Ni muhimu kuanza tafakari kitaalimungu na kisheria juu ya kujiuzulu kwa Papa kutoka katika huduma ya Petro,aliandika Mons Pennis. Ni muhimu kuanza tafakari kitaalimungu na kisheria juu ya kujiuzulu kwa Papa kutoka katika huduma ya Petro,aliandika Mons Pennis.  (ANSA)

Kitabu kuhusu Ratzinger:"Papa alishuka kutoka kiti cha enzi"

Mtaalam wa Vatican Giacomo Galeazzi katika kitabu kilichochapishwa na Rubbettino,kuhusu historia,ushuhuda,anafuatilia maisha ya Papa Benedikto XVI.Tangu mafunzo yake,mang’amuzi ya Mtaguso,hadi upapa na miaka kama Papa Mstaafu.Mons.Pennisi:“Ni muhimu kutafakari kitaalimungu na kisheria kuhusu kujiuzulu kwa Papa katika huduma ya Petro.

Na Angella Rwezaula; - Vati[ Audio Embed Kitabu kuhusu Papa Benedikto XVI:mafunzo, upapa na baadaye]can.

Miaka kumi sasa imetokea tangu alipoonekana hadharani mara ya mwisho Papa Benedikto XVI kama Papa wa Kanisa la Ulimwengu. Ilikuwa mnamo tarehe 28 Februari 2013, ambapo Papa Mstaafu Benedikto XVI aliposalimia ulimwengu uliokuwa unatazama jengo la Castel Gandolfo katika hotuba yake fupi bila kusoma ambapo alisema: “Ninyi mnajua kwamba siku yangu hii ni tofauti na siku zilizopita; Mimi si Papa tena Mkuu wa Kanisa Katoliki, kufikia saa mbili za usiku nitakuwa bado, na kisha basi sivyo tena. Mimi ni mhujaji tu anayeanza hatua ya mwisho ya hija yake katika ardhi hii”. Uwanja ulikuwa umejaa waamini na pia katika mitaa ya jirani. Watu walipiga kelele “Asante” na mabango, yakitikiswa pamoja na bendera na mabango, yalisomeka: “Usiende mbali”. Mara baada ya hapo, milango ya ilifungwa na Walinzi wa Uswiss. Kujiuzulu katika Upapa, kuliwasilishwa mnamo tarehe 11 Februari, na kuanza kutekelezwa Makao ya Kitume kuwa wazi, kwa mara ya kwanza katika karne nyingi, si kwa sababu ya kifo cha Papa.

Kifuniko cha kitabu cha Giacomo Galeazzi
Kifuniko cha kitabu cha Giacomo Galeazzi
Siku ya kuondoka Castel Gandolfo kurudi Roma
Siku ya kuondoka Castel Gandolfo kurudi Roma
Siku ya kuchaguliwa kwake 2005
Siku ya kuchaguliwa kwake 2005

Ili kuelewa haya yote, sasa ikiwa ni miezi miwili tangu kifo cha mtu ambaye alikuwa Papa mstaafu kwa miaka kumi, Giacomo Galeazzi katika kitabu chake anakusanya tena taarifa za historia ya kibinafsi ya Joseph Ratzinger yaani Papa Benedikto XVI, akitumia vyanzo vya kihistoria na uandishi wa habari, lakini pia historia na matukio madogo yaliyoashiria maisha yake, mafunzo yake, na miaka minane ya upapa wake. Kwa hivyo katika kurasa 188 za kitabu hicho inawezekana, kwa mfano, kupata miongoni mwa wengine jina la rais wa zamani wa Jamhuri ya Italia, Francesco Cossiga, ambaye mara nyingi alinukuu mazungumzo yake na Benedikto XVI, ambaye ilihusishwa mapendo ya fasihi na pia shauku keki. Siku ya Dominika mkuu wa zamani wa nchi ya Italia alikuwa anamtumia keki mjini Vatican.

