Tafuta

2023.04.26 Kardinali Hollerich na  Grech Katika Ofisi ya Habari Vatican kuwakilisha mambo mapya ya Sinodi. 2023.04.26 Kardinali Hollerich na Grech Katika Ofisi ya Habari Vatican kuwakilisha mambo mapya ya Sinodi. 

Sinodi,mapya yaliyojiri:walei wana haki ya kupiga kura&50% ni wanawake

Mambo mapya yaliyonzishwa na mabadiliko ya muundo wa washiriki katika Sinodi ya Oktoba,Vatican:Washiriki 70 wasio maaskofu ni sehemu ya mkutano pia kupiga kura,waliotambuliwa na Mabaraza ya Maaskofu na Mabaraza ya Makanisa ya Mashariki na kuteuliwa na Papa.Wanawake wawe 50% na uwepo wa vijana uthaminiwe:Sio mapinduzi,lakini ni utajiri wa Kanisa.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Jumatano tarehe 26 Aprili 2023 imewakilishwa  kwa waandishi wa vyombo vya habari kuhusu mambo mapya katika eneo la mkutano katika Ofisi ya Vyombo vya Habari vya Vatican. Kwa hiyo haitabadilika, Asili wala jina  ambalo linabaki kuwa Sinodi ya Maaskofu, lakini kinachobadilika ni muundo wa washiriki katika mkutano ujao wa mwezi Oktoba mjini Vatican kuhusu mada ya sinodi. Kwa njia hiyo  washiriki wasio maaskofu yaani walei pia watakuwapo  walioteuliwa moja kwa moja na Papa na asilimia 50% yao imeombwa iwe ni wanawake. Ombi la wazi ni pamoja na lile la kuthamanisha uwepo wa vijana. Kila mtu atakuwa na haki ya kupiga kura, kufikia idadi ya washiriki wa kupiga kura katika Ukumbi Mpya wa Sinodi wenye takriban  kati ya  washiriki 370 zaidi ya washiriki 400 kwa ujumla. Haya ndiyo mabadiliko msingi na mapya yalioanzishwa tarehe 26 Aprili 2023 na Papa kwa ajili ya Sinodi ambayo yatatia mhuri wa sinodi aliyoanzisha mwenyewe mnamo mwaka 2021 katika kipindi cha vuli. Kwa mujibu wa makardinali Makadinali Mario Grech Katibu mkuu wa Sinodi na Jean- Claude Hollerich mratibu  mkuu, wa Sinodi kwa waandishi wa habari wakati wa uwakilishi wamebainisha kuwa haya “Sio mapinduzi bali ni mabadiliko muhimu na  ni utajiri wa Kanisa ambalo litakuwa kamili zaidi.”

Washiriki wa wasio maaskofu

Masharti hayo mapya, yaliyowasilishwa tarehe 26 Aprili  katika barua kwa wakuu wa Mabaraza ya Bara yaliyoadhimisha Sinodi za kibara  katika bara la Afrika, Asia, Mashariki ya Kati na Australia, hayatafutilia mbali sheria ya sasa, ya katiba ya kitume Episcopalis Communio ya 2018 ambayo tayari ilikuwa inaonesha uwepo wa “wasio maaskofu”. Kwa habari iliyotolewa na ambayo ina hakika katika muktadha wa mchakato wa sinodi ambao Papa Francisko alitaka kuanza kutoka chini imebainishwa kuwa idadi ya watu ni  70 ambao nni Mapadre, watu waliowekwa wakfu, mashemasi, walei, wanaotoka katika Makanisa mahalia na kuwawakilisha Watu wa  Mungu. Kwa maana hiyo hakutakuwapo tena na “wasikilizaji”.

