Hollerich:Sinodi kwa ajili ya kuungana katika kuhudumia Mungu
Na Andrea Tornielli
Siku moja baada ya kutangazwa kwa muundo mpya wa Sinodi ya Maaskofu, Kadinali Jean-Claude Hollerich Mjesut, mwenye umri wa miaka 64, Askofu Mkuu wa Luxemburg na Mratibu mkuu wa Mkutano ujao wa Sinodi anaitathmini kazi hiyo katika mahojiano na vyombo vya habari vya Vatican.
Mkutano wa kawaida la Sinodi ya Maaskofu mnamo Oktoba 2023 utajumuisha idadi kubwa ya washiriki wenye haki ya kupiga kura ambao si maaskofu: mapadre, wanaume na wanawake watawa, walei wanaume na wanawake wenye asilimia 50 ya wanawake na mkazo maalum katika ushiriki wa vijana. Je, uamuzi huu una umuhimu gani?
Hili si jambo geni kabisa, kwa sababu huko nyuma kumekuwepo na wanachama wenye haki ya kupiga kura ambao hawakuwa maaskofu. Hakukuwa na wapiga kura wanawake, lakini wanachama wasio maaskofu. Kwa hiyo inaweza kusemwa kwamba kundi hilo dogo sasa linazidi kuwa kubwa. Sinodi inabaki kuwa ya maaskofu, kwa sababu askofu daima ni mchungaji wa Kanisa lake, mtu hawezi kuona kazi iliyotengwa na watu wake, na watu wake. Mimi ni askofu mkuu wa Luxemburg, ninapokuwa Roma ninakosa Kanisa langu: Ninawaza watu ninaowaona katika safu ya kwanza, safu ya pili, safu ya tatu katika kanisa kuu, ninawaza wale ninaokutana nao kila siku… na ninawakumbuka. Sehemu ndogo ya watu hawa watakuwepo kwenye Sinodi ili kuwa pamoja na wachungaji wao. Watakuwa na utume wa pekee, tayari wamepata uzoefu mkubwa wa masinodi katika majimbo, kisha katika ngazi ya Mabaraza ya Maaskofu na hatimaye katika ngazi ya Bara. Na sio maaskofu wote watakaoshiriki wamekwisha pata uzoefu huu. Hivyo kazi ya wajumbe hawa wapya ni kuwa mashuhuda wa yale waliyoyapitia ili kuyafikisha.
Pamoja na hayo, Je, Sinodi inabaki kuwa “ya maaskofu”?
Ndiyo, inabaki hivyo kwa sababu maaskofu ndio wengi! Ni juu la Maaskofu kutekeleza utambuzi, ambao umefanyika katika ngazi mbalimbali na hatimaye kumfikia Baba Mtakatifu. Sasa kuna hatua ya maaskofu, lakini kuna suala la utambuzi na jambo hili limetolewa kwa watu wa Mungu. Wajumbe wapya wa Sinodi wanawakilisha kwa namna ya kusema, sehemu isiyo maaskofu ya watu wa Mungu
Je, tunaweza kusema kwamba ni sinodi ya maaskofu inayoambatana na uwakilishi wa watu wa Mungu?
Lakini maaskofu pia ni wa watu wa Mungu! Angalau ningependa kuwa mshiriki wake… vinginevyo ningejisikia vibaya! Tunahitaji kuwaelewa zaidi kama mashuhuda na kumbukumbu ya mchakato wa sinodi iliyotekelezwa hadi sasa.
“Sinodi juu ya kisinodi” ni jina la kiufundi, ambalo linasikika mbali na maisha ya watu. Kwa wale ambao wamepata uzoefu huu, hata hivyo, ni kinyume kabisa. Je, unaweza kutuambia lengo la Sinodi hii ni nini?
Hii: kama sisi, pamoja, tunaweza kuwa Kanisa la kimisionari, leo na kesho. Tunawezaje kuwa Kanisa la sinodi na la kimisionari. Nadhani ni muhimu kusisitiza hili: sio uchambuzi au kutafakari, hapana! Tupo ili kuliishi Kanisa jinsi Mungu anavyotaka kwa nyakati zetu, kutangaza Injili kwa ulimwengu, kwa watu wa zama zetu. Na hiyo ni nzuri. Kanisa daima limekuwa sinodi. Mtakatifu Yohane Krisostom alisema kwamba Sinodi na Kanisa vinafanana… Safari tunayofanya, ushirikishwaji wa watu wote wa Mungu, inaonesha kwamba Roho Mtakatifu anatuongoza kwa namna ya kutekeleza kile ambacho Mtaguso Mkuu wa Pili wa Vatican na hasa Katiba “Lumen gentium” vilibainisha.
