Tafuta

Shule ya Ufundi na kazi (Scuola delle Arti e dei Mestieri.Fabbrica di San Pietro),Mfuko wa Fratelli Tutti. Shule ya Ufundi na kazi (Scuola delle Arti e dei Mestieri.Fabbrica di San Pietro),Mfuko wa Fratelli Tutti. 

19 Aprili ni uzinduzi wa Shule ya Sanaa na Ufundi ya Fabbrica di San Pietro

Siku hiyo itasimamiwa na Antonio Preziosi,mkurugenzi wa Rai Bunge na atatambulishwa na Kadinali Mauro Gambetti,rais wa ‘Fabbrica di San Pietro’ na wa Mfuko wa ‘Fratelli tutti’ kwa salamu kutoka kwa Waziri wa Utamaduni nchini Italia.

Na Angella Rwezaula;- Vatican.

Uzinduzi wa kitaaluma wa Shule ya Sanaa na Ufundi ya Fabbrica di San Pietro utafanyika Jumatano tarehe 19 Aprili 2023, saa 7 mchana, katika ukumbi wa Kanisa la Mtakatifu Petro, uliohamasishwa kwa ushirikiano na Mfuko wa  Fratelli tutti. Tarehe hiyo  itasimamiwa na Antonio Preziosi, mkurugenzi wa Rai Bunge, itatambulishwa na na Kadinali Mauro Gambetti, rais wa ‘Fabbrica di San Pietro’ na wa Mfuko wa  Fratelli tutti kwa salamu za kitaasisi kutoka kwa Waziri wa Utamaduni, nchini Italia Bwana Gennaro Sangiuliano.

Mafunzo hayo yamekabidhiwa kwa Mario Cucinella, mbunifu, Mhakiolojia na msomi, mwanzilishi wa MCA, ambaye atazungumza na wanafunzi wa Shule na wageni waliopo kuhusu mada ya “Mafundi wa kidigitali wa usanifu na muundo. Kufikiria kwa mikono yako.” “Kwa karne nyingi, mikono imechangia kukabidhi tamaduni na maarifa; imetoa uhai kwa mawazo, kwa kuyatafsiri kuwa umbo; imeunda mpya, imetunza urithi wetu wa kiutamaduni; imerudisha vitu vilivyoharibiwa na kuviruhusu kuishi baada ya muda;imeleta historia kwetu na itaongoza katika siku zijazo.” Kwa hiyo ni muhimu kwamba ziwepo shule zinazotunza maarifa kwa njia ya mikono, zinazowaongoza katika ujuzi wa nyenzo za kale na mpya, za mbinu mpya zinazounga mkono ujuzi wa ufundi; na kwamba elimu hii inaenea kwa wakati na anga ili kuwepo na mwendelezo kati ya wakati uliopita, uliopo na ujao”.

Tafakari iliyotolewa na mbunifu Cucinella juu ya kufikiria kwa mikono yako” kwa mujibu wa  Kardinali Gambettiamesema  inarudisha katikati mwelekeo muhimu wa elimu, ambayo inajua jinsi ya kuunganisha tena maarifa ya kubahatisha na ya vitendo:  kwa hiyo (Scuola delle Arti e dei Mestieri della Fabbrica di San Pietro) yaani “Shule ya Sanaa na Ufundi ya Fabbrica di San Pietro” inataka kuwapa wanafunzi mfano mzuri katika hili pia, kuweka mbinu na teknolojia katika mazungumzo na kuiunganisha, sanaa na masomo ya kinadharia”.

Katika uzinduzi huo pia utahudhuriwa na Dk. Assunta di Sante, ambaye amekabidhiwa jukumu la kisayansi la Shule, na Profesa Nicoletta Marconi wa (Chuo Kikuu cha Roma cha Tor Vergata), profesa na mshauri wa kisayansi. Tukio hilo litahitimishwa na Padre Francesco Occhetta, katibu mkuu wa Mfuko wa  ‘Fratelli tutti’ na mkurugenzi wa Shule ya Sanaa na Ufundi. Uzinduzi wa kitaaluma pia utatoa fursa ya kuonesha, mbele ya mwili wenye heshima na wanafunzi, masomo ya mzunguko unaofuata.

15 April 2023, 16:16