Mkutano Mkuu wa Maaskofu

Sekretarieti Kuu ya Sinodi imeeleza kuwa Uamuzi huu unaimarisha uthabiti wa mchakato kwa ujumla, unaojumuisha katika Mkutano kumbukumbu hai ya awamu ya maandalizi, kupitia uwepo wa baadhi ya waliohusika katika hilo. Kwa namna hiyo umaalum wa Mkutano wa Sinodi  ya Maaskofu hauonekani kuathiriwa, bali hata kuthibitishwa. “Tunazungumza juu ya  asilimia 21% ya Mkutano ambao unabaki kuwa Baraza la Maaskofu, pamoja na ushiriki fulani wa wasio maaskofu”, Kardinali Hollerich alisisitiza tena. “Kuwepo kwao kunahakikisha mazungumzo kati ya unabii wa watu wa Mungu na utambuzi wa wachungaji.”

Uchaguzi na uteuzi

Katika maelezo yao wanabainisha kuwa zaidi hasa, washiriki “wasio maaskofu” wanateuliwa na Papa kutoka katika orodha ya watu 140 waliotambuliwa na Mabaraza ya Maaskofu na Baraza la Mababa wa Makanisa Katoliki ya Mashariki (20 kwa kila moja). Kama ilivyotajwa, inaombwa nusu ya wanawake na vijana wathaminiwe: “Kwa sababu ulimwengu wetu uko hivvyo”, makadinali hao wawili walisema. Katika uchaguzi unazingatia ujuzi kwa ujumla, ‘busara’, lakini pia ujuzi na ushiriki katika mchakato wa kisinodi. Kwa hiyo kama wajumbe, wana haki ya kupiga kura. Mantiki  muhimu, hata kama Kardinali Grech amebainisha“kwamba siku moja tutaweza kufanya bila kura. Kwani Sinodi ni utambuzi, sala, hatukai nyuma ya kura.”

Watawa wa kike watano na kiume watano

Watawa watano wa kike na watano wa kiume waliochaguliwa na mashirika husika ya Wakuu wa Mashirika Makuu na Wasimamizi Wakuu (Uisg kwa tawi la wanawake na Usg kwa tawi la wanaume) pia watakuwa na haki ya kupiga kura. Kwa upande wao ni jambo jipya  nyingine wanaochukua nafasi ya Watawa kumi wa taasisi za maisha Kitawa  iliyotabiriwa huko nyuma. Chaguzi zote zilizofanywa katika mkutano na kura za siri na Sinodi, Vikao na Mabaraza ya Maaskofu husika, lazima ziidhinishwe na Papa. Majina ya waliochaguliwa hayajulikani kwa umma hadi Papa atakapothibitisha uchaguzi huo.

Wawezeshaji

Jambo jingine jipya ni kwamba Mkutano pia utahudhuriwa,  lakini bila haki ya kupiga kura na ‘wataalam’, watu wenye uwezo katika nyadhifa mbalimbali juu ya mada inayojadiliwa. Pia kutakuwa na wajumbe wa Udugu(Fratenity), washiriki wa Makanisa mengine na Jumuiya za Kikanisa,na kwa mara ya kwanza, zitajitokeza kwenye Sinodi, sura za “wawezeshaji” pia wao  ni wataalam watakaowezesha kazi hiyo kwa nyakati mbalimbali.  Kardinali Grech alielezea, kuwa ni chaguo, lililozaliwa kutokana na uzoefu wa vikundi vya utafiti ambavyo viliwaonesha kuwa wataalam hawa wanaweza kuunda nguvu ambayo inaweza kuzaa matunda.  Kadhalika kuna maaskofu ambao hawajawahi kushiriki katika Sinodi, kwa hiyo hali ya kiroho lazima iwezeshwe,  alifafanua Kardinali Hollerich, huku akisisitiza kwamba kwa mara ya kwanza pia kutakuwa na maaskofu kutoka katika nchi ambazo hazina Baraza la Maaskofu. Luxembourg ni mojawapo ya nchi hizo, lakini pia kuna  Estonia, na Moldavia. Hivyo, makadinali hao wawili walikubaliana, kuwa “Kanisa litakuwa kamili zaidi na itakuwa ni furaha kuwa kuliunganisha tena zima  jijini Roma.”

26 April 2023, 18:20