Mandalizi ya Sinodi Ijayo yanaendelea:Kuanzia 12-19 Aprili 2023 ni kamati ya kuandaa kitendea Kazi. Mandalizi ya Sinodi Ijayo yanaendelea:Kuanzia 12-19 Aprili 2023 ni kamati ya kuandaa kitendea Kazi.  (Vatican Media)

Sinodi:kazi inanzia kwenye Instrumentum Laboris ya mkutano wa Oktoba

Kwa muda wa Juma moja,wataalamu kutoka nchi zote wataanzisha tafakari itakayopelekea kuandikwa kwa waraka wa kitendea kazi kwa ajili ya kikao cha kwanza cha Mkutano Mkuu wa XVI wa Kawaida wa Sinodi ya Maaskofu.Kwa hiyo mkutano wa maandalizi ni kuanzia 12-19 Aprili 2023 mjini Vatican.

Na Angella Rwezaula,- Vatican.

Kuanzia Jumatano tarehe 12 hadi  19 Aprili,kundi la wataalam kutoka mabara matano na ambao wameshiriki katika mchakato wa sinodi katika nyadhifa mbalimbali, wanakutana kwenye Sekretarieti Kuu ya Sinodi kwa muda wa kufanya kazi na utambuzi juu ya Hatua ya Bara na hati saba za mwisho za Mikutano ya Sinodi ya Bara kwa lengo la kuanzisha tafakari ambayo baadaye itatoa ufafanuzi wa Instrumentum Laboris,yaani hati ya kufanya kazi katika kikao cha kwanza cha Mkutano Mkuu wa XVI wa Kawaida wa Sinodi ya Maaskofu, kuanzia tarehe 4 hadi 29 Oktoba ijayo.

Mikutano ya Sinodi ya Bara

Baada ya muda wa maombi na kipindi cha utangulizi, kazi zinaonesha ushiriki mpana katika Jukwaa zima la Bara na uzoefu ulioishi wakati wa makusanyiko saba ya sinodi ya bara. Baadaye, Nyaraka za Mwisho zilizotumwa kwa Sekretarieti Kuu ya Sinodi, matunda ya utambuzi wa jumuiya ya Watu wa Mungu, zitachambuliwa kwa kina ili kubainisha mivutano na vipaumbele vinavyopaswa kuchunguzwa wakati wa kusanyiko la mwezi Oktoba ijayo. Siku hizo zitaadhimishwa na adhimisho la kila siku la Ekaristi na nyakati za sala ya kibinafsi na ya jumuiya. Mkutano huo utafanyika kwa milango iliyofungwa. Na mwishoni mwa mkutano, mkutano na waandishi wa habari utafanyika tarehe 20 Aprili 2023. Taarifa zaidi kuhusu hili zitawasilishwa moja kwa moja na Ofisi ya vyombo vya habari Vatican..

Washiriki

Wanaoshiriki katika kazi hizo mo : Makadinali Mario Grech na Jean-Claude Hollerich, Monsinyo Luis Marin de San Martín, Sr Nathalie Becquart, Monsinyo Timothy Costelloe, Monsinyo Lucio Andrice Muandula, Monsinyo Daniel Flores, Monsinyo Pierangelo Sequeri, Monsignor Codamasz Monsignor Trafny, Padre Giacomo Costa, Padre Dario Vitali, Dada Shizue Hirota, Padre Giuseppe Bonfrate, Profesa Myriam Wylens Profesa. Anna Rowlands, Maprofesa Myriam Wylens na Anna Rowlands, Padre Pasquale Bua, Sr. Marie-Kolbe Zamora, Paolo Foglizzo, Thierry Bonaventura, Susan Pascoe mtandaoni pamoja na Mauricio López Oropez, Paolo Foglizzo, Thierry Bonaventura, Susan Pascoe na kwa njia ya mtanadano na Mauricio Lopez Oropeza.

Mkutano wa kuandaa Kitenda kazi cha Sinodi ya Oktoba ijayo
12 April 2023, 16:22