Tafuta

Mkutano wa Kibara wa Sinodi Barani Asia huko Bangkok Februari 2023 Mkutano wa Kibara wa Sinodi Barani Asia huko Bangkok Februari 2023 

Sr. Hirota:Ushiriki wa wanawake katika Sinodi ni muhimu!

Sr.Hirota aliyeitwa kuwa sehemu ya Tume ya maandalizi ya mkutano mkuu wa kawaida wa Maaskofu utakaofanyika mjini Vatican,Oktobaa anafanya kazi nchini Japan.Kazi ya tume ni kuandaa Instrumentum laboris ambayo Wachungaji wa Kanisa la Ulimwengu watajadili.Katika mahojiano ametafakari kazi nao kwamba kuna njia,ukweli na uzoefu tofauti kama wa wanawake.

Na Angella Rwezaula; - Vatican.

Tume iliyoundwa tarehe 15 Machi 2023  itatayarisha waraka ambao utakabidhiwa kwa maaskofu kwa ajili ya mkutano wao mkuu wa kawaida wa Sinodi. Na itakuwa hasa hati hii, Instrumentum laboris, msingi ambao utambuzi wa maaskofu utaanza ambao, kwa uamuzi wa Baba Mtakatifu Francisko, utafanyika katika hatua mbili ya Sinodi hii, ya kwanza ni Oktoba ijayo, na ya pili mnmo Oktoba 2024, baada ya mchakato mrefu ulionaza mnamo 2021. Kauli mbiu inayoongoza mchakato wa safari ya Sinodi ni: “Kwa ajili ya Kanisa la Sinodi: Ushirika, Ushiriki na Utume, ambayo Makanisa mahalia, majimbo na parokia, vyama, jumuiya na watu binafsi walijihoji kwanza, na baadaye Makanisa ya bara moja baada ya jingine kwa kutoa maisha kwa makanisa ya Ulaya, Afrika, Kaskazini na Kusini mwa Amerika, Asia, Australia na visiwa vyake vyote na Mashariki ya Kati.

Ilikuwa ni kusikiliza kila mtu na kwamba hakuna anayehisi kutengwa, ambayo yamekuwa ni maneno ya kuzingatia ya mikutano mingi ambayo ilifanyika katika ngazi zote katika awamu hizo mbili. Na wakati wa kusikiliza, mkusanyiko wa sauti na muhtasari wake uliiandaliwa na baadaye kutumwa kwa Sekretarieti Kuu ya Sinodi, ya kile kilichojitokeza polepole kutoka katika mtazamo wa uongofu wa Kanisa kwa mtindo unaoshauriwa wa sinodi, ambamo wabatizwa, Wachungaji, na watu wa kipekee wa Mungu, wako njiani na kutoka nje kuelekea ulimwengu wote. Wajumbe saba wa Tume ya matayarisho ya Baraza la Maaskofu ambao kazi hiyo sasa inapitia chini ya urais wa Kardinali Mario Grech, ambaye ni katibu mkuu wa Sinodi. Miongoni mwao kuna mtawa wa Kijapani, Sr. Shizue Filomena Hirota, wa Shirika la Wamishonari wa Mercedarian wa Berriz huko Tokyo. Katika huduma yake alihudumu nchini Nicaragua, Mexico, Ufilipino na Roma na alishirikiana na Pax Christi. Kwa sasa ni mshauri wa Baraza la Kikatoliki la Haki na Amani la Baraza la Maaskofu Katoliki nchini Japan na ni mjumbe wa bodi ya Jumba la Makumbusho la Wanawake hai wa Vita na Amani. Mnamo Oktoba 2022, Sista Hirota aliratibu Mkutano Mkuu wa Mabaraza ya Maaskofu wa Asia (FABC) kabla ya Mkutano wa Bara, lakini ulioandaliwa kwa mtindo wa Sinodi.

Sr. Hirota kwa hiyo ndiye mwanamke pekee ambaye amechaguliwa kuwa sehemu ya Tume na katika mahojiano na Vatican News mwandishi hakuweza  kupuuza kipengele hiki maalum na tafakari ya swali la wanawake katika Kanisa kwamba kama Mtawa na katika mchakato wa Sinodi walizungumza kuhusu wanawake watawa wakati wa mchakato wa sinodi wakitilia mkazo hitaji la kuthamini zaidi jukumu na mchango wao, kama ule wa wanawake kwa ujumla.  Vile vile iliibuka ni kiasi gani wanawake watawa  tayari wanafanya kazi, kwa mfano, katika uwanja wa kazi za kijamii.

