Mwakilishili wa Vatican ameacha nchi ya Nicaragua
Monsinyo Marcel Diouf,aliyekuwa na majukumu ya Ubalozi wa Vatican huko Managua nchini Nicaragua amehamishiwa huko Costa Rica.Kufungwa kwa makao ya kidiplomasia ya Vatican yametokea kutokana na maombi ya Serikali ya
Vatican News.
Tarehe 17 Machi 2023, Mwakilishi wa Vatican nchini Nicaragua Monsinyo Marcel Diouf, aliacha nchi hiyo na kuhamishiwa huko Costa Rica. Kufungwa kwa makao ya kidiplomasia ya Vatican nchini humo yamefuatia kutokana na kuombwa na serikali ya Nicaragua mnamo tarehe 10 Machi 2023.
Kuwaaga wanadiplomasia wengine kabla ya kuondoka
Ulinzi wa Makao ya Ubalozi wa Vatican na mali yake ilikabidhiwa, kwa mujibu wa Mkataba wa Vienna wa Mahusiano ya Kidiplomasia, kwa Jamhuri ya nchi ya Italia. Na kabla ya kuondoka Monsinyo Diouf aliwaaga wawakilishi wa Kidiplomasia waliyoidhinishwa nchini Nicaragua kutoka Umoja wa Ulaya, Ujerumani, Ufaransa na Italia.
18 March 2023, 14:18