Tafuta

2023.02.28:Miili ya anga iliyopewa majina ya wanaastronomia wa Kijesuit na Papa 2023.02.28:Miili ya anga iliyopewa majina ya wanaastronomia wa Kijesuit na Papa 

Papa na Wajesuit watatu watoa majina manne ya Miili ya sayari ndogo!

Mizunguko midogo katika anga imepewa majina kwa heshima ya Papa Gregori XIII,zamani aliitwa Ugo Boncompagni na mapadre watatu Wajesuit,Johann Hagen,Bill Stoeger na Robert Janusz,wote wanahusishwa na utaalamu wa masuala ya sayansi mjini Vatican.Majina rasmi yalitangazwa na Jumuiya ya Kimataifa ya Astronomia.

Na Angella Rwezaula; - Vatican.

Wanaitwa 562971 Johannhagen, 551878 Stoeger, 565184 Janusz na 560974 Ugoboncompagni ambayo ni majina ya Sayari ndogo nne zilizobatizwa kwa majina ya wanaastronomia watatu wa kijesuit wa  Vatican na Papa Gregori XIII (Ugo Boncompagni) aliyeishi karne ya XVI na ambaye anadiwa kufanya marekebisho ya kalenda (ambayo baadaye iliitwa ya Gregoriana) na mwanzo wa mapokeo ya wanajimu na wajumbe wa kipapa. Wanaastronomia wa Kijesuit ambao wamepewa majina ya sayari ndogo Johann Hagen, ambaye alikuwa mkurugenzi wa Vatican wa utafiti  wa anga kuanzia 1906 hadi 1930, Bill Stoeger, (1943-2014), mwanakosmolojia (kitengo fulani cha astronomia, elimu ya muundo na ukuzi wa maarifa ya dunia) na Mtaalimungu, na Robert  Janusz, ambaye kwa sasa ni mhudumu wa elimu ya Sayari, wa Vatican. Majina manne ya wanaastronomia maarufu yalichapishwa na Jumuiya ya Kimataifa ya Astronomia katika taarifa yake hivi karibuni mnamo tarehe 7 Februari 2023.

Wanaastronomia watatu wa Kijesuit na Papa Gregory XIII
Wanaastronomia watatu wa Kijesuit na Papa Gregory XIII

Wanaastromia na Wajesuit

Zaidi ya wanaastonomia  thelathini leo hii kuna jina la Wajesuiti wengi. Miongoni mwao Padre  Christopher Clavius, aliyeagizwa na Papa Gregori XIII kufanya kazi kwenye mpango  wa kalenda  yake inaitwa 20237 Clavius ​​​​ na Padre Giovanni Battista Riccioli (1598-1671) ambaye aliendeleza mfumo wa utaratibu wa majina ya mwezi ambao bado unatumika hadi leo; “Bahari ya Utulivu” inayojulikana sasa ambayo Apollo 11 ilitua, kwa mfano, ilipewa  jina lake. Kwa kuwa Wajesuit waliosafiri sana katika karne nyingi, kuna wanaastrominia wengine wanaowakilisha kutoka sehemu mbalimbali za dunia, kama vile Ufilipino (4866 Badillo), Paraguay (6438 Suarez), China (31124 Slavicek), Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (23443 Kikwaya)  na Argentina (2490 Bussolini). Wanaastronomia wengine kadhaa wametajwa na wanaastronomia wa  Vatican miongoni mwao ni pamoja na 302849 Richardboyle, 119248 Corbally, 14429 Coyne, 4597 Consolmagno, 23443 Kikwaya na 11266 Macke.

Elimu ya Anga
Elimu ya Anga

Mchakato wa kutoa jina la mizunguko midogo ya sayari

Kulingana Umoja wa Kimataifa wa Astronomia, ugawaji wa jina fulani kwa sayari ndogo hufanyika kupitia mchakato ambao, katika hali nyingine, unaweza kudumu miongo kadhaa. Wakati sayari mpya ndogo inagunduliwa, inapewa jina la majaribio, kulingana na tarehe ya ugunduzi wake. Mzingo wa kitu unapoamuliwa hivi kwamba nafasi yake inaweza kutabiriwa kwa uhakika katika siku zijazo za mbali, kwa kawaida baada ya kuzingatiwa mara nne au zaidi inapokaribia Dunia, basi hutolewa namba ya uhakika, iliyotolewa kwa mfululizo na Kituo cha Utafiti cha Sayari (IAU). Kwa wakati huo mgunduzi wake anaalikwa kupendekeza jina. Pia kuna pendekezo  kwa hili kwamba: Hakuna majina ya wanyama au majina ya kibiashara yanayoruhusiwa, na majina ya watu binafsi au matukio yanayojulikana hasa kwa sababu za kisiasa au kijeshi hayawezi kutumika hadi miaka 100 baada ya kifo cha mtu binafsi au tarehe ya tukio. Haki za kumtaja, basi, haziwezi kununuliwa. Majina yanayopendekezwa yanahukumiwa na jopo la wanaastronomia wa kitaalamu kumi na tano kutoka duniani kote wenye maslahi ya utafiti kuhusiana na sayari ndogo na vimondo.

Wanaastromonia wa Vatican watoa majina ya mizungungo midogo ya sayari
01 March 2023, 09:19