Katika hilo maoni yako ni yapi kwa kile ambacho kimesemwa hadi sasa kuhusu uwepo wa wanawake katika Kanisa?Kwa upande wake Sr Hirota amejibu kwamba “Sikushiriki katika awamu zilizopita za Sinodi, lakini nilikuwepo kwenye Mkutano Mkuu wa FABC, ulioleta pamoja Mabaraza ya Maaskofu wa Japan na uliandaliwa kwa mtindo wa  sinodi nyingi, lakini haukuwa hatua ya Sinodi. Nilikuwa pale nikiwakilisha Talitha Kum Asia, ambayo inafanya kazi pamoja na waathirika wa Biashara haramu ya  binadamu. Na lazima niseme kwamba ilikuwa chanya sana kuwepo hapo, kwa sababu dhamira ya Talitha Kum ilimulikwa  na shukrani kwa uwepo wetu suala la usafirishaji haramu wa binadamu uliwakilishwa vema. Lakini zaidi ya hayo, nadhani kulikuwa na wanawake wachache sana walioonekana katika mkutano mkuu ule na kulikuwa na filamu iliyoonesha ambapo kulikuwa na ushuhuda kutoka kwa msichana wa miaka 14 pekee na alikuwepo na kuzungumza. Na maaskofu walivutiwa sana. Lakini tukiangalia historia ya Mabaraza ya Maaskofu wa Asia, tayari mnamo mwaka 1986, wakati wa mkutano mkuu, kulikuwa na aina ya warsha kuhusu wanawake. Na siku zote nakumbuka kwamba kulikuwa na mtaalimungu wa Kihindi aitwaye Stella Faria, ambaye mara kwa mara alirudia kusema: “Mwanamke ni mtu wa kibinadamu. Mwanamke ni mtu wa kibinadamu.  

Kwa sababu gani kuna hali nyingi katika Asia na pia mahali pengine, ambapo wanawake hawatendewi kama binadamu? Na ilikuwa muhimu kwa sababu maaskofu walivutiwa sana na msisitizo wake kwamba mwisho, katika hati ya mwisho, kuna sentensi inayosema kwamba mwanamke ni mwanadamu. Kwa hiyo watu ambao hawakuwapo wakajiuliza: Je, Maaskofu wanatambua kwamba wanawake ni wanadamu tu sasa hivi? Zaidi ya  yote, tunajua jinsi hali ilivyo ngumu kwa wanawake kwa ujumla. Pamoja na Talitha Kum tunafanya kazi na wanawake wote ambao ni waathirika wa biashara haramu ya binadamu. Kisha kuna baadhi ya makutaniko ambayo yana shule za elimu ya wanawake. Tuna kila aina ya mipango ya ukombozi kutoka katika utumwa wao. Hili limekuwa kwa muda mrefu wasi wasi mkubwa wa Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu Asia  FABC. Zaidi ya hayo, katika Asia, Kanisa Katoliki ni walio wachache tu. Kwa hiyo, tunafanya kazi na kila mtu na pia tunafanya kazi na wanawake wa dini mbalimbali, kwa sababu moja ya mambo ambayo tumeelewa ni kwamba wengi wa waanzilishi wa taasisi za kidini walikuwa kwa ajili ya ukombozi wa wanawake, lakini kiukweli kwamba wanaume walichukua uongozi, Kanisa kama taasisi haijajitolea kila wakati kwa uwazi sana katika ubinadamu wa wanawake, kwa hivyo ni vizuri kufanya kazi na wanawake.

