Kubaliano kati ya Vyombo vya habari Vatican na Laterano kuhusu huduma za kihariri
Na Angella Rwezaula, - Vatican.
Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano Dk. Paolo Ruffini na mkuu wa Chuo Kikuu cha Kipapa cha Lateran Dk. Vincenzo Buonomo tarehe 13 Aprili 2023 walitia saini makubaliano yenye lengo la kusimamia shughuli za uhariri wa chuo kikuu cha Papa. Kwa mujibu wa taarifa, inasemomeka kuwa Makubaliano hayo yataruhusu uzalishaji wa kazi na majarida ya kisayansi ambayo yanajumuisha mchango unaotolewa na Chuo Kikuu kwa jumuiya ya kimataifa ya wasomi”. Kazi zilizoundwa ndani ya mfumo wa makubaliano hayo zitakuwa na alama za kibiashara zilizosajiliwa za Chuo Kikuu cha Laterano (University Press-Pontificia Universitas Lateranensis) na Duka la Vitabu Vatican.
Mada za vitabu
Vitabu hivyo ambavyo pia vipo katika mfululizo, vinatofautiana katika nyanja mbalimbali za kinidhamu, kitaalimungu, kifalsafa, kisheria, sayansi ya amani na ushirikiano wa kimataifa, ikolojia na mazingira na hivyo vinaambatanishwa na uchapishaji wa mara kwa mara wa majarida ya kifahari Apollinaris kwa ajili ya kanuni na sheria za kanoni na kiraia (utroque jure, Aquinas kwa ajili ya falsafa, Lateranum kwa ajili ya Taalimungu, Studia e Documenta Historiae et Iuris) kwa sheria ya Kirumi na historia ya kisheria na Mapitio ya Sheria ya Laterano kwa sheria linganishi na sheria za kimataifa kwa sasa iliyochapishwa mtandaoni".
Utekelezaji wa Praedicate Evangelium
Makubaliano hayo, hayo, yanaenda sambamba na utekelezaji wa masharti ya Katiba ya Kitume Praedicate Evangelium, ambayo katika ibara ya 183 inakielelezo, katika umoja wa kimuundo na kwa kuzingatia sifa za kiutendaji, umoja wa uhalisi wote wa Kiti kitakatifu cha Vatican katika muktadha ya Tasinia ya mawasiliano, ili mfumo mzima ujibu kwa njia thabiti mahitaji ya utume wa uinjilishaji wa Kanisa", yanahitimishwa maelezo.