wote ili kushinda vita dhidi ya habari mbaya, ambayo inatufanya tufikiri kwamba uovu tayari umeshinda”.
Kuhusiana na filamu ambayo ingetolewa mchana, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano aliwahakikishia kuwa ingechapishwa kwenye tovuti za Vatican News, kwenye lugha nne. Kwa hiyo alisisitiza kuwa “Inastahili kutazamwa.”Na ni vizuri kwamba wangeiona wao kwa mara ya kwanza pamoja hapo. Mkuu wa Baraza la Mawasiliano Vatican, aliwahimiza kwamba baada ya kuitazama wazungumzie juu yake na kupendekeza kwa watu wengine wanaowafahamu ili waione kwenye majukwaa ya Vatican News na waishirikishe kwenye mitandao yao ya kijamii, kibinafsi na kitaasisi. Ni “filamu ambayo inahoji, kwa mfano, inahusu Afrika, Togo na Ghana hasa, lakini ni kwa ujumbla inawahusu wanawake, inahusu ulimwengu mzima pia. Inahusu upendo na utunzaji. Inaeleza juu ya maisha ya wanawake wengi wasioonekana, ili kurejesha uwezo wetu wa kuona, kuelewa, na kuchukua hatua ili kukomesha unyanyasaji wowote, kuanzia vurugu ya hila ya kutojali,” amesisitiza Dk. Ruffini.
Filamu hiyo, iliyoongozwa na Lia Beltrami, huku Sr. Eleonora Agassa akiwa mkurugenzi msaidizi, kwa hakika “inachambua historia, ikisimulia kupitia sanaa yake ya uzuri wa upendo, ya kuvunja tabia mbaya inayotufanya kuwa vipofu na viziwi. Inazungumza juu ya maisha na ili yaweze kutunzwa na kulindwa kila wakati”.
In-Visibles kama kichwa chake “inaonesha kwa hakika mateso ambayo hupitia maishani mwetu. “Pia inatuonesha jinsi wanawake watawa wanavyojua jinsi ya kusuka mtandao huu usioonekana wa upendo ambao unaruhusu mchakato huu kutoka kifo hadi uzima kutokea katika maisha ya wale wanaowahudumia. Jinsi wanavyozalisha na kurejesha maisha kama akina mama kwa haki yao wenyewe, kupitia upendo huo ambao daima ni wa ushindi”. Kama Papa ilivyoandika katika waraka wa Amoris Laetitia n168 kuwa: “Kila mwanamke anashiriki katika 'siri ya uumbaji, ambayo inafanywa upya kwa kila kuzaliwa'. Kwa hiyo Wanawake kama asemavyo Papa Francisko ndio wanaoifanya dunia kuwa nzuri, wanaoilinda na kuiweka kuwa hai. Dk. Ruffini amefafanua kuwa wanawake wanaleta neema inayofanya mambo kuwa mapya, kukumbatia kunajumuisha, ujasiri wa kujitoa.
Kwa njia hiyo sasa mtandao huu wa upendo unaotuunganisha sisi sote unaeleweka ambao umefumwa na wanawake. “Katika ulimwengu wetu ambao umegawanyika sana, tunahitaji sana watu wanaojua jinsi ya kufanya kile kisichoonekana kionekane, watu wanaotufundisha njia nyingine ya kuona mambo, ya kuona zaidi ya kuonekana, kwa macho ya upendo” Huo ni mtazamo wa “wale ambao hawageuzi visogo mbele ya maumivu na dhuluma, lakini ambao huinama juu ya maumivu hayo ili kuponya, na ambao wanakabiliwa na dhuluma ili kuukomboa, ambao daima wanafikiri kwamba upendo ni ushindi daima na kwamba maisha yatashinda na kuendelea”. Kwa hiyo Dk Ruffini amehitimisha kwamba “hivi ndivyo ulivyo. Hivi ndivyo mlivyo wanawake” Amewashukuru na kuwatakia wafurahi filamu hiyo.