Ujumbe wa Papa wa Siku ya 60 ya Kuombea Miito Duniani kwa mwaka
Na Angella Rwezaula, - Vatican.
Katika uwakilishi wa Ujumbe wa Papa Francisko wa Siku ya 60 ya Kuombea Miito Duniani kwa mwaka 2023 kwa waandishi wa vyombo vya habari, Kardinali Lazzaro You Heung-sik, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Wakleri ameshukuru uwepo wake hapo, akiwa kama sauti ya hisia za wahudumu wake wa Baraza hilo kwamba kwa pamoja katika mwaka ambao ni kumbu kumbu ya miaka 60, tangu kuanzishwa kwa Siku ya Kuombea Miito duniani iliyoanzishwa na Mtakatifu Paulo VI mnamo 1964, wamefikiria kushirikishana Ujumbe wa Baba Mtakatifu ambao muda mfupi ungechapishwa. Lengo la Siku hiyo kiukweli ni unabii wa Papa wakati alikuwa katikati ya Mtaguso wa II wa Vatican. Hii ni fursa kwa ajili ya kuita furaha ya kukutana na Yesu ambaye anaokoa dhidi ya huzuni wa maisha yaliyofungwa ndani ya ubinafasi, inapanua upep na kujaza moyo(rej. Evangelii gaudium, 1-2). Utamu na kutiwa moyp furaha ambayo inatokana na kukutana na Yesu ni kile ambacho kinaruhusu kila mmoja wao kugundua wito wake: kuwa Mungu kiiukqweli aliota ndoto ambayo anatamani kuotimiza kwa sisi na yuko nasi katika mpango ambao utasindikiza kwa sababu, katika kumpokea na kujikamilisha kwa uhuru wote, tunaweza kupata maana ya kweli ya maisha na kutimiza ubinadamu wetu, lakini hatua utume kwa njia ya mchango wa ujenzi wa ulimwengu wa kidugu zaidi , haki zaidi, mshikamano zaidi , uliotanguliza na kutimiza Ufalme wa Mungu.
Baba Mtakatifu Francisko, katika Ujumbe wake kwa Siku ya 60 ya Kuombea Miito Duniani, anasisitiza kwa uthabiti huu "mabadiliko ya kukutana" kati ya Mungu na mwanadamu, ambayo ndiyo kiini cha kile tunachomaanisha kwa neno "wito". Na anatusihi tugundue tena ukuu wa Mungu, kwa sababu pale tu tunapotoa nafasi kwa ajili yake na wito wake, ndipo maisha yetu yanastawi na uhuru wetu unatambulika katika wema na ukweli. Baba Mtakatifu anafanya uchaguzi sahihi: kuanza kutoka kwa Mungu, kutoka kwa neema yake, kutoka kwa baba na maombi yake ambayo anasonga kwetu, kuja na kututafuta na kuzungumza nasi "kama na marafiki" (Dei verbum, 2). Ni kutokana tu na zawadi ya bure na ya ukarimu ya urafiki ambayo Bwana huja kukutana nasi ndipo kuna uwezekano wa kutekeleza utume katika maisha yetu, katika Kanisa, katika jamii na katika historia. Kwa ufupi, utume wetu hapa duniani unazaliwa kutokana na neema ya Mungu!
Neema na utume basi, ni nguzo mbili na vipimo viwili vya msingi vya kila wito na, kwa hiyo, ni maneno mawili ambayo Papa Francisko anakazia katika Ujumbe wake. Mungu alituumba kwa upendo na kwa upendo na, kwa hiyo, kugundua wito wetu wenyewe, katika maisha ya kibinafsi, katika Kanisa, katika jamii, upeo tunaoingia ili kufungua wenyewe kwa furaha lazima uwe wa upendo: maisha yaliyotolewa, maisha ambayo yanahatarisha mipango ya upendo kushinda majaribu ya hesabu na ubinafsi, na kuruhusu sisi wenyewe kuongozwa na"Ndoto ya Mungu anayetuita". Mpango huu wa Mungu unangoja mwitikio kutoka kwetu na, tusipobakia kutojali, hatuinyimi sauti ya Mungu, hatukatai mwaliko wake wa "kuruka juu", basi wito wake unakuwa thabiti katika utume, katika uchaguzi wa maisha na kujitolea kunakopatikana katika mambo ya kila siku, katika maeneo tunayotembelea mara kwa mara, kwa maneno na mitazamo tunayoishi, katika kila hali.
Kardinali Lazzaro alisema haikwepeki taarifa yake kwamba, kama mwaka 2022, Ujumbe tena mwaka huu 2023 unaweka lafudhi juu ya wito wa kujitolea, wa kawaida kwa Wakristo wote: wote wameitwa kuwa mstari wa mbele, kufanya sehemu yao ili dunia inaweza kuwa makao ya kawaida ambamo watu mmoja-mmoja na watu wanaishi pamoja kama kaka na dada, chini ya macho ya Baba mmoja. Hii bila shaka ndiyo maana kamili na ya kina ya safari ya sasa ya sinodi ambayo Papa Francisko ametualika: kutembea pamoja, lakini kwenda mbele. Na katika hili kila mwanamume na mwanamke aliyebatizwa, bila ubaguzi, ana sehemu ya utendaji, hadi kufikia hatua ya kuweza kusema juu yake mwenyewe: "Mimi ni utume juu ya dunia hii, na hii ndiyo sababu niko katika ulimwengu huu" (Wahimizo la Kitume. Evangelii gaudium, 273). Katika maneno ya Papa Francisko aliyochagua ya Ujumbe huu, kwa hiyo tunaweza kugunda moyo wenyewa wa habari njema ya Injili, kila mmoja weru anayo nafasi katika moyo wa Mungu, bila kubaguliwa, kila mmoja wetu alifikiwa , aliumbwa na kuitwa kwa upendao na daima, kila mmoja weru ameita na Baba na ametumwa katika ulimwengu na katika kanisa kama ishara hii ya upendo.
