Papa Francisko amekutana na Waziri Mkuu wa Lebanon:mada ni utulivu
Na Angella Rwezaula, - Vatican.
Baba Mtakatifu Francisko, Alhamisi tarehe 16 Machi 2023, amekutana na Waziri Mkuu wa muda wa Lebanon, Bwana Najib Mikati, na wasindikizaji wake. Habari hizo zimetolewa katika taarifa kwa vyombo vya habari kutoka Ofisi ya Habari ya Vatican na msemaji wake na kwamba, baada ya mkutano na Papa mkuu wa serikali ya Lebanon alikutana pia na Kardinali Pietro Parolin, Katibu wa Vatican akisindikizana na Askofu Mkuu Richard Gallagher, Katibu wa Mahusiano na Mataifa na Mashirika ya Kimataifa.
Wasiwasi kwa hali ya Walebanon
Wakati wa mazungumzo yao kwa mujibu wa taarifa ni kwamba wameonesha wasiwasi wa Vatican kuhusiana na hali ngumu ya kijamii na kiuchumi ambayo idadi ya watu wa Lebanon wanapitia, iliyochochewa na mkwamo wa kitaasisi ambao nchi hiyo inajikuta ndani yake yenyewe, ambayo inangojea kwa haraka uchaguzi wa Rais mpya wa Jamhuri hiyo.
Umuhimu wa kuishi pamoja kwa amani kati ya imani tofauti
Zaidi ya hayo, taarifa imebainishwa, kwamba katika kusisitiza umuhimu wa uwepo wa lazima wa Wakristo huko Lebanon na Mashariki ya Kati yo, hitaji lilithibitishwa tena la kuishi pamoja kwa amani kati ya Walebanon wa imani tofauti na kuimarishwa ili kuhakikisha amani na utulivu pia katika kanda nzima
Zawadi
Baba Mtakatifu Francisko wakati wa kupeanda zawadi kama utamaduni, kwa mujibu wa taarifa ni alimpa Waziri Mkuu kazi ya shaba yenye jina la “Upendo wa Kijamii", inayoonesha mtoto akimsaidia mwingine kuamka, yenye maandishi “ Kupenda kusaidia; na baadhye hati za kipapa kuanzia na Ujumbe wa Amani wa mwaka huu; Hati kuhusu Udugu wa Kibinadamu na kitabu kuhusu Statio Orbis cha mnamo tarehe 27 Machi2020, kilichohaririwa na LEV.
Na kwa upande wa Waziri Mkuu alimpatia Papa kifaa cha kuwekea maji ya baraka iliyochongwa kwa jiwe na picha ya Mama wa Mateso.