Tafuta

2023.03.27 Tiziano Onesti na Bi Mariella Enoc  wa Bambino Gesù. 2023.03.27 Tiziano Onesti na Bi Mariella Enoc wa Bambino Gesù. 

Tiziano Onesti rais mpya wa Bambino Gesu’

Kuanzia 2017 alikuwa sehemu ya Bodi ya Wakaguzi wa hospitali na uteuzi wake unafuatia kujiuzulu kwa Bi Mariella Enoc,aliyeteuliwa wakati huo huo kuwa mshauri wa miradi ya maendeleo ya hospitali hiyo.

Vatican News

Katibu wa Vatican, mwenye dhamana aliyopewa na Baba Mtakatifu, Papa Francisko amemteua Bwana Tiziano Onesti kuwa Rais wa  Hospitali ya Watoto ya Bambino Gesù kwa miaka 3 ijayo ambapo ataanza wajibu huo kuanzia tarehe Mosi Aprili 2023. Bwana Tiziano Onesti alizaliwa huko Rocca di Papa, Roma mnamo 1960. Ni profesa wa Kawaida wa Uchumi wa Makampuni katika Chuo Kikuu cha Mafunzo ya Roma Tre na ameshika majumu mbali mbali ya uendeshaji na utawala katika vituo vya masoko ya kijamii ikiwa ni pamoja na (Reli ya Taifa, Trenitalia, Eni, Telecom,Kundi la Waariri  la ’Espresso, Aeroporti di Puglia)  na makumpuni mengine yasiyo ya kibiashara.

Tangu 2017 Profesa Tiziano Onesti alikuwa mjumbe wa Bodi ya Wakaguzi wa Hesabu za Hospitali ya Bambino Gesu’ na kuteuliwa kwake kunafuatia baada ya kujiuzulu kwake Dk. Mariella Enoc mwanzoni mwa Februari mwaka huu mwenye umri wa miaka 79 ambaye alikuwa ameshikilia nafasi ya urais huo mnamo 2015. Na wakati huo Bi Mariella Enoc ameteuliwa kuwa Mshauri wa miradi ya maendeleo ya hospitali kwa wakati unaofaa. Mabadiliko hayo yanafanyika katika kipindi cha ukuaji mkubwa wa hospitali hiyo, huku juhudi nyingi zikiendelea, ikiwa ni pamoja na makao makuu mapya, mchakato wa kuweka kidijitali na uimarishaji wa muundo mpya wa shirika, kuendelea kuimarisha ujuzi wa usimamizi uliopo kwa wingi katika Hospitali.

27 March 2023, 17:32