Kijana na Mtaguso
Mbinu ya kusimulia historia ni ile ya kurudi nyuma. Tunaanza kutoka sasa yaani, kutoka katika mazishi ya tarehe 5 Januari 2023 na jeneza la kiasi na muhimu katika Uwanja wa Mtakatifu Petro ili kurudi nyuma ya kijana na upinzani wa kiakili dhidi ya unazi, masomo ya kitaaluma na, zaidi ya yote, uzoefu wa mtaalam wa usawa. Kwa Mtaalimungu kijana aliyeishi Roma katika Hoteli ya Zanardelli, ambapo alijifunza lugha ya Kiitaliano ya Mtaguso wa Pili wa Vatican ilikuwa ishara halisi ya hatima, ya Mungu, kwa mujibu wa mwandishi.
Aliishi vipindi vinne vya tukio hilo kuu lililozama katika mdundo wa kusisimua wa mipango, vikao vya kazi, kutafakari na kuandika nyaraka kwa mawasiliano ya karibu na maaskofu wakuu na wataalimungu wa karne ya 20, kutoka kwa Congar hadi Rahner, Volk, De Lubac hadi Danièlou”, jambo ambalo lilienea katika mawazo yake.

Uchaguzi wa Papa 2005
Tukio lingine la kihistoria ambalo kitabu hiki kinaleta uhai tena ni kuhusu Mkutano wa uchaguzi wa Upapa 2005 ambao ulimchagua Mrithi wa 264 wa Petro. Haikuwa mshangao kwa mtu yeyote, anaandika Galeazzi, akikumbuka uhusiano wa karibu na mtangulizi wake Yohane Paulo II, ambaye mnamo tarehe 16 Aprili 2002 alikataa kujiuzulu baada ya ushauri kutoka kwa Mkuu wa Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa ambaye alikuwa ametimiza miaka 75. Wakati ule Karol Wojtyla, alikuwa tayari amechoka sana kutokana na ugonjwa, japokuwa hakuwa na nia ya kuacha kuwa mshiriki mwenye mamlaka katika serikali kuu ya Kanisa.

Mawazo juu ya fedha na kanuni zisizoweza kujadiliwa
Imani ya ngano, uaskofu kama ubaba, mizizi na urithi wa Papa wa kiakili, aliyekua katika wazo juu ya Mtakatifu Augustino, Mtakatifu Bonaventure na Origen, ni mada zingine zilizochunguzwa katika kitabu hixho, pamoja na uchambuzi wa kuvutia juu ya hali ya sasa ya taalimunu ya Joseph Ratzinger, Mtaalimungu ambaye si mbunifu lakini ambaye amerejesha usasa kwenye mapokeo, anathibitshwa Galeazzi katika kitabu hicho. Mwandishi wa habari pia anafuta uwanja wa kutokuelewana kuhusu mapambano ya kibiolojia yaliyofanywa na Benedikto XVI, akifafanua uundaji ambao umeweka alama ya upapa mzima, hasa kwa ile ya kanuni zisizoweza kujadiliwa kuhusu bioethics (ulinzi wa maisha, wa familia, wa elimu ya uhuru) ”. Na pia kinafichua wazo la Papa wa Ujerumani kuhusu uchumi na fedha, ambalo limewavutia baadhi ya wasomi wa kilimwengu kama vile Marcello Pera au Massimo Cacciari au “mcha Mungu asiyeamini Mungu” kama vile Giuliano Ferrara, na kuwa marejeo kwa wale ambao wana imani, kwa ufafanuzi wa “Ratzingerian Marxists” umetumika.

Maneno ya baadaye ya Pennisi
Hoja, ya mwisho, ambayo pia ilisisitizwa na Askofu Mkuu Michele Pennisi, wa Monreale, katika maneno ya nyuma aliyotia saini ambapo anatoa mwaliko kuwa: “Baada ya uamuzi wa kinabii ya Papa Benedikto kuacha kulitumikia Kanisa la ulimwengu wote, ni muhimu kuanza kutafakari kutoka hatua ya mtazamo wa kitaalimungu na kisheria juu ya hali ya Papa wa Roma ambaye anaacha kutekeleza huduma ya Petro.”

 

Papa Benedikto XVI. Mafunzo, upapa na baadaye

 

01 March 2023, 10:52