Tafuta

Sekretarieti kuu ya Sinodi ya Maaskofu imeteuwa wajumbe wa Tume ya Maandalizi ya Maadhimisho ya Sinodi ya XVI ya Maaskofu. Sekretarieti kuu ya Sinodi ya Maaskofu imeteuwa wajumbe wa Tume ya Maandalizi ya Maadhimisho ya Sinodi ya XVI ya Maaskofu.  (Vatican Media)

Sinodi ya VXI ya Maaskofu: Wajumbe wa Tume ya Maandalizi ya Sinodi ya Maaskofu

Wajumbe walioteuliwa kwenye Tume ya Maandalizi ya Maadhimisho ya Sinodi ya XVI ya Maakofu ni kama ifuatavyo: Padre Giacomo Costa, SJ., Mratibu wa Tume, Askofu Timothy John Costelloe, SDB; Askofu Daniel E. Flores; Sr. Shizue Hirota, MMB; Askofu Lucio A. Muandula; Prof. Dario Vitali; pamoja na Padre Tomasz Trafny, Katibu wa Tume. Tume itafanya kazi chini ya uongozi wa Kardinali Mario Grech, Katibu mkuu wa Sinodi za Maaskofu: Umoja, Ushiriki na Utume!

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Maadhimisho ya Sinodi ya XVI ya Maaskofu yananogeshwa na kauli mbiu “Kwa Ajili ya Kanisa la Kisinodi: Umoja, Ushiriki na Utume.” Maadhimisho haya yamegawanyika katika awamu kuu tatu kuanzia Mwezi Oktoba 2021 hadi Oktoba 2024. Awamu ya kwanza ilikuwa ni kwa ajili ya Makanisa mahalia pamoja na taasisi zote zinazoendeshwa na kusimamiwa na Kanisa Katoliki nayo yalianza tarehe 10 Mwezi Oktoba 2021 hadi 15 Agosti 2022. Maadhimisho ya Awamu ya Pili ya Sinodi ni kuanzia Mwezi Septemba 2022 hadi Machi 2023 na hapa kutakuwa na Ujumbe na vipaumbele vya watu wa Mungu, vitakavyotumika kutengeneza: “Hati ya Kutendea Kazi; Instrumentum laboris.” Awamu ya Tatu ya Maadhimisho ya Sinodi katika ngazi ya Kanisa la Kiulimwengu ni kuanzia mwezi Oktoba 2023. Kardinali Mario Grech, Katibu mkuu wa Sinodi za Maaskofu kwa mamlaka aliyokabidhiwa na Mama Kanisa amewateuwa wajumbe wa Tume ya Maandalizi ya Maadhimisho ya Sinodi ya XVI ya Maaskofu itakayokuwa chini ya uongozi wake.

Wajumbe wa Tume ya Maandalizi ya Maadhimisho ya Sinodi XVI Wameteuliwa
Wajumbe wa Tume ya Maandalizi ya Maadhimisho ya Sinodi XVI Wameteuliwa

Wajumbe walioteuliwa ni kama ifuatavyo:

Padre Giacomo Costa, SJ., Mratibu wa Tume

Askofu Timothy John Costelloe, SDB;

Askofu Daniel E. Flores;

Sr. Shizue Hirota, MMB;

Askofu Lucio A. Muandula;

Prof. Dario Vitali; pamoja na

Padre Tomasz Trafny, Katibu wa Tume.

Na Kardinali Jean-Claude Hollerich, SJ, Mwezeshaji wa Sinodi ya XVI ya Maaskofu, atashiriki kikamilifu katika maandalizi haya, kama sehemu ya utume wake.

Tume ya Sinodi ya XVI ya Maaskofu
15 March 2023, 14:21