Kwa hivyo katikati ya mkutano mkuu ujao ni njia hiyo ya kuwa Kanisa, na sio mada ya mtu binafsi?
Ndiyo, na ninaamini hii pia ni jibu kwa ugonjwa wa wakati wetu. Kwa sababu kile kinachooneesha wakati wetu wa baada ya kisasa au wa dijitali, kama tunavyotaka kuiita, ni ubinafsi ambao unasisitizwa kila siku. Na tunaona kwamba kwa ubinafsi huu ubinadamu hauwezi kuendelea: tunahitaji vipengele vya jumuiya ili kuendelea. Halafu kuna hali ya kuongezeka kwa ubaguzi, katika jamii na kwenye vyombo vya habari, hata kwa wale wanaorejea Ukatoliki. Watu wa Mungu kutembea pamoja ni mwitikio kwa mienendo hii. Tahadhari: si kwamba ‘tulivumbua’ sinodi ili kuitikia mielekeo hii, bali ni Roho Mtakatifu ambaye katika kipindi hiki ameamsha tena hamu ya sinodi ambayo tayari jumuiya ya kwanza ya Kikristo ilipitia. Na ni njia ya kukabiliana na changamoto zinazotukabili, kwa sababu vinginevyo ubinadamu uko hatarini.
Papa mara nyingi anasisitiza umuhimu wa kusikiliza katika wakati ambapo kila mtu anazungumza na kila mtu anabishana, lakini ni wachache wanaosikiliza…
Kama askofu, ninaona kwamba ninaposikiliza wakati fulani mimi hubadilisha mawazo yangu, na hunisaidia vizuri. Jimbo langu ni kubwa, nchi yangu ina wakazi 660,000, lakini askofu ana msafara wa watu ambao wamezidi kufanya mafunzo yaleyale, wakati mwingine sehemu zile zile, na maprofesa wale wale, wanaofikiria sawa. Kuna ushahidi ambao hauonekani kwa kila mtu katika watu wa Mungu. Kwa maana hiyo ni vyema kuwa na uwazi huu, kujua jinsi ya kusikiliza. Na ni vyema watu nao wakaenda kuwasikiliza maaskofu, kwa sababu maaskofu hawana jukumu la kusikiliza tu bali pia lile la kutoa majibu na kuwa wachungaji wa watu. Hatuna bunge la sinodi, ambapo wengi huamua na kila mtu kufuata, sinodi si bunge. Tunataka kutambua mapenzi ya Mungu, turuhusu Roho Mtakatifu atuongoze.
Utaratibu huu unafanyikaje?
Ni mchakato wa kiroho na kwa sababu hii tuna mazungumzo haya ya kiroho, au tuseme mazungumzo haya katika Roho: ni njia ya kusikiliza na kuingia katika mazungumzo si kwa mtazamo wa upinzani, kufikia hitimisho la pamoja. Ni wazi kwamba daima kuna haja ya uongofu katika mchakato huu: wakati mwingine ni askofu ambaye lazima aongoke, wakati mwingine hata walei wanapaswa kuongoka.
Inatokea kwamba hata katika Kanisa tunakabiliana na mawazo ya kisiasa, ambayo tunataka ‘kutegemea’ kupata matokeo fulani. Ni nini hasa kinacholeta tofauti?
Ubunge fulani wa kikanisa ni zaidi ya sinodi ya ndugu zetu wa Kiprotestanti. Ni lazima tufanye sinodi ya Kikatoliki, ambayo ni tofauti. Tumeweka huduma, umoja wa maaskofu, wajibu kwa ajili ya Kanisa, ukuu wa Petro. Haya yote hayatatokomezwa na sinodi. Sinodi badala yake ni upeo ambao ushirikiano wa maaskofu na ukuu wa Papa unatekelezwa, ili kutafuta mapenzi ya Mungu pamoja.Kwa hiyo si suala la kusema: kuna tatizo hili, kuna nafasi hizi mbili, ambao ina ushindi wa wengi na ndivyo inavyoendelea. Kwa sababu hii inaharibu Kanisa, hatutaki. Kama jumuiya ya kikanisa lazima tutembee pamoja.
Je, “kutembea pamoja” maana yake ni nini?
