Kard.Erdo:Asante Papa kuleta habari njema ya huruma na upole
Na Angella Rwezaula- Vatican.
Kardinali Peter Erdo Askofu Mkuu wa Esztergom-Budapest, mara baada ya misa, alitoa shukrani kwa Baba Mtakatifu Franciko kwa dhati kufika kwake katika ziara ya kitume. Kardinali Edro amesema kwamba wakati mwanzoni mwa huduma yake ya Upapa aliposema kwamba Kanisa lazima liwe na ujasiri wa kwenda pembezoni, alizungumza kutoka moyoni mwao. Kwa sababu hiyo, Baraza la Maaskofu wao walisema katika itifaki yao kwamba jumuiya ya Kikatoliki ya Hungaria, kama wengine wengi, waishi katika pembezoni. Danube inayovuka jiji lao ilikuwa kwa karne kadhaa mpaka wa Milki ya Roma. Baadaye Milki ya Wafranki pia ilipanua uvutano wake hadi Danube. Wao walikuwa eneo la kaskazini kabisa ndani ya Milki ya Ottoman, hapo katikati mwa Ulaya. Kwa hiyo, wameishi kwenye ukingo wa mashariki mwa Jumuiya ya Wakristo Magharibi kwa miaka elfu moja.
Kardinali Erdo alirudia kumshukuru Baba Mtakatifu ambaye alifika kwa; kwa watu wao wanaozungumza lugha ambayo watu wachache sana ulimwenguni wanazungumza.. Amefika kukutana na watu wao ambao kwa miaka elfu moja wameshikamana kwa upendo na Ukristo wa Magharibi, ambao badala yake, kama walivyohisi zaidi ya mara moja, wameusahau. Ameshukuru kuwatembelea maskini na wakimbizi ambao wamefika kwao kutoka nchi jirani ya Ukraine. Amemshukuru kutembelea watoto wagonjwa, vijana ambao wanamaanisha changamoto kuu na fursa kuu kwa Kanisa lao. Ameshukuru kwa kuwapelekea habari njema ya huruma na upole.
Kardinali Edro amesema Watu wanaoishi kando ya Danube wamejifunza kwamba mto mkubwa sio tu kikomo, lakini, ikiwa wanaweza kujenga madaraja kwa busara, ni wazi kwamba wanaweza kuunganisha watu wa Kaskazini na Kusini, Mashariki na Magharibi. Mfano huo ulitolewa na mfalme wao wa kwanza Mtakatifu Stefano, ambaye anaheshimiwa hadi leo hii na Makanisa ya Kikatoliki na Kiorthodox. Kwa hakika, Kardinali Erdo alisisitiza kuwa alitangaza Kristo katika enzi ambapo Makanisa ya Mashariki na Magharibi yalikuwa bado katika ushirika kamili. Kwa hiyo amezidi kumshukuru Baba Mtakatifu, Francisko kwa kuwapelekea ujumbe wa mazungumzo na amani ambao unafaa hasa siku ya hiyo. Mungu abariki hadhi yake na huduma yake tele! Na kwa kuhitimisha aliomba wapewe Baraka ya kitume.