Tafuta

Monsinyo Fernando Ocariz Brana, Mkuu wa Opus Dei alipokutana na Papa Monsinyo Fernando Ocariz Brana, Mkuu wa Opus Dei alipokutana na Papa  (Vatican Media)

Opus Dei,Kongamano la muktadha wa Motu Proprio‘Ad charisma tuendum’

Siku tatu za kazi,kuanzia 12-17 Aprili 2023 jijini Roma limefunguliwa kongamano la kurekebisha sheria kuhusiana na hati ya Papa ambaye aliamuru kuhamishwa kwa uwezo wa Baraza la Maaskofu lililopita,akithibitisha kwamba mkuu hawezi tena kutunukiwa agizo la kiaskofu.Wanaudhuria ni wanachama 274 wa Opus Dei kutoka mabara matano.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Kuanzia tarehe 12 hadi 17 Aprili 2023, waamini 274 wa Opus Dei kutoka sehemu mbalimbali za dunia wanakusanyika mjini Roma pamoja na askofu na makasisi wake kutafakari kuhusu kanuni za awali na kuzipatanisha na Motu Proprio  ya “Ad Charisma Tuendum” ambayo Papa Francisko aliomba kupyaishwa kwa baadhi ya vipengele vya  hati ambayo inafafanua utume na kudhibiti maisha ya prelature ( yaani mkuu wa shirika hilo.

Kazi ya maandalizi ya kongamano hilo

Motu proprio ilirekebisha vifungu viwili vya Katiba ya Kitume Ut Sit (ambayo Opus Dei ilifanywa utangulizi mnamo 1982 ili kuzirekebisha na kuendana kwa sheria iliyolchapishwa hivi karibuni na Katiba ya Kitume ya Praedicate Evangelium, ya Curia Romana. Katika makala yake ya tatu, waraka huo unaongeza kwamba Sheria za Opus Dei zipaswa kurekebishwa ipasavyo kwa pendekezo la Mkuu wa Shirika lenyewe, ili kuidhinishwa na vyombo vyenye uwezo wa makao  makuu ya Kitume" (Ad charisma tuendum, n. 3). Kwa utangulizi huo, Mkuu wa  Opus Dei, Fernando Ocáriz, ameitisha kongamano maalum. 

Mapendekezo madhubuti

Hapo awali, Mkuu alikuwa ameomba ushiriki wa waamini wote wa baraza la kabla ambao walitaka kutoa mapendekezo maalum juu ya mada hiyo. Katika ujumbe wa tarehe 30 Machi 2023, alielezea lwamba “Mapendekezo hayo yalichunguzwa Roma, kwa msaada wa wataalam, kuwasilisha mapendekezo madhubuti katika Kongamano. Yale ambayo hayakuhusu ombi la Vatican yaliyo katika motu proprio yanaweza kuzingatiwa, kama nilivyoandika katika ujumbe wa mwezi Oktoba, katika majuma yajayo ya kazi, yaliyoitwa mara moja,na yatatumika kuandaa Kongamano Kuu la Kawaida la 2025. Ni nyenzo ya thamani, ambayo ningependa kuwashukuru tena.”

Kumsikiliza Roho, kuambatana na mafundisho ya mwanzilishi

Wanawake 126 na wanaume 148, wakiwemo mapadre 90, watashiriki katika mkutano huu mkuu. Washiriki wanatoka Afrika (6.6%), Amerika (36%), Asia (6.2%), Ulaya (50%) na Australia (1.1%). Mnamo  tarehe 12 Aprili 203, kabla ya kuanza mikutano, Padre ameongoza iibada ya Misa takatifu ambayo kwayo vikundi vya kazi vimeanza. Matokeo yatakayojitokeza kwa siku hizi yatawasilishwa kwenye Baraza la Makasisi. Mkuu wa Opus dei Ocáriz tayari alikumbusha kwamba “Kongamano Kuu zote ni nyakati maalum sana za umoja katika Kazi yote, na za Kazi na Baba Mtakatifu na Kanisa zima. Katika majauma haya kwa hiyo amesema wanataka  kukumbuka hasa nia ya Mtakatifu Josemaria: Omnes cum Petro ad Iesum per Mariam (Wote pamoja na Petro, kuelekea Yesu, shukrani kwa Maria)”. Mkuu wa Opus Dei amesema  husaidia kukutana na Yesu kazini, katika maisha ya familia na katika mzunguko nzima wa shughuli za kila siku. Leo hii  watu 93,600 ni wa wanchama, ambapo asilimia 60% ni wanawake. Kuna watu wengi zaidi ambao, wakiwemo washiriki na marafiki wa waamini wa Opus Dei, wanashiriki katika shughuli za malezi ya Kikristo zinazoandaliwa na watu wa Opus dei.

12 April 2023, 16:30