Kardinali, You amesema na huru unaokoa ni mwaliko hata kwa Kanisa. Kiukweli awali ya ya yote kwa Kanisa ambalo linapaswa kupeleka habari njema ulimwenguni. Ni Kanisa ambalo kwa uso mpole na mikono iliyopanuka lazima kujua kusema kwa kila mwanamke na kila mwanaume kuwa umependwa na Mungu, na Bwana yupo kwa ajili ya maisha yako. Kwa hiyo katika utofauti na wingi wa karama zake, Jumuiya ya Kikristo inaalikwa kuwa mahali pa makaribisho ambako hakubagui yoyote kamwe na kuweka vizingiti vya ugwiji wa Rohi, bali ni ambalo linasaidia wote kugundua wito wake. Kazi ambayo inahitaji juhudi za walei na wachungaji zifanyike, kila mmoja na kila hisia binafsi, na kila mchakato wa maisha kwa ajili ya kuvuka kizingiti cha Jumuiya ya Kikristo inaweza kupata zana inayofaaa kwa ajili ya utafiti wa furaha yake binafsi na kugundua mpango wa Mungu, kwa ukimya, sala, kusikiliza na kutambua (kung’amua). Kila mtu anahitaji, leo hii kuliko hapo awali, Kanisa moja linalo sindikiza ambalo linamshika mkono na kufanya kuwa karibu katika safari ya kila mmoja, kwa kupokea maswali na kumsadia hatua zake. Na kama matashi ya Papa Francisko tutaweza kupanua kila mahali nafasi ya upendo.
Kwa upande wa Afisa wa Baraza la Kipapa la Wakleri Monsinyo Eamonn Mclaughlin, katika kitengo cha Uchungaji alisema kuwa katika kila parokia ingefaa kubainisha mtu (padre, mtawa au mlei) au kikundi cha waamini chenye jukumu lakuendeleza uchungaji wa miito. Anatumaini kwamba, Vituo vya Miito vitaanzishwa na kukuzwa katika Majimbo, Mikoa na nchi binafsi, vinavyoitwa kuendeleza daima huduma ya kichungaji ya miito. Na anawaalika kila mtu, kama aliyebatizwa, sio tu kushirikiana, lakini kuwajibika kwa mpango huu maalum wa Kanisa. Monsinyo Mclauhhlin alisema:"katika kazi ya uinjilishaji ya Kanisa, kuzaliwa, kusindikiza na utambuzi wa miito, hasa ile ya ushemasi na ukuhani ina umuhimu wa kipekee. Jumuiya ya Kikristo, kwa hiyo, inaona haja ya kukuza miito ya kipadre, kwa kushirikiana na neema ya Mungu kuendeleza utume wake. Papa anavyoandika katika ujumbe wake: tunaitwa kushuhudia imani. Katika kazi hii, mchango mkubwa sana unatoka kwa familia, ambazo, kama Mtakatifu Paulo VI alivyokumbuka, ikiwa zimehuishwa na roho ya imani, mapendo na utauwa, zinaunda seminari ya kwanza, na pia kutoka kwa jumuiya za parokia.
Wajibu wa pekee wa huduma ya kichungaji ya miito ni ya wale wanaotunza elimu ya vijana, ili kuwasaidia, kuwasindikiza na kuwatia moyo kugundua wito wa kimungu wa kumfuata Bwana kwa imani, matumaini na mapendo. Kwa hiyo, mapadre wana mtazamo maalum wa upendo kwa ajili ya kukuza miito ya ukuhani. Ushuhuda wa mapadre wanyenyekevu na wenye furaha, ambao wanaishi maisha matakatifu na yenye uwiano, walio katika upendo na Bwana na wanaonuka arufu ya kondoo, kwa hakika unaweza kuwatia moyo wengi kumfuata Kristo. Maaskofu, kama wale ambao kimsingi wanawajibika kwa wale walioitwa katika maisha ya kihuduma, pia kwa ushuhuda wao kama wachungaji wema, wanakuza ushirikiano kati ya mapadre, watu waliowekwa wakfu na walei (zaidi ya wazazi na waelimishaji wote) na pia na walei, vuguvugu na vyama ndani ya kanisa. mpango mwafaka wa uchungaji. Sisi sote tuliobatizwa sio tu washiriki bali tunawajibika pamoja kwa mpango huu mahususi wa Kanisa. Kwa hiyo, maombi yetu sote yainue Mbinguni, ili miito izaliwe na kukua, kulingana na Moyo wa Yesu, Kuhani Mkuu na wa Milele".