Baraza la Kipapa la Mashirika ya Kitawa wako tayari na tovuti
Na Angella Rwezaula- Vatican.
Tovuti mpya ya Baraza la Kipapa la Mashirika ya Kitawa na vyama vya Kitume sasa liko mtandaoni (www.vitaconacrata.va). Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari kutoka Baraza hilo la Kipapa ni kwamba Tovuti, katika toleo lake jipya kabisa linalenga kuwa chombo cha mawasiliano na habari kwa kila mtu, hasa kwa wanaume na wanawake waliowekwa wakfu.
Ufikiaji wa haraka wa habari
Tovuti hiyo inakusanya habari, shughuli, nyaraka na machapisho ya Baraza lenyewe. Mbali na nyenzo na marejeo, pia ina baadhi ya machapisho ya Baraza hilo katika lugha mbalimbali, kuanzia barua kwa wanaume na wanawake waliowekwa wakfu zinazotolewa kwenye mwadhimisho ya kila Mwaka wa Siku ya Watawa duniani na nyaraka nyingine za Kipapa. Kwa hiyo, Injini ya utaftaji kwenye ukurasa wa nyumbani hunakuruhusu kupata habari zote kwa haraka.
Ishara ya ukaribu na kushiriki
Tovuti hiyo pia inataka kuwa ishara ya ukaribu na ushirikiano ambapo Baraza la Kipapa hilo linakusudia kukubali mwaliko wa Papa, uliotolewa na Papa Francisko katika Ujumbe wa Siku ya Mawasiliano Duniani 2023: “Nina ndoto ya mawasiliano ya kikanisa ambayo yanajua jinsi ya kujiruhusu kuongozwa na Roho Mtakatifu, mpole na wakati huo huo wa kinabii, ambaye anajua jinsi ya kupata aina mpya na njia za tangazo la ajabu ambalo ameitwa kuleta kwenye milenia ya tatu”, alisisitiza Papa katika ujumbe wake hivi karibuni.