Kanisa la Mtakatifu Yohane Mbatizaji la Mërqij nchini  Albania Kanisa la Mtakatifu Yohane Mbatizaji la Mërqij nchini Albania 

Ziara ya Askofu Mkuu Gallagher nchini Albania

Safari ya Katibu wa Mahusiano na Mataifa na Mashirika ya Kimataifa inafanyika kuanzia tarehe 18 hadi 20 Machi 2023 kwa mwaliko wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Albania Bwana Olta Xhaçka na Askofu Angelo Massafra,Rais wa Baraza la Maaskofu wa Albania.

Vatican News

Kuanzia tarehe 18 Machi Katibu wa Mahusiano na Mataifa na Mashirika ya Kimataifa, wa Vatican Askofu Mkuu Paul Richard Gallagher, atakwenda nchini Albania. Hii ilitangazwa na Sekretarieti ya Vatican katika ukurusa wa tweet kwenye akaunti ya ‘Terza Loggia’. Safari hiyo inafanyika kwa mwaliko wa Waziri wa Mambo ya Nje Bwana Olta Xhaçka nchini Albania na rais wa Baraza la Maaskofu wa Albania, Askofu Angelo Massafra. Hata hivyo kumbukumbu ya ziara ya Papa Francisko mjini Tirana tarehe 21 Septemba 2014 bado ni hai nchini humo, na hata ziara ya kihistoria ya Mtakatifu Yohane Paulo II mnamo tarehe 25 Aprili 1993 haijasahaulika kabisa.

Kulingana na mpango wa ratiba ya ziara hiyo, Jumamosi  tarehe 18 Machi Askofu Mkuu  Gallagher atakuwa huko Tirana, ambapo atakutana na Waziri Olta Xhaçka, na kisha Scutari, ambapo ataadhimisha Misa katika Kanisa Kuu na kutembelea Jumba la Makumbusho la Mashahidi waliowekwa wakfu kwa wale walioteswa wakati wa utawala wa kikomunisti.  Siku ya Dominika  tarehe 19 Machi, ataadhimisha Misa katika Kanisa Kuu la Rreshen na atakutana na maaskofu wa Baraza la Maaskofu. Jumatatu 20 Machi, atakutana na viongozi wa kidini wa nchi hiyo huko Tirana, rais wa Bunge la Jamhuri, Lindita Nikolla,  na atatembelea Chuo Kikuu Katoliki cha Mama Yetu wa Shauri Jema, Kanisa Kuu katoliki, Kanisa Kuu la Kiorthodox na Msikiti huko mji mkuu wa Albania.

Nchini Albania, Vatican ilikuwa imeanzishwa uhusiano wa uwakilishi wake mnamo mwaka 1920, lakini kuanzia 1945, pamoja na ujio wa utawala wa Kikomunisti, uwakilishi ulibaki wazi, baada ya kufukuzwa kwamwakilishi wa Vatican, Monsinyo Leone Nigris, na kifo cha kutisha cha mrithi wake. Askofu Mwenyeheri Frano Gjini, aliyepigwa risasi mnamo mwaka 1948 kwa kukataa kutii amri iliyotolewa na kiongozi wa Albania Enver Hoxha ya kuunda Kanisa la kitaifa lililojitenga na Roma. Uhusiano wa kidiplomasia kati ya Vatican na Albania ulianzishwa tena  mnamo tarehe 7 Septemba 1991, baada ya kuanguka kwa udikteta wa kikomunisti.

17 March 2023, 16:04