(Giovanni Battista Montini) lilikuwa jina la Ubatizo la Mtakatifu  Papa Paulo VI. (Giovanni Battista Montini) lilikuwa jina la Ubatizo la Mtakatifu Papa Paulo VI. 

Tuzo ya VI kimataifa 2023 itatolewa na Papa Francisko

Taasisi ya Paulo VI,inayo hamasishwa na Kazi kwa ajili ya Elimu ya Kristo ya Brescia,imetangaza utoaji wa utambuzi wa kimataifa tarehe 29 Mei 2023 baada ya kusimama kwa miaka michache.Mkutano na waandishi wa habari wa uwakilishi utakuwa tarehe 19 Aprili 2023 ambapo wataeleza majina ya waliochaguliwa katika toleo 2023.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Tarehe 29 Mei 2023, katika Ukumbi wa Clementina wa Jumba la Kitume, Baba Mtakatifu Francisko anatarajia kukabidhi Tuzo ya Kimataifa ya Paulo VI, katika maadhimisho ya miaka 60 ya kuchaguliwa kwa Papa Montini kwenye kiti cha upapa. Jina la mtu atakayetunukiwa mwaka huu 2023 atatangazwa Jumatano  tarehe 19 Aprili, 2023 saa 12.00 kamili, wakati wa mkutano na waandishi wa habari ambao utafanyika katika Ofisi ya Vyombo vya Habari vya Vatican.

Baada ya kusimama kwa muda sasa wanapyaisha utoaji wa tuzo

Taarifa kwa vyombo vya habari kutoka kwa taasisi inayohamasisha  Tuzo hiyo, Taasisi ya Paulo VI ya Brescia, iliyoanzishwa mara  baada ya kifo cha Montini kwa mpango wa Kazi ya Elimu ya Kikristo ya Brescia kama Kituo cha Mafunzo na Hati juu ya takwimu, kazi na mafundisho ya Yohane Mbatizaj Montini-Paolo VI, inaarifu kwamba “baada ya miaka michache ya kusimamishwa, sasa ameanzishwa tena utoaji wa Tuzo, ili kumulika watu mashuhuri ambao wamejitofautisha katika nyanja mbali mbali za kiutamaduni na katika kuhamasisha kuishi pamoja kwa haki ya binadamu na ambayo, kwa njia tofauti, inashuhudia uhai wa urithi wa kiroho wa Paulo VI.

Miongoni mwa washindi wa matoleo yaliyopita

Miongoni mwa washindi wa matoleo yaliyopita Ni : Hans Urs von Balthasar kwa masomo ya taalimungua (1984), Olivier Messiaen kwa muziki (1988), Oscar Cullmann kwa Uekumene (1993), Paul Ricoeur kwa falsafa (2003) na Mfululizio wa vitabu vya Vyanzo wa Ukristo (Sources Chrétiennes) kwa ajili ya elimu (2009).

15 April 2023, 10:10