Tunapotembea, Kristo ndiye kitovu. Kuna watu wa kulia, kushoto, kuna wale wanaotembea mbele, kuna wale ambao huchukua muda mrefu na kukaa nyuma: ni kawaida tunapotembea barabara pamoja. Lazima tujifunze kwamba mivutano fulani katika Kanisa ni ya kawaida, ina maana kwamba Kanisa liko karibu na watu, kwa sababu si kila mtu anafikiri kwa njia sawa katika mabara yote, juu ya matatizo yote. Kwa hiyo ni muhimu kusikiliza kwa heshima kubwa pia kwa tamaduni mbalimbali, kutafuta mapenzi ya Mungu, kuamua pamoja mwelekeo wa safari. Kwa kuwa kuna watu kadhaa ambao "wananipata" upande wa kushoto, tuseme ninatembea kushoto. Nikimchukua Kristo kama kitovu na kumtazama kutoka upande wa kushoto, simwoni tu, namwona Kristo pamoja na watu wakienda kulia. Siwezi kumwona Kristo bila kuwaona pia: ina maana kwamba hata wale wanaotembea kwenda kulia ni sehemu ya jumuiya yangu. Ina maana kwamba lazima tutembee pamoja. Natumaini kwamba uzoefu wangu kama huo utatokea kwa wale wanaokwenda kulia, kwa wale wanaoenda mbele, kwa wale wanaorudi nyuma ... Ikiwa Kristo ndiye kitovu na Roho Mtakatifu ndiye chombo na dhamana ya kwamba Bwana aliyekufa na kufufuka yuko katika kitovu na sisi sote ni wanafunzi wamisionari.
Wakati fulani, hata hivyo, inaonekana kwamba inashughulikia au inajali sana mambo mengine, miundo na mikakati.
Kanisa haliwezi kuwa na shughuli nyingi kila wakati likizungumza juu ya miundo yake yenyewe, shirika lake lenyewe. Huwezi kuona ni ajabu klabu ya soka ambapo wanazungumza tu kuhusu sheria bila kucheza mchezo? Hakutakuwa na watu wengi wa kujiunga na klabu hiyo na kuunga mkono timu yao! Ni vivyo hivyo hata kwa Kanisa: imani yetu inaishi kwa kutumikia, ndani ya Kanisa na nje ya Kanisa. Tunaishi katika huduma ya Mungu na katika huduma ya watu.
Kulikuwa na uzoefu gani na pia jambo jipya la hatua ya bara la Sinodi?
Ilikuwa nzuri sana, tuliona kile ambacho mikutano tofauti ya maaskofu ilipendekeza katika ngazi ya mabara tofauti. Pia tuliona tofauti: kwa mfano, katika hatua nyingi za bara kila mtu alipenda picha ya hema. Lakini barani Afrika si kwa sababu kwao hema ni hema ya wakimbizi, ni hema la taabu, ya umaskini, ambalo linaweza kuchanika na wanapendelea hema la familia ya Mungu ambalo, wakati familia inaweza kupanuliwa. Nilielewa wakati huo kwamba hatuwezi kuwasilisha picha moja, lakini picha nyingi zinazozungumza na tamaduni tofauti za kidini za watu wetu. Na nina hakika wale wanaopenda picha ya hema wanaweza kujifunza kitu kutoka katika mfano wa familia ya Mungu, na kinyume chake. Ilikuwa muhimu kushiriki katika mikutano ya bara, nilifanya sio kuzungumza, sio kushawishi, lakini kusikiliza, kutambua utofauti uliopo. Itabidi tufanye hivyo kwenye Sinodi ya Maaskofu.
Kutoka katik hati nane za mwisho, zile za mabara, lakini pia kutoka kwa ile ya Sinodi ya dijitiali ni nini kinachoibuka? Mada ya mtu binafsi au njia ya sinodi katika kuwa Kanisa?
“Sinodi ya kidijital” ilikuwa tukio la ajabu ... Kutoka katika nyaraka zote kunajitokeza uzoefu ambao umekuwa, furaha ya watu. Katika Ulaya, katika Asia, wameomba waweze kurudia makusanyiko hayo. Niliogopa Ulaya, kwa sababu tunajua kwamba kuna tofauti kubwa. Lakini hata hapa watu wanataka kuendelea na lazima tusonge mbele na tofauti zetu na tutembee pamoja. Ni lazima tuangalie kile ambacho ni muhimu kwa muungano, kwa ajili ya ushiriki, kwa ajili ya utume na kuwasilisha katika Sinodi ya Maaskofu mwezi Oktoba.
Mlifanyaje kazi ya kutoa nuru ya michango ya mabara tofauti?
