Katika miaka 10 ya Papa Francisko:Wanawake zaidi wanafanya kazi Vatican!
Na Gudrun Sailer – Vatican.
Katikamiaka kumi iliyopita, idadi ya wanawake walioajiriwa Vatican imeongezeka kwa kiasi kikubwa hadi kufikia 1,165. Idadi ya wafanyakazi wa kike na idadi yao ya wafanyakazi haijawahi kuwa kubwa hapo awali, kulingana na uchunguzi wa Vatican News na mamlaka husika ya Vatican. Idadi ya wanawake katika nyadhifa za uongozi wa Vatican pia imeongezeka chini ya Papa Francisko. Hivi sasa kuna wafanyakazi wa kike 1,165 wanaofanya kazi kwa Papa, ikilinganishwa na 846 pekee ya mwaka ambao Papa Francisko alichukua madaraka mnamo mwaka 2013. Asilimia ya wanawake katika jumla ya wafanyakazi wa Vatican kwa hiyo ilipanda katika nafasi ya sasa ya papa kutoka chini ya asilimia 19.2 hadi asilimia 23.4 leo hii. Takwimu hizi zinarejea vitengo viwili vya utawala kati ya mahali Patakatifu na serikali ya mji wa Vatican kwa pamoja.
Ongezeko la wafanyakazi wanawake Vatican
Ongezeko la wafanyakazi wa kike linaonekana zaidi ikiwa mtu atatazama kwa upande wa patakatifu yaani, Curia Romana. Hapa, idadi ya wanawake imeongezeka kutoka asilimia 19.3 hadi 26.1 katika kipindi cha miaka kumi iliyopita. Hii ina maana kwamba zaidi ya mfanyakazi mmoja kati ya wanne katika mahali patakatifu sasa ni mwanamke, kwa takwimu kamili 812 kati ya 3,114. Katika kiwango cha mishahara cha kiwango cha hatua ya kumi kinachotumika Vatican, wanawake wengi katika Curia Romana wamepatikana kwa miaka mingi kwenye hatua ya sita na saba. Kwa hivyo wanafanya taaluma ambazo kwa kawaida huhitaji digrii ya kitaaluma, kama vile wanasheria, wakuu wa idara, watunza kumbukumbu au wataalamu wa utawala. Mnamo 2022, asilimia 43 ya wanawake walioajiriwa katika Curia Romana walifanya kazi katika ngazi ya sita na saba.
Makatibu wasaidizi wengi ni wanawake
Wakati huo huo, wanawake wamepanda mara kwa mara hadi ngazi ya mtendaji, ambayo inazidi kiwango cha mishahara cha hatua kumi. Leo hii wanawake watano wanashikilia cheo cha katibu masaidizi na mmoja katika cheo cha katibu kwenye Kiti Kitakatifu. Makatibu na makatibu wa wasaidizi ni ngazi ya pili na ya tatu ya usimamizi katika mamlaka nyingi za curia Romana na ni sehemu ya timu ya usimamizi pamoja na Mwenyiti, yaani mkuu wa mamlaka; ngazi zote tatu hujazwa kwa kuteuliwa na Papa. Katika Baraza la Kipapa la Kuahamasisha Maendeleo Fungamani ya Binadamu, Papa Francisko alimteua katibu mwanamke kwa mara ya kwanza mnamo 2021, ambaye ni Sr. Alessandra Smerilli wa Italia. Ni wadhifa wa juu zaidi kuwahi kushikiliwa na mwanamke katika mahali Patakatifu. Makatibu wasaidizi mjini Vatican kwa sasa wanafanya kazi katika Baraza la Kipapa la Watawa, la Walei, Familia na Maisha (makatibu wasaidizi ni wawili wa kike), kwa ajili ya Utamaduni na Elimu na katika Sekretarieti ya Vatican. Hata hivyo, mwakilishi huyo Francesca Di Giovanni (70), anayefanya kazi, hivi karibuni ataondoka kwa sababu za umri na nafasi yake itachukuliwa na Padre. Sekretarieti Kuu ya Sinodi pia ina Katibu Msaidizi, ambaye ni Sr. Nathalie Becquart, mtawa wa kifaransa, ikumbukwe kwamba Sinodi pia si sehemu ya Kiti Kitakatifu (katika kitengo cha uchunguzi wa takwimu).
Ilichukua muda kurudisha nafasi ya wanawake katika uongozi
Kihistoria, uteuzi wa wanawake wataalam katika ofisi za juu za Curia Roman ulianza na Papa Paulo VI. Katika upapa wake, alikuwa ni Rosemarie Goldie wa Australia ambaye alifanya kazi katika Baraza la Kipapa la Walei, kuanzia 1967 hadi 1976 kama mmoja wa makamu wawili wa Baraza hilo. Baada ya mapumziko marefu, hapakuwapo na mwanamke hadi 2004 ambapo Mtakatifu Yohane Paul owa Pili alimteua katibu msaidizi aliyefuata Sr. Enrica Rosanna katika Baraza la Kipapa la Mashirika ya kitawa. Chini ya Baba Mtakatifu Francisko, kwa hiyo uteuzi wa wanawake katika nafasi za uongozi umeongezeka, lakini bado umebaki katika kiwango cha chini; chini ya asilimia tano ya majukumu yote ya uongozi katika Curia Romana kwa sasa ambayo yamekabidhiwa wanawake, na kwa sasa hakuna Mwenyekiti yoyote wa Baraza la Kipapa ni mwanamke. Lakini mchakato umewekwa katika maandishi ya msingi ya mageuzi ya Curia Romana kwenye katiba ya Praedicate Evangelium(2022), ambapo Papa Francisko aliwebainisha kwamba katika siku zijazo walei na hivyo hata wanawake pia wanaweza kuongoza mabaraza kuwa wenyeviti au marais.