Papa Francisko alithibitisha mara kwa mara kuwepo kwa mtazamo tofauti wa wanawake ikilinganishwa na wa kiume. Wewe ndiye mwanamke pekee kuwa sehemu ya Tume, je, unahisije  wajibu na fursa hii ya kutoa macho ya kike kwenye Kanisa na juu ya ukweli kupitia nafsi yako? Wakati Kardinali Hollerich, mraribu  mkuu wa Sinodi, aliponiuliza kama nilikuwa tayari kushiriki na Tume, nilifikiri kungekuwa na watu wengi na hivyo nikasema ndiyo. Lakini basi tulikuwa na mkutano wa kwanza kupitia Mtandanoni ba ndipo niligundua, kwa mshangao, kwamba nilikuwa mwanamke pekee kati ya makadinali, maaskofu na mapadre. Nilijiuliza kwanini na bado ninajiuliza, lakini sote tunatambua kuwa ni muhimu sana kumekuwa na ushirikishwaji mzuri wa wanawake katika mchakato wa sinodi, kile tunachofanya hapa kwenye Sekretarieti Kuu ya Sinodi ni sehemu yake, na mengineyo yametengwa kwa ajili ya maaskofu. Lakini kuna wanawake, wanaume, watu wasiowekwa wakfu kwenye mchakato wa Sinodi na utume wa maaskofu haufanywi kwa nafasi binafsi, askofu yuko hapa akiwawakilisha watu wa Mungu. Basi nilijisemea moyoni: “Sawa, niko ninafanya kazi nao na ninawakumbusha kuwa kuna njia tofauti, ukweli tofauti, na uzoefu tofauti."

Je, ni mtazamo gani wa ndani unapendekeza kutekeleza kazi yako ndani ya Tume katika maandalizi ya Mkutano wa Maaskofu? Kiukweli, bado tuku katika siku za mwanzo na ni mapema kutathimini kazi. Siku hizi tumezungumza mengi kuhusu maana ya imani na ushiriki wa wanawake na mengine. Nafikiri jukumu langu hasa ni la kufanya kazi na pia ninadhani ni muhimu kuwa na uzoefu wa sinodi miongoni mwetu kama kikundi, kwa sababu moja ya sifa za Sinodi hii inapaswa kuwa hasa ile ya kuwa na uzoefu wa jumuiya, wa kuhisi wafuasi wote wa Yesu na kupata uzoefu wa Roho. Kwa hivyo, nadhani tunahitaji kuwa na uzoefu wa jumuiya ya Mungu hapa na kuwa na aina hiyo ya uzoefu wa jumuiya, tunahitaji kujiandaa. Katika hilo linahitaji mafungo yetu ya kiroho ya siku tatu. Kwa mchakato wa sinodi kuna mazungumzo ya kufanya mazoezi ya mazungumzo ya kiroho" yaani, kusikilizana kwa kina,na lazima kitu kitokee. Tunajua kuna mambo yenye utata, lakini jambo zuri ni kwamba hatuogopi kuongelea mambo yenye utata, maana mpaka sasa katika hatua nyingine, ningezungumzia suala la kuwekwa wakfu kwa wanawake, kwa mfano, yote yangekwisha, lakini sasa tunaweza kusema kwa uhuru. Na kisha kuna suala zima la LGBTQ ambalo sio rahisi, sio rahisi.

Na hii sio Sinodi ya watu wa LGBTQ na sio hata Sinodi ya kuwekwa wakfu kwa wanawake, hata kama mada hii pia itaibuka. Jambo la muhimu ni aina ya mtazamo tutakaokuwa nao katika kushughulikia masuala haya magumu sana, ambayo Kanisa, kwa namna fulani, halijawahi kukabiliana nayo. Hivyo hii ni changamoto. Na hiyo inaweza kuwa ndiyo maana Papa aliamua kufanya vikao viwili vya Mkutano Kuu la Maaskofu kwa mwaka 2023 na 2024. Ninahisi kwamba tunapaswa kujiandaa, kama kikundi, na makadinali na maaskofu wanajua vizuri zaidi kuliko mtu yeyote,  ni aina gani ya ugumu au makabiliano yanayofanyika katika sehemu fulani za ulimwengu na za Kanisa. Kwa hivyo ninadhani ni changamoto na tutaona kitakachotokea. Bado hatujamaliza. Tutafanya kazi kuandaa Instrumentem laboris, yaani kitendea Kasi ambacho sisi sote tutakuwa hapa Roma katikati ya mwezi Aprili, kwa hivyo tutaona na ninahisi kama kusema: njoo Roho Mtakatifu! Alihitimisha mahojiano hayo.

29 March 2023, 16:07