Tafakari ya II ya Kwaresima 2023:Injili ni nguvu ya Mungu kwa wokovu
Na Angella Rwezaula - Vatican.
Kuanzia Evangelii Nuntiandi ya Mtakatifu Paulo VI hadi Evangelii gaudium ya Papa Francisko mada ya uinjilishaji imekuwa kitovu cha tahadhari ya Majisterio. Waraka mkubwa wa Mtakatifu Yohane Paulo II umechangia katika hilo, pamoja na kuanzishwa kwa Baraza la Kipapa la Uinjilishaji lililohamasishwa na Papa Mstaafu Benedikto XVI. Hangaiko hilohilo laweza kuonekana katika kichwa kilichopewa katiba kwa ajili ya mageuzi ya Curia Romana ya Praedicate Evangelii na katika Baraza la Kipapa la Uinjilishaji lililopewa kutoka baraza la kale la Propaganda Fide. Kusudi lile lile kwa sasa limetolewa katika Sinodi ya Kanisa. Ni kwa ajili hiyo ya kuinjilisha, ambayo Mhubiri Mkuu wa Nyumba ya Kipapa Kardinali Raniero Cantalamesaa, alipenda kujikita nayo katika tafakari yake ya Pili kwa Kwaresima, Ijumaa asubuhi tarehe 10 Machi 2023, katika Ukumbi wa Paulo VI, kwa uwepo wa Baba Mtakatifu Francisko.
Katika tafakari ya Pili ya kwaresima iliyoongozwa na Mada ya “Injili ni Nguvu ya Mungu kwa wokovu” kutoka Warumi 1:16, Kardinali Cantalamessa amesema kuwa ufafanuzi mfupi na kamili zaidi wa uinjilishaji ni ule unaoweza kusomwa katika Waraka wa Kwanza wa Petro, ambapo mitume wanafafanuliwa kama: “wale waliowahubiri ninyi Injili katika Roho Mtakatifu” (1 Pt 1:12). Hiyo ina mambo muhimu katika uinjilishaji, yaani yaliyomo ndani yake ya Injili na njia yake katika Roho Mtakatifu. Ili kujua maana ya neno “Injili,” njia salama zaidi ni kumuuliza mtume Paulo ambaye alitumia neno hilo la Kigiriki mara ya kwanza katika lugha ya Kikristo. Tunayo bahati ya kuwa na maelezo kupitia mkono wake ambayo yanaeleza anachomaanisha juu ya “Injili,” na ni Waraka kwa Warumi. Kichwa chake kinatangazwa kwa maneno haya: “Siionei haya Injili, kwa maana ni uweza wa Mungu uuletao wokovu, kwa kila aaminiye” (Warumi 1:16).
Kwa ajili ya mafanikio ya kila jitihada mpya katika uinjilishaji, ni muhimu kuweka wazi kiini muhimu cha tangazo la Kikristo, na hakuna mtu ambaye ameliangazia vizuri zaidi kuliko mtume katika sura tatu za kwanza za Barua kwa Warumi. Juu ya ufahamu na matumizi ya ujumbe wake kwa hali ya sasa inategemea, kardinali anao uhakika kwamba, kama watoto wa Mungu watazaliwa kutokana na jitihada zetu, au kama tutalazimika kurudia na Isaya kwamba: Tumekuwa na mimba, tumekuwa na utungu, tumekuwa kana kwamba tumezaa upepo; hatukufanya wokovu wo wote duniani, wala hawakuanguka wakaao duniani.(Is 26:18). Ujumbe wa Mtume katika sura hizo tatu za kwanza za Waraka wake unaweza kufupishwa katika mambo mawili: kwanza, ni hali gani ya ubinadamu mbele ya Mungu kufuatia dhambi; na pili, mtu anatokaje humo, yaani, anaokolewaje kwa imani na kufanywa kiumbe kipya. Hebu tumfuate Mtume katika hoja zake msingi.
Afadhali, tumfuate Roho anayesema kupitia kwake. Sasa tumeingia, tunamshukuru Mungu, awamu mpya ambayo tunajitahidi kuona tofauti, si lazima kuwa zisizokubaliana na kwa hiyo zipiganiwe, lakini, iwezekanavyo, kama utajiri wa kugawanywa. Katika hali hii mpya, himizo la kuwa na “uhusiano wa kibinafsi na Kristo” halina hatari yoyote. Kwa hakika, njia hii ya kuwaza imani inaonekana kwetu kuwa ndiyo pekee inayowezekana, ikizingatiwa kwamba imani haiwezi kuchukuliwa kuwa jambo la kawaida tena, na kwamba haichukuliwi kama watoto ndani ya familia au mazingira ya shule, lakini lazima iwe tunda la kibinafsi na uamuzi. Mafanikio ya utume hayawezi kupimwa tena kwa idadi ya imani umoja bali ni jinsi watu wengi wamepitia hadi kuwa Wakristo wa jina hadi Wakristo halisi, yaani, kusadikishwa na kutenda kazi katika jumuiya.