Nafasi zilihifadhiwa makardinali, maaskofu na mapadre
Hapo awali, nafasi hii ilihifadhiwa kwa makadinali na maaskofu wakuu. Katika mahojiano ya mwezi Desemba mwaka jana, Papa Francisko alitangaza nia yake ya kumteua Mwenyekiti wa kwanza mwanamke katika takriban miaka miwili. Katika mji wa Vatican, ambalo ni taasisi tofauti ya kiutawala kutoka serikali ya Vatican, Papa Francisko aliteua wanawake wawili kushika nyadhifa za juu katika miaka kumi ya upapa wake. Hawa ni Barbara Jatta, mkurugenzi wa Makumbusho ya Vatican mwaka 2016, na Sr. Raffaella Petrini, katibu wa mambo ya jumla ya Vatican 2022. Ingawa walei walikuwa wakiongoza Mabaraza ya Vatican kila wakati, mtawa wa Kiitaliano aliweza kuchukua nafasi ya askofu katika serikali hii.
Kitabu cha Papa ebu tuote ndoto
Wakati huo huo, asilimia ya wanawake walioajiriwa Vatican ilidumaa karibu asilimia 19 wakati wa Papa Francisko. Kwa hiyo, maendeleo katika Kiti Kitakatifu pekee yanawajibika kwa ongezeko endelevu la wanawake Vatican. Kwa ujumla, wafanyakazi katika mahali patakatifu wanashikilia kazi zenye sifa zaidi kuliko katika mji wa Vatican. Wanawake wengi wamepangiwa ngazi ya nne za mshahara; ambao wanafanya kazi, kwa mfano, kama wasaidizi wa mauzo au, kwa wanaume, kama walinzi katika Makumbusho ya Vatican. Kuhusu nafasi za uongozi, Papa Francisko sio tu ameweka baadhi ya viongozi wanawake Vatican, lakini pia amewateua wengine kwenye nyadhifa ambapo wanaweza kushawishi Vatican huku wakidumisha uhuru wao. Yeye mwenyewe aliandika haya katika kitabu chake Let us Dream. Kwa hivyo, Papa Francisko kwa mfano alikuwa papa wa kwanza kuwateua wanawake kama "washiriki" wa ofisi za matibabu, hatua ambayo haikuzingatiwa kwa kiasi kikubwa. Hadi wakati huo, ni makadinali tu na baadhi ya maaskofu walikuwa washiriki wa “mabaraza ya kimapokeo. Wajumbe pamoja na wakuu na makatibu wana haki ya kupiga kura katika mkutano mkuu wa mwaka.
Katika mchakato wa kuwachagua maaskofu yumo mwanamke
Baraza la Uchumi, linalojumuisha wajumbe 15, kwa sasa linajumuisha makadinali wanane na walei saba, sita kati yao ni wanawake, akiwemo Mwingereza Leslie Jane Ferrar, aliyekuwa Mweka Hazina wa Mfalme Charles wa Wales. Mnamo mwaka 2019, Papa Francisko aliteua wakuu saba watawa wa kike kwa ajili ya Baraza la Kipapa la Mashirika ya Kitawa, Taasisi na vyama vya kitume kwa kishindo kimoja. Mnamo mwaka 2022, aliwateua wanawake wawili watawa na mlei kuwa washiriki wa Baraza la Kipapa la Maaskofu, ambapo wanashiriki katika mchakato wa kuwachagua Maaskofu wa Kanisa zima, pamoja na Makardinali na Maaskofu ambao ni washiriki wa Baraza hilo kama walivyo.
Roma iwe kielelezo cha Kanisa la ulimwengu kwa viongozi wanawake
Katika kipindi cha miaka kumi ya Upapa, Papa Francisko ameongeza uwepo, mwonekano na ushawishi wa wanawake mjini Vatican. Mara kadhaa, hata hivyo, alionya dhidi ya kuona kazi ya wanawake katika Kanisa na vile vile katika Vatican kwa mtazamo wa kiutendaji. Katika kitabu cha "Let us Dream", yaani 'ebu tuote', Papa Francisko alielezea kuwa ni changamoto kwake "kuunda nafasi ambapo wanawake wanaweza kuchukua uongozi kwa njia ambayo itawawezesha kuunda utamaduni na kuhakikisha kuwa wanathaminiwa, wanaheshimiwa na kutambuliwa". Kwa kuweka njia ya kuwapendelea wanawake, Papa Fransisko hatimaye anataka Roma iwe kielelezo cha Kanisa la ulimwengu mzima katika suala hili.