Askofu Mkuu Gallagher:Ziarani 24-25 Aprili huko Liechtenstein
Na Angella Rwezaula, - Vatican.
Katibu wa Vatican wa Mahusiano na Mataifa na Mashirika ya Kimataifa ametembelea Liechtenstein tarehe 24-25 Aprili. Baada ya mikutano ya kitaasisi na waziri mkuu na waziri wa mambo ya nje wa nchini ndogo la Ulaya, tarehe 24 askofu mkuu amezungumza kwenye Mkutano unaoongzwa kauli mbiu "Diplomasia na Injili" katika ukumbi wa mji mkuu Vaduz wa nchi hiyo. Ratiba yake ilikuwa ni mchana kumtembelea kwa heshima Mrithi wa Mfalme Alois von und zu Liechtenstein. Tarehe 25 Aprili ataadhimisha Misa katika Kanisa kuu la Mtakatifu Florin.
Ziara ya siku mbili katika Nchi ndogo sana ya Liechtenstein ya Askofu Mkuu Paul Richard Gallagher, katibu wa Vatican wa Mahusiano na Mataifa na Mashirika ya Kimataifa. Ratiba yake ya ziara hiyo, iliyotangazwa na Sekretarieti ya Vatican kwenye tweet kwenye akaunti ya Terza Loggia, ambayo kwa hiyo ilianza mapaema tarehe 24 Aprili, na kukutana na Waziri Mkuu Daniel Risch na baadaye na Waziri wa Mambo ya Nje, Elimu na Michezo Dominique Hasler.
Askofu Mkuu Gallagher atazungumza katika mkutano kuhusu "Diplomasia na Injili", katika ukumbi wa mji wa Vaduz. Tukio rasmi la mwisho la siku litakuwa ziara ya heshima kwa Mfalme aliyeko kwenye maradakani Alois von und zu Liechtenstein. Tarehe 25 Aprili, Katibu wa Vatican anayehusika na Mahusiano na Mataifa na Mashirika ya Kimataifa ataongoza Ibada ya Ekaristi Takatifu itakayofanyika katika Kanisa kuu la Mtakatifu Florin mjini Vaduz, kabla ya kurejea tena mjini Vatican.
Tuijue Nchi hii ndogo
Kwa muda mrefu nchi ilikuwa sehemu ya Dola Takatifu la Kiroma ingawa chini ya utawala wa kikabaila. Dola hilo liliposambaratishwa na Napoleon Bonaparte (1806), Liechtenstein ilijiunga na Shirikisho la Rhein hadi mwaka 1813 ambapo lilifutwa, halafu na Shirikisho la Ujerumani (1815-1866). Ndipo ilipopata uhuru kamili ikitegemea ulinzi kutoka Uswiss.
Lichtenstein imekuwa nchi tajiri baada ya vita kuu ya pili ya dunia kwa sababu serikali ya mtemi ilidai kodi ndogo kabisa zilizohamasisha makampuni mengi ya nje kufungua ofisi zao nchini. Kwa upande wa Siasa Mkuu wa nchi ni mtemi Hans-Adam II anayeitwa kwa jina kamili Johannes, Hans “Adam II Ferdinand Alois Josef Maria Marko Aviano Pius von und zu Liechtenstein”. Tangu tarehe 15 Agosti 2004 amemkabidhi mwanawe Alois madaraka ya utawala.
Bunge la wabunge 25 huchaguliwa na wananchi wote. Sheria zote zinapaswa kukubaliwa na mtemi. Mawaziri watano wa serikali huteuliwa na bunge na kuthibitishwa na mtemi. Wananchi wote wana haki ya kupeleka mapendekezo ya sheria, au kudai kura ya wananchi wote juu ya sheria iliyopitishwa na bunge na kuthibitishwa na mtemi. Na kwa upande wa Lugha rasmi na ya kawaida ni Kijerumani. Wakati huo huo kwa upande wa dini, wakazi wengi ni Wakristo, hasa Wakatoliki (78.4%) na Wakalvini (7.9%).