Tuzo ya Reporter della Terra”kwa Osservatore Romano
Na Angella Rwezaula, - Vatican.
Kama sehemu ya tukio la OnePeopleOnePlanet ambalo lilifanyika katika Ukumbi wa Nuvola di Fuksas huko Eur jijini Roma, tuzo ya ‘Earth Reporter’ ilitolewa kwa wahariri wa Osservatore Romano Jumamosi tarehe 22 Aprili 2023. Kupitia Marathon kwa njia ya televisheni ambayo ilikuwa ni sehemu ya matukio mengi yaliyoandaliwa katika siku za hivi karibuni na EarthDay Italia katika muktadha wa Siku ya Kimataifa ya Mama Sayari Dunia.
Tuzo hiyo ambayo pia ilitolewa kwa magazeti mengine, ni kutambua dhamira iliyotolewa kwa ajili ya masuala ya mazingira na uhamasishaji. Hasa, mwandishi wa habari Chiara Giallonardo (naye tayari alipewa utambuzi sawa katika matoleo ya awali), katika kutoa tuzo kwa mkurugenzi wa Osservatore Romano, Bwana Andrea Monda, alisisitiza pia mpango wa kila mwezi wa Gazeti la Osservatore kwa njia ndefu ambayo inakusudia kutoa huduma ya watu katikati na utambuzi wa hadhi ya kila mwanadamu, hata aliye mdogo zaidi na aliyetengwa.
Bwana Monda aidha alikumbuka kwamba kwa miaka kadhaa Gazeti la Osservatore Romano na Radio Vatican wameunda hata nafasi na vipengele hasa kwa mpango wa unaoongozwa na Waraka wa Papa Francisko wa Laudato si' ambao unasimulia historia zinazohusiana na mada ya utunzaji wa nyumba ya Kawaida na kutaka kutaja majina ya baadhi ya wafanyakazi wenzao wanaohusika na mpango huo kama vile Giada Aquilino, Cecilia Seppia na Marco Bellizi.