Tafuta

2023.03.13 Kitabu cha Padre Enzo Fortunato kuhusu mchakato wa Mtakatifu Francis wa Assisi na katika mtazamo wa Upapa wa Francisko 2023.03.13 Kitabu cha Padre Enzo Fortunato kuhusu mchakato wa Mtakatifu Francis wa Assisi na katika mtazamo wa Upapa wa Francisko 

Usomaji wa Kifransiskani wa upapa wa Papa Francisko

Ushiriki mkubwa mjini Roma kwa ajili ya uwasilishaji wa ‘Mchakato wa Francis’ ambacho ni kitabu cha Padre Enzo Fortunato(OFMconv) kutokana na majaribu halisi ambayo Mtakatifu Francis wa Assisi na Papa walipaswa kukabiliana nayo katika maisha yao.Kwa mujibu wa mwandishi wa kitabu “Kilicho muhimu zaidi ni jibu la wote wawili:ukosefu wa uamuzi kwa wengine.

Na Angella Rwezaula; - Vatican.

Kimewakilishwa kitabu chenye kichwa “mchakato wa Francis”, cha Padre Enzo Fortunato (OFMconv) ambacho kinafuatilia mtazamo wa awali uliolenga mchakato ambao Mtakatifu Francis wa Assisi na Papa Francisko walipaswa kukabiliana nayo katika maisha yao. Kwa mujibu wa mwandishi akihojiwa na Telepace kando ya uwasilisho ulilofanyika Dominika 12 Machi alasiri jijini Roma katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Anastasia huko Palatino alisema: “Inafurahisha kwamba wote wawili wanajibu kwa ukimya, bila kuchochea mantiki ya uchokozi,

Dibaji ya Kadinali Zuppi

Hata hivyo katika dibaji, Kardinali Matteo Zuppi rais wa Baraza la Maaskofu Italia (CEI) pia alisisitiza juu ya mwitikio wa wahusika wakuu wawili kwamba: “Si suala la kukwepa makabiliano, bali kupindua mpango na mantiki ya shutuma” kungezidisha chuki. Mantiki ya moyo badala yake inafungua nafasi kwa njia nyingine ya kuelewa uhusiano wa kibinadamu

Mizizi ya Mtakatifu Francis

Kitabu hiki kinaanza kutoka katika michakato mitatu iliyoashiria wasifu wa Mtakatifu Francis wa Assisi. Ya kwanza na ya pili inajulikana sana na inatia wasiwasi, kwa upande mmoja, mgogoro na Baba yake Pietro di Bernardone ambao uliishia kwa kumvua mtoto wake kijana nguo, kwa upande mwingine, uhusiano tata ulioanza na Papa Innocent III ambao ulisababisha kupitishwa kwa kanuni. Hata hivyo, kati ya tatu, si kila mtu anaifahamu kwamba kanuni ya “XI” inashughulika na njia ambayo ilisababisha mtu maskini kujiuzulu kutoka katika uongozi wa utaratibu wake mwenyewe, kwa maelezo ya  Padre Enzo Fortunato, mwandishi wa kitabu hicho, akiingia katika kiini cha kufanana na Papa Francisko.

Michakato

Katika miaka hii kumi, Papa Francisko amelazimika kukabiliana na baadhi ya majaribu, ambayo mara nyingi yanaambatana na matangazo makubwa ya vyombo vya habari, ndani na nje ya Kanisa. “Vyombo vya habari na wakati mwingine michakato muhimu”, mwandishi ametoa maoni. Mwanzilishi wa jumuiya ya Mtakatfu Egidio Andrea Riccardi pia aliunga mkono maoni hayo kwamba: “Papa Francisko hakika ndiye papa aliyekosolewa zaidi katika historia”, alisema wakati wa uwasilishaji, akielezea shukrani yake kwa mtazamo “usio wa sherehe” unaofuata kiasi.

Maneno ya Kadinali Gambetti

Kwa upande wa Kardinali Mauro Gambetti, Mkuu wa Kanisa Kuu la Kipapa la mji wa  Vatican alikabidhiwa hitimisho ambapo anabainisha kwamba:“Pengine bado tunapaswa kuelewa unabii ambao Papa Francisko ameuleta katika historia” .

14 March 2023, 16:46