Kwa maelezao zaidi ni “mkutano huu wa kibinafsi” maarufu na Kristo unajumuisha nini hasa? Ni kama kukutana na mtu moja kwa moja, baada ya kumjua kwa miaka mingi tu kupitia picha. Mtu anaweza kujua vitabu kuhusu Yesu, mafundisho, uzushi kuhusu Yesu, na dhana kuhusu Yesu, lakini asimjue akiwa hai na sasa. Kwa hiyo kuna vivumishi viwili: Yesu aliye hai na Yesu wa sasa!). Kwa waòo wengi, hata waamini waliobatizwa, Yesu ni tabia ya kizamani, utu, si mtu aliye hai. Inasaidia kuelewa tofauti kuangalia kile kinachotokea katika nyanja ya kibinadamu wakati unataka kumjua mtu hadi kumpenda. Mtu anaweza kujua kila kitu kuhusu mwanamke au mwanamume: jina lao, wana umri gani, wamefanya masomo gani, ni wa familia gani... Kisha siku moja cheche huwashwa na mtu akampenda mwanamke huyo. Kila kitu hubadilika. Wanataka kuwa na mtu huyo, kuwa naye kwa ajili yao wenyewe, wakiogopa kutompendeza au kutostahili kwake.
Je, tunaweza kufanya nini ili kuruhusu cheche hii kwa mtu wa Yesu iwashwe katika mioyo ya wengi? Haitawashwa kwa yeyote anayesikiliza ujumbe wa Injili isipokuwa unawaka angalau kama hamu na kama azimio kwa yeyote anayeutangaza. Kumekuwa na kuna tofauti; neno la Mungu lina nguvu zake lenyewe na linaweza kutenda, nyakati fulani, hata likitamkwa na wale ambao hawaishi kulingana nalo; lakini huo ndio ubaguzi. Kwa ajili ya kuwafariji na kuwatia moyo wale wanaofanya kazi kitaasisi katika fani ya uinjilishaji, Kardinali Cantalamessa amewambia kwamba si kila kitu kinawategemea wao. Inategemea wao kuunda mazingira ya kuwaka na kuenea kwa cheche hiyo ambayo hufanyika kwa njia na wakati usiotarajiwa. Katika matukio mengi ambayo nimeyajua maishani mwangu, ugunduzi wa kubadilisha maisha wa Kristo uliletwa kwa kukutana na mtu ambaye tayari amepata neema hiyo, kwa kushiriki katika kusanyiko, kwa kusikia ushuhuda, kwa kuwa na uzoefu wa uwepo wa Mungu ndani yake, wakati wa mateso makubwa, na hawezi kunyamaza juu yake, kwa sababu ilifanyika vile vile kwake kwa kupokea kile kinachoitwa ubatizo wa Roho. Kwa hiyo hapo kunaonekana haja ya kuzidi kuwategemea walei, wanaume na wanawake, kwa ajili ya uinjilishaji. Wao huingizwa zaidi katika kiungo cha maisha ambacho hali hizo hutokea kwa kawaida.
Pia kwa sababu ya uchache wa idadi yake, ni rahisi kwa mapadre kuwa wachungaji kuliko wavuvi wa roho: ni rahisi zaidi kuwachunga wale wanaokuja Kanisani na neno na sakramenti, kuliko "kuwatupa kwenye kilindi cha maji" (Lk. 5:4) kuvua samaki kwa wale walio mbali. Walei wanaweza kujikita kwa ajili ya wachungaji kazi ya wavuvi. Wengi wao wamegundua maana ya kumjua Yesu aliye hai na wana shauku ya kushiriki uvumbuzi wao na wengine. Harakati za kikanisa zilizoibuka baada ya Mtaguso zilikuwa kwa wengi mahali walipofanya ugunduzi huo. Katika mahubiri yake kwa ajili ya Misa ya Krisma ya Alhamisi Kuu mnamo 2012, katika mwisho wa upapa wake, Benedikto wa kumi na sita alisema: “Yeyote anayezingatia historia ya zama za baada ya maridhiano anaweza kutambua mchakato wa upyashaji wa kweli, ambao mara nyingi ulichukua sura zisizotarajiwa katika harakati za maisha na kufanya karibu kushikika uhai usioisha wa Kanisa takatifu, uwepo na ufanisi wa Roho Mtakatifu.”
Kando na matunda mazuri, baadhi ya harakati hizi pia zimetoa matunda yaliyooza. Tunapaswa kukumbuka usemi huu: “Usimtupe mtoto nje na maji ya kuoga.” Kwa kuhitimisha kwa maneno ya Ratiba ya Akili kwa Mungu ya Mtakatifu Bonaventure kwa sababu yanapendekeza wapi pa kuanzia ili kutambua, au kufanya kwa upya, “mkutano wetu wa kibinafsi na Kristo” na kuwa watangazaji wake kwa ujasiri: Hekima hii ya siri zaidi ya fumbo hapana mtu anajua isipokuwa yule anayeipokea; hakuna anayeipokea isipokuwa anaye itamani; hakuna anayetamani isipokuwa wale ambao wamechomwa ndani na Roho Mtakatifu aliyetumwa na Kristo duniani”.