Kama kikundi, kwa njia ya sinodi. Sio shughuli ya mtu mmoja. Kulikuwa na vikundi kadhaa vilivyofanya kazi katika mada mbalimbali: ukuu, huduma kwa waliowekwa wakfu, huduma za ubatizo, ushirikiano wa maaskofu. Tulijiuliza makusanyiko ya bara walisema nini juu ya hili na tukaiweka pamoja, tukiangalia yale ambayo Majisterio ya Kanisa, Mapapa, Mtaguso wa Pili wa Vatikano inasema, kujumuisha kila kitu kilichojitokeza katika safari ya pamoja.
Je, tutegemee nini kutoka katika Instrumentum laboris?
Itakuwa maandishi mafupi. Itatusaidia katika kushirikisha, katika ushiriki, ili washiriki wa Sinodi waweze kujieleza. Hakika ninatumaini washiriki nao wako huru kusema: tuyatupilie mbali, tufanye mengine, pia kwa sababu tuna Sinodi ya miaka miwili mbele yetu na hakuna haraka. Hatupaswi kuja kwenye maelewano ya bandia. Tuna muda wa kuelewa kweli wito wa Mungu kwa ajili ya Kanisa lake katika ulimwengu wa leo.
Kwa dhati ni kitu gani kitatokea kati ya sasa na Septemba?
Maandishi yatatumwa na kuwasilishwa kwa washiriki. Ninadhani bado tutakuwa na kazi nyingi, kwa sababu kuna mambo mengi mapya ya kuona hatua kwa hatua. Na haisemwi kwamba maamuzi yetu, ya mwandishi, katibu mkuu, katibu maalum, lazima yafuatwe, kwa sababu kila kitu kitawasilishwa kwa Baraza la Sinodi na kwa Papa. Hakuna sinodi bila maaskofu, wala dhidi ya maaskofu, na hakuna sinodi bila Petro au dhidi ya Petro. Kila kitu kinapendekezwa kwa Baba Mtakatifu kwa kibali chake, kwa baraka zake, vinginevyo hatuwezi kuendelea. Sisi ni Wakatoliki na tunataka kubaki Wakatoliki!
Umeshiriki katika mikutano ya mabara tofauti. Je, ulikumbana pia na majibu ‘vuguvugu’ au upinzani wowote?
Niliona majaribu mawili. La kwanza ni ile ya kufananisha kila kitu kwenye mifumo ya zamani. Ni kishawishi ambachoo kwa urahisi ninafafanua kama ‘walio sawa’, ambayo inasema: tunataka kufanya kile ambacho tumekuwa tukifanya kila wakati, hatutaki kuwa na wasiwasi juu ya kitu kipya. Lakini pia kuna majaribu ya “mlengo wa kushoto” ambayo kwayo masuala yote yanayoonekana kuwa muhimu katika Kanisa lazima yajadiliwe katika Sinodi. Lakini hii haiwezekani. Sinodi ina kichwa na cheo hiki ni kazi kwetu: sinodi,Umoja, ushiriki, utume. Sinodi itazingatia hili, sio mada nyingine zote. Itajadili umuhimu wa mada nyingine tutakazomletea Baba Mtakatifu ili aweze kuzitafakari kwa namna apendavyo. Lakini Sinodi itahusu sinodi.
Je, Sinodi inawezaje kumhoji mtu ambaye hatahusika moja kwa moja na hajapata fursa ya kuwa hivyo katika awamu ya maandalizi majimboni?
Kwanza ningeomba tuombe, kwa maana ili kuyafanya mapenzi ya Mungu unahitaji kusali sana. Ni lazima tupate usaidizi wa maombi ya Kanisa zima. Na kisha ningekuomba tujaribu kuishi Sinodi katika moyo binafsi, katika jumuiya ya kila mmoja, kazi au kikanisa kwa sababu kwa njia hii sala yao haitabaki kuwa ya kufikirika. Ninaota ushiriki mkubwa katika maombi ya Sinodi. Kadinali Mario Grech alisema jambo ambalo nimeliona kuwa zuri: tujaribu kuwa na mtindo wa Yesu. Unapoona Kanisa, ni lazima umtambue Yesu. Hili ni muhimu sana, vinginevyo tunawezaje kuinjilisha ikiwa watu hawatambui Yesu ndani yetu? Na kwa hili tunahitaji uongofu. Sinodi haiwezekani bila uongofu na ubadilishaji huu hutumikia kila mtu, kulia, kushoto na katikati.