Maandalizi ya Siku ya Vijana itakayotanguliwa na mkutano kuhusu mazingira. Maandalizi ya Siku ya Vijana itakayotanguliwa na mkutano kuhusu mazingira. 

Katika WDY,Lisbon vijana wanajadili mitindo ya maisha endelevu

Mkutano wa nne wa kimataifa juu ya utunzaji wa uumbaji unaohamasishwa na Mfuko wa Yohane Paulo II kwa Vijana utafanyika tarehe 31 Julai katika mji mkuu wa Ureno. Miongoni mwa mada zilizoshughulikiwa,uchumi,familia, maliasili,siasa na teknolojia. Pia kuna nafasi za mikutano kwa njia ya mtandao.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Mada itakayoongoza mkutano wa IV wa Kimataifa la Utunzaji wa kazi ya Uumbaji litakalofanyika tarehe 31 Julai, katika  Chuo Kikuu cha Ureno, katika mkesha wa Siku ya Vijana Duniani ( WYD) huko  Lisbon 2023 inasema: “Vijana walio msatari wa mbele katika ikolokia: mitindo ya Maisha inayosaidia ubinadamu uliopayishwa.” Kwa mujibu wa taarifa ya waandaaji, iliyotolewa tarehe 14 Aprili 2023, wana nukuu kifungu cha waraka wa Papa Francisko juu ya utunzaji wa mazingira kwamba: “Mambo mengi yanapaswa kubadili mwelekeo, lakini ni sisi wanadamu juu ya yote tunaohitaji kubadilika. Hatuna ufahamu wa asili yetu ya pamoja, ya kumiliki kwetu sisi sote, na ya siku zijazo za kushirikiwa na kila mtu. Ufahamu huu wa kimsingi ungewezesha ukuzaji wa imani mpya, mitazamo na aina za maisha. Changamoto kubwa ya kitamaduni, kiroho na kielimu iko mbele yetu, na itatuhitaji tuanze njia ndefu ya kufanya upya.” (Laudato si’, 202).

Kwa hiyo kwa kufuata mada zilizotangulia za matoleo yenye mada: “vijana ni walinzi wa  Uumbaji wa Wakati ujao kwa kiwango cha binadamu tunachotafuta”(Rio de Janeiro 2013); Kwa ikolojia fungamani: Vijana kama mawakala wa mabadiliko” (Krakow, 2016); “Vijana kwa Makazi Yetu ya Pamoja: Uongofu wa Kiikolojia kwa Vitendo” (Panama, 2019) ndiyo njia iliyochukuliwa hadi sasa ya vijna wa Vijana wa Paulo II, katika muktadha wa Siku ya  XXXVIII  ya Vijana Duniani jijini Lisbon, Agosti 2023), wanaandaa  tena Kongamano la nne la Kimataifa la Utunzaji wa Uumbaji. Mada ni “Ahadi ya Vijana kwa ikolojia fungamani: Mitindo ya Maisha kwa Ubinadamu Mpya” na itafanyika Lisbon katika Chuo Kikuu katoliki cha Ureno tarehe 31 Julai.

Vijana wanapojitayarisha kiroho kwa ajili ya WYD 2023, wengi wao wameweka wazi kwamba wanachukulia ikolojia fungamani kuwa moja ya mada kuu ya papa wa sasa, na kwamba wanataka kujitolea kwao kibinafsi. Mkutano huo umeandaliwa kwa namna ambayo itawaleta vijana washiriki pamoja na wataalam ambao watatoa tafakari zao kuhusu maeneo matano ya maisha ya binadamu kuanzia na uchumi, elimu na maisha ya familia, maliasili, siasa na teknolojia. Uzuri na upya wa mkutano huo ni kwamba baadhi ya nafasi zake zitaona uzoefu wa mtandao kupitia matumizi ya teknolojia ya hali ya juu. Hii itaruhusu ushiriki katika mkutano kuwa jumuishi zaidi na upatikane. Njia iliyofuatwa katika miaka ya hivi karibuni na Taasisi ya Vijana ya Yohane Paul II inaendana na Upapa wa Papa Francisko.

Kwa hiyo wasiwasi huo unatokana na kile kinachotokea kwa nyumba yetu ya kawaida kuelekea ufahamu wa sababu za kibinadamu za mgogoro wa kiikolojia na kujitolea kwa hatua maalum inayoendelea kulenga kulinda kazi ya Uumbaji. Kwa mujibu wa Daniele Bruno rais wa Mfuko huko, amesisitiza kuwa lengo la ubadilishanaji huu wa mawazo ni kueleza kwa pamoja tafakari ya mitindo ya maisha ambayo tayari tumetumia, na pia kuzungumzia njia mpya tunazohitaji kutumia katika kuishi maisha yetu ili kujiandaa na changamoto za kiutamaduni, kiroho na kielimu zinazowasubiri vijana na vizazi vijavyo. Ubinadamu wetu mpya lazima usiitazame Dunia kama rasilimali ya kutumiwa vibaya bali kama zawadi kutoka kwa Mungu kwetu.” Washiriki watakuwa wajumbe vijana chuo kikuu kutoka mabaraza ya maaskofu, harakati la kimataifa na vyama na vyuo vikuu vya Kikatoliki watakaokwenda Lisbon kuhudhuria siku ya Vijana duniani (WYD).

Hitimisho la hati ya kazi

Kama ilivyokuwa katika mikutano iliyopita, itahitimisha kwa hati  yaani Ilani ya mwisho inayotokana na majadiliano ambayo yatatumika kama msingi wa hatua zaidi na kutafakari. Vyombo vifuatavyo vinashirikiana katika kuandaa mkutano huo: Baraza la Kipapa la Walei Familia na Maisha ambao ndio msingi usadizizi wa chombo hicho; Baraza la Kipapa la Kuhamasisha Maendeleo Fungamani ya Binadamu; WYD Lisbon 2023 Foundation; Chuo Kikuu Katoliki cha Ureno, ambacho ni mwenyeji wa tukio hilo; Chuo Kikuu cha Moyo Mtakatifu na Shule ya Juu kwa ajili ya Mazingira, Harakati ya Kimataifa la Laudato si; Mfuko wa Mfalme Albert II wa Monaco na Mfuko wa Magis; chini ya udhamini wa Mabalozi wa Ureno na Mfalme wa Monaco kwa Vatican.

15 April 2023, 16:24