Siku ya Wazee ni fursa ya kurejesha hadhi kwa wale waliokataliwa
Na Angella Rwezaula, - Varican.
Mnamo Dominika tarehe 23 Juali 2023,inatarajiwa kuadhimishwa Siku III ya Kimataifa ya Babu na wazee. Mada iliyochaguliwa na Baba Mtakatifu ni “Huruma zake kizazi hadi kizazi"(Lk 1,50) ambayo inajea uhusiano na Siku ya Kimataifa ya Vijana (WYD) ambayo itakuwa imefanyika siku huko Lisbon nchini Ureno kuanzia tarehe 1-6 Agosti 2023). Siku ya Kimataifa ya Vijana (WYD) inaongozwa na kauli mbiu “Maria aliamka na kwenda kwa haraka”(Lk 1,39) ambayo inatuonesha kiukweli, kijana Maria alijiweka katika safari kwenda kumtembelea binadamu yake mzee Elizabeth na ambaye alitamka kwa sauti kuu ya Kusifu (Magnificat) nguvu ya uhusiano kati ya vijana na wazee, alisema Papa Francisko.
Katika fursa ya Siku ya vijana, Baba Mtakatifu anatarajia kuadhimisha liturujia ya Ekaristi takatifu katika Uwanja wa Mtakatifu Petro na ambapo wanaalikwa Parokia zote, majimbo yote, na vyama mbali mbali na jumuiya za kikanisa duniani kote, kuadhimisha Siku hiyo katika muktadha huo wa kichungaji. Kwa mujibu wa Baraza la Kipapa la Walei, Familia na Maisha wanajikita katika kujenga Kanisa moja ambalo linachangamotisha utamaduni wa ubaguzi kwa furaha iliyokaa ya mkubati mpya kati ya vijana na wazee, kama alivyosema Papa Francisko wakati wa katekesi yake mnamo tarehe 11 Machi 2015. Kwa sababu hiyo, siku hiyo inataka kukuza na kuunga mkono uenezaji wa huduma ya kichungaji ya wazee inayojua kuthamini wito wao wa pekee katika Kanisa kuanzia katika kusambaza imani hadi kwa mdogo zaidi, kutoka katika ulezi wa mizizi na kutoka katika yale yanayoweza kuwa ya kuzingatiwa utume halisi wa uzee na ya kuombea katika sala.
Mnamo mwaka wa 2020, Barazala la Kipapa la Walei Familia na maisha walianza kuhamasisha Kongamano la I la Kimataifa juu ya utunzaji wa kichungaji wa wazee kwa kuongozwa na mada “Utajiri wa miaka” kuhusu tukio hilo linaweza kusomeka katika E book ambapo inaweza kupakuliwa kwa uhuru kutoka kwa tovuti ya Baraza la Kipapa ya Familia. Na tangu mwaka wa 2021, Baraza hilo limekuwa likihimiza maadhimisho ya Siku ya Bibi na Babu na Wazee Duniani. Tukumbuke kuwa, mnamo Mwaka 2022 katika siku ya II ya Kimataifa ya Wazee, kwa upende wa Afrika, ilikuwa ni fursa ya kuwaweka wazee katika kitovu cha wasiwasi wa kichungaji wa majimbo mengi. Pia Papa Francisko alikutana na vijana na wazee huko Canada